Fred Mpendazoe akamatwa kwa tuhuma za kumiliki gari la wizi


Moseley

Moseley

Senior Member
Joined
Jul 10, 2010
Messages
186
Likes
15
Points
35
Moseley

Moseley

Senior Member
Joined Jul 10, 2010
186 15 35
Sadick Mtulya

ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chadema, Fred Mpendazoe janaalipatwa na msukosuko wakati alipokamatwa na askari wa Jeshi la Polisi ambao walidai kuwa alikuwa anamiliki na kutumia gari la wizi, tukio ambalo amelielezea kuwa lilipangwa kwa lengo la kumchafua.

Mpendazoe, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi huo wa ubunge kwa njia ambayo ameielezea kuwa ilijaa ukiukwaji wa sheria, alihojiwa na polisi kwenye kituo cha Buguruni kwa takriban saa mbili kabla ya kuachiwa bila ya masharti.


Mpendazoe, mmoja wa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya ufisadi, alikamatwa jana majira ya saa 3:30 asubuhi eneo la Uwanja Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na diwani wa Chadema wa Kata ya Segerea, Azuri Mwamboji pamoja na Buhari Mgonyezi ambaye aligombea udiwani wa Kata ya Kinyerezi.


Hata hivyo, Mpendazoe, ambaye alihama CCM mapema mwaka huu wakati akiwa mbunge wa Jimbo la Kishapu na kujiunga katika Chama cha Jamii (CCJ) na baadaye Chadema, aliachiwa majira ya saa 5:44 asubuhi na maafisa upelelezi wakamueleza kuwa wataendelea na uchunguzi.

"Kwa kuwa namba zako za simu umetuachia, wewe nenda. Sisi tutatimiza wajibu wetu wa kuendelea na uchunguzi. Hatua tutakayofikia tutakufahamisha,'' alisema afisa upelelezi mmoja.


Mpendazoe amefungua kesi Mahakama Kuu kupinga matokeo ya ushindi wa Dk Makongoro Mahanga kwenye Jimbo la Segerea, baada ya zoezi la kuhesabu kura kuingiwa na dosari kubwa zilizocheleweshwa kutangazwa kwa matokeo.

Hata hivyo, Dk Makongoro ameshateuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira.

Mpendazoe anatuhumiwa kumiliki na kutumia gari la wizi aina ya Toyota Corona, lenye rangi nyeupe ambalo inadaiwa liliripotiwa kuibwa tangu Juni mosi, 2010.

Lakini mbunge huyo wa zamani wa Kishapu aliiambia Mwananchi jana kuwa tuhuma hizo zimelenga kumchafua na kwamba ni hujuma.

"Askari walinikamata kwa nguvu kubwa, hadi kufikia hatua ya kutishia kutumia silaha endapo ningeendelea na msimamo wangu wa kutaka kujieleza... sisi ni raia na katika mazingira haya inabidi tusaidiwe,'' alisema Mpendazoe ambaye aliruhusiwa kuondoka na gari hilo.


Alifafanua kuwa tukio hilo lilipangwa kwa makusudi na kusisitiza kuwa gari hilo ni lake na amekuwa akilimiliki tangu mwaka 2007.

"Hadi sasa polisi hawajaniambia ni mtu gani aliyefungua mashtaka haya (ya kudai kuibiwa gari hilo). Hii ni hujuma kutoka kwa watu ambao hawanitakii mema pamoja na dola kuendelea kunikandamiza. Gari nimelitumia katika kipindi chote cha kampeni zilizopita za uchaguzi mkuu,'' alisema.


"Jana (juzi) tu, nilikuwa nalo kituo cha polisi cha Sitakishari, Ukonga nilipokuwa nimekwenda kuomba kibali cha kufanya mkutano wa harambee ili kuwaomba wananchi kunichangia fedha kwa ajili ya kuendeshea kesi niliyofungua kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Makongoro.''


Hata hivyo, Mpendazoe alisema kuwa polisi walimnyima kibali hicho na kulalama kuwa eneo alilokuwa amekusudia kufanya mkutano ndilo aliloruhisiwa Dk Mahanga wiki iliyopita kufanya mkutano wa kuwashukuru wakazi wa Segerea kwa kumchagua.

Mpendazoe pia alidai kuwa wiki iliyopita alitumia gari hilo kwenda kituo kikuu cha kati cha polisi kuomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara.


"Ajabu nyingine gari hili hili, wiki iliyopita nilikuwa nalo... mbona hawakunikamata,'' alihoji Mpendazoe.

Alikwenda mbali na kusema: " Kulingana na mazingira haya, hisia zangu ni kwamba hizi ni hujuma na demokrasia inaaza kukandamizwa.''

Kamanda wa Polisi Ilala, Faustine Shilogile hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa maelezo kuwa hakuwa ofisini.


"Nitafute baadaye; kwa sasa sina taarifa kamili na muda huu (saa 6:30 mchana) nipo njiani natoka uwanja wa ndege.... naenda hapo kituoni,'' alisema.

Alipopigiwa simu baadaye, hakupokea.


Source: Mwananchi
 
manenge

manenge

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2008
Messages
280
Likes
5
Points
0
manenge

manenge

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2008
280 5 0
Hizo ni gharama za kuingia upinzani. Hata hivyo Mungu ni mkubwa kuna siku yatafikia tamati. lets keep on praying
 
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Messages
20,562
Likes
1,583
Points
280
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2007
20,562 1,583 280
mbona hawalikamati JIZI namba moja lililoko pale MAGOGONI...jizi la kura tena mchana kweupe
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
27,247
Likes
30,527
Points
280
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
27,247 30,527 280
Tatizo la Askari wetu wanakubali kutumiwa kukandamiza na kubambika kesi kwa baadhi ya watu. Kama jambo hili halina ukweli, basi badala ya kumchafua Mpendazoe,litamjenga kwa wapiga kura wake na wananchi wengine maana nao wanakumbana sana na tatizo hilo la kubambikiwa makesi kila siku.
Tusubiri hatima ya kesi yake ya kumn'goa Ubunge yule naibu waziri.
 
Nyambala

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
4,470
Likes
30
Points
135
Nyambala

Nyambala

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
4,470 30 135
Haya mawazo ya kikomunisti sijui yatakujatoka lini vichwani mwa watu wa serikali ya bongo!
 
kaburunye

kaburunye

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2010
Messages
675
Likes
8
Points
0
kaburunye

kaburunye

JF-Expert Member
Joined May 12, 2010
675 8 0
Jeshi la polisi lisikubali kutumiwa na wanasiasa. Mtatuingiza kwenye matatizo mnapoanza uonevu na kunyanyasa raia wasio na hatia wakati wahalifu wakuu mafisadi wala hawaguswi.
 
S

Somi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2009
Messages
868
Likes
347
Points
80
S

Somi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2009
868 347 80
Hawa polisi badala ya kwenda kulinda doria kule maeneo wanapouwawa raia kama kibondo, malagarasi ,ngara n.k. Wanamkamata mpendazoe kwa kutumia vitisho vya silaha hii inadhihirisha hawa polisi wengi wao wapo ktk lile kundi tunalopiga vita la mafisadi
 
sulphadoxine

sulphadoxine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
2,264
Likes
12
Points
135
sulphadoxine

sulphadoxine

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
2,264 12 135
Polisi wa bongo wanamatatizo sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
3,849
Likes
29
Points
145
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
3,849 29 145
jamani njaaaaaaaa ni hatari sana hasa kwa hawa askari wetu ukiwa na hela wanakuabudu ka mungu sijui yataisha lini labda baada katiba mpya
 
Jambazi

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Messages
16,253
Likes
15,357
Points
280
Jambazi

Jambazi

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2014
16,253 15,357 280
Hizi tuhuma huenda zilikuwa zinaukweli ndani yake....
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
30,599
Likes
17,438
Points
280
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
30,599 17,438 280
Gari ipi Ilikuwa ile mark two box au

Ova
 
Malyenge

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Messages
5,885
Likes
2,164
Points
280
Age
48
Malyenge

Malyenge

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2012
5,885 2,164 280
Yaani tukio la mwaka 2010 bado mnachangia tuu?
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
13,779
Likes
8,516
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
13,779 8,516 280
Now ....Mahanga Chadema ...Mpendazoe CCM ....kama hujajifunza kutokuwa serious sana na siasa za Kibongo unatafuta ugonjwa wa moyo siku moja ....
 

Forum statistics

Threads 1,235,987
Members 474,928
Posts 29,242,501