Magonjwa Mtambuka
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 29,637
- 26,044
Wiston Mogha aliyekuwa mwanachama wa ACT Wazalendo KULIA, AKIWA NA Frank Ruhasha kutoka chama cha demokrasia na maendeleo chadema.
Frank Ruhasha kutoka Chadema alisema amekuwa katika chama hicho kwa zaidi ya miaka 13 na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika mkoa wa Kigoma ikiwemo ya katibu wa chama hicho wilaya ya Kigoma,mjumbe baraza kuu taifa na mjumbe mkutano mkuu wa chama taifa.
Amesema ameamua kukikimbia chama chake cha mwanzo kutokana na kutokuwa na matarajio ya kushika dola kutokana na aina ya siasa wanazo zifanya kwa sasa.
Aidha Ruhasha ameongeza kuwa kwa sasa kinahitajika chama chenye siasa mbadala ambacho kitatumia upole kusongesha mipango yao na si ukali kwani aina ya siasa kwa kipindi hiki imebadilika hivyo inapaswa pia vyama vya upinzani vitoe mwelekeo tofauti utakao sababisha matokeo mazuri.