Francis Godwin astahili tuzo ya mwaka kuanika mauaji dhidi ya polisi Nyororo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Francis Godwin astahili tuzo ya mwaka kuanika mauaji dhidi ya polisi Nyororo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Digutu Wamunu, Sep 7, 2012.

 1. D

  Digutu Wamunu Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu watanzania wapenda Amani,


  Naandika haya kwa masikitiko makubwa sana baada ya kushuhudia jinsi serikali ya nchi yetu inavyowatafuna wananchi wake hadharani na kudhani kuwa watanzania wote ni mambumbu. Sitapenda kurudia yaliyokwisha kusemwa na watu wengi, taasisi za kutetea haki za binadamu, vituo vya televisheni ambavyo vimefanya mahojiano na mashahidi wa uwazi kabisa, bali mimi naomba nielekeze fikra zangu kwa huyu mwandishi wa habari Francis Godwin, ambaye alikuwa mstari wa mbele kabisa wakati mashambulizi ya kumwua Mwangosi yanaendelea. Bila yeye bila shaka watanzania tungegubikwa na giza nene bila kujua nini kilitokea siku ile, na hawa simba wala watu ( polisi waliohusika kumuua Mwangosi pamoja na serikali) wangekuwa na kazi ndogo sana ya kupindisha ukweli, hata wasingefikia kuunda hii tume ambayo kwa kweli ni ya kihayawani ( kwani hawajui hata wanachokifanya, wako kama maroboti), nasema hivi kwa sababu wao wanatekeleza tu kile ambacho wanaambiwa bila hata kutumia akili zao za kuzaliwa. Kwa sababu hiyo wataelekezwa na serikali hata namna ya kuandika ripoti ya kuwaridhisha watanzania kwa kuwatia changa la macho.


  Fikra zangu kwa Godwin Francis:
  Mwandishi huyu ni mpiganaji wa kweli, ni ujasiri wa hali ya juu na wa aina yake katika kufanya aliyoyafanya, na aliyafanya hayo kwa upendo wa kweli na kwa kusukumwa na moyo wake kuwa sasa asimamie ukweli. Wakati ule Francis Godwin alipokuwa akielezea kwa mara ya kwanza katika yale mahojiano ya channel 10, naamini kila mtanzania aliyekuwa anamsikiliza alishtuka na kuona labda anaota, au labda ni filamu ya kuigiza, kwamba haiwezekani polisi ndani ya serikali ya nchi yetu ya amani ifanye haya, hii si Tanzania yetu tunayoijua ambayo inasifika kuwa ni kisiwa cha amani. Lakini ukweli unabaki kuwa kilichoelezwa na Francis Godwin ni sahihi na ndicho kilichotokea, wote tumeshuhudia picha za kutisha, na hatimaye mwandishi huyu kuanza kusakamwa kwa nia ya kutaka kuuawa na serikali - (kupitia jeshi la polisi) ili kupoteza ushahidi.

  Nina maswali mengi ambayo nashindwa kupata majibu, lakini naamini watanzania mtanisaidia kuyatafakari:

  1. Nini kinachofuata kwa Francis Godwin?

  2. Jee ni nani anayewaza sasa hivi juu ya usalama wa maisha yake?

  3. Kuna akina- Francis Godwin wangapi katika nchi ya Tanzania ambao tunawapoteza kwani watabadili misimamo yao baada ya kuona mateso ya huyu mwandishi ambayo sasa yawezekana anajutia alichokifanya baada ya kukosa msaada na hajui cha kufanya bali ni kusubiri kifo?

  4. Je tunasubiri Francis Godwin auawe ili watanzania na wenye dhamana ya kutetea haki za binadamu ndipo waanza kujipanga na kuishtaki serikali kwa mara ya pili?

  5. Je hatuoni kwamba Francis Godwin ameanzisha njia ya kuanza kufanya mapinduzi ya kweli ambayo si ya kupigana kwa silaha na kuuana, bali ya kufikiria nje ya duara na kuchambua namna ya kuinusuru nchi yetu dhidi ya serikali iliyovuka mipaka katika kuongoza na kulinda wananchi wake?

  6. Wapiganaji wa haki za binadamu - mipaka yenu iko wapi katika hali kama hii mnapoona serikali imegeuka kugeuza wananchi kuwa kitoweo chao.

  Hatujachelewa hata kidogo! Bado tuna nafasi ya kuonyesha busara zetu katika nafasi tulizo nazo, ili kujaribu kumsaidia amiri jeshi mkuu wa nchi hii mheshiwa raisi ambaye ameelemewa na mzigo wa watendakazi dhaifu, na sasa udhaifu unadhihirika kwake kwavile ni msemaji wa mwisho. Tunaamini kuwa mheshimiwa raisi Kikwete ana dhamira njema kabisa na wananchi wake, na kamwe hataki watanzania wafike hatua ya kukosa matumaini na serikali, lakini nadhani tayari ameshachelewa sana kuzuia hilo, kwani tayari watanzania tayari tumekosa amani na serikali ya nchi yetu.

  Ninaamini kuwa tusipochukua hatua ya kuonyeshesha ushirikiano kwa huyu raia mwema aliyejitoa mhanga na kutufumbua macho watanzania wote, kuna uwezekano mkubwa sana wa Francis Godwin kuuawa au kufa katika mazingira ya kutatanisha. Inawezekana isiwe mwaka huu wala mwaka kesho, lakini ni kitu ambacho hawa simba wala watu wana utaalamu nacho sana na tena wa hali ja juu. Pia kwa kutochukua hatua ya kumlinda huyu Francis Godwin tutawafanya watanzania wengine waogope kufanya mambo na kusimamia haki ambapo tunaididimiza nchi yetu kwa kurudisha nyuma kiwango cha maendeleo ya nchi yetu.

  Nawaombeni watanzania wote tusaidiane kufikiri katika hili ili tuyanusuru maisha ya huyu mwandishi aliyejawa na hofu. Tumwosheshe kwa vitendo kuwa tupo pamoja nae, na tunaungana nae katika kupigania ukweli na haki.


  Mwisho naomba niseme kuwa jambo hili kwa sasa linastahili kufanyiwa kazi na kupima dhamira za taasisi mbalimbali kuona kama kweli zipo kwa ajili ya upiganaji kama katiba zao zinavyosema, au zipo kwa ajili ya kupata kipato chao cha kila mwezi na kwa ajili ya kukidhi matakwa ya wafadhili wanaotoa pesa ktk taasisi hizo. Taasisi hizi ni kama:

  1. Twaweza. Kama kungekuwa na uchaguzi wa watu kuchagua nani aongoze nchi na kuleta mabadiliko na maendeleo ya kweli kwa watanzania, Twaweza wangeshika nchi. Hakika hii ni taasisi ambayo si lelemama. Inapata kila aina ya misukosuko lakini bado inasonga mbele. Tunajua kuwa katika harakati za kumwokoa Francis Godwin Twaweza hawahusiki moja kwa moja, lakini hii ni emergency ambayo haina taasisi maalumu ya kushughulikia jambo hili. Lakini hapa tunatafuta nguvu ya pamoja ya kuhakikisha huyu mwwandishi anabaki salama, na awe na Amani kuwa tupo kwa ajili yake, baada ya serikali kushindwa kumlinda na badala yake kugeuka kuwa adui wa huyu mwandishi (kupitia jeshi la polisi).

  2. HakiElimu. Hii pia ni taasisi ilijaa watu makini (proactive) wenye upeo wa kutafakari na kuchambua mambo kwa umakini. Ni vizuri tukaungana na kuwa na msimamo wa pamoja bila kujali objectives za mashirika tunayotoka. Hapa tuangalie busara zetu na tutangulize utu, tukijua kuwa kuwa hatuna serikali.

  3. Policy Forum: Sihitaji kurudia kusema, ila pia kwa umakini wa chombo hiki hebu tutatue hii changamoto na tuonyeshe support kwa huyu kijana ambaye hana mtetezi.

  4. UTPC ; Hiki ni chombo ambacho kwa hakika kilitakiwa kuonyesha uwezo wao ki-professional katika intervention ya hili swala, hasa ikiwa kama nyie kama kitovu cha kulinda haki za waandishi wa habari Tanzania nzima. lakini kama nilivyosema awali – huu si muda wa kulumbana, bali ni kuunganisha nguvu ya pamoja kwa njia ya Amani.


  5. Balozi zote nchini Tanzania zinazopenda kusema mengi kuhusu Uongozi, Utawala bora na uwajibikaji. Sasa zimeshuhudia jambo hili ambalo liko wazi. Tunaomba msaada wao ili kusaidia kuonyesha serikali kuwa kwa kweli imevuta mpaka, na huyu kijana ni evidence ya kutosha kwa mengi machafu yaliyofichwa na ambayo wengi wetu hatujui, ila kwa ujasiri waliotuonyesha hadharani katika kumwua Daudi Mwangosi ni dhahili kuwa wamezoea kuyafanya haya mara nyingi, na wanajua kuwa watanzania watawadanganya na tutawaamini tu. Sitashangaa kupata ripoti yah ii tume iliyoundwa ikisema – Camera ya Merehemu ilitengenezwa na material ambazo zikiwa karibu na bunduki yenye bomu la machozi basi Camera hiyo inalipuka, ndio maana Camera ya Mwangosi ililipuka na kumchana mara moja na kumwumiza vibaya hata askari mmoja ambaye alikuwa akijaribu kumtoa ili asikae karibu na ile bunduki. Lazima watakuja na kioja cha ajabu na lengo lao ni kujisafisha na kuisafisha serikali machoni pa wengi na mbele ya ulimwengu unaowakilisha na hizi balozi. Sasa ombi letu ni kwa hizi balozi ambazo mmeshuhudia yaliyotokea, tusaidieni kuimulika serikali ili ijue kuwa imevuka mpaka.

  6. Vituo vyote vya kutetea haki za binadamu Tanzania zikiongozwa na Legal and Human Rights Centre ( Pamoja na kuishtaki serikali pia ni vizuri mkatoa mfano wa kuigwa katika ku-act katika kunusuru maisha ya huyu si kusubiri hadi afe). Hivi katika utendaji wa kazi zenu huwa mnafanyaje ikiwa serikali imemtishia uhai wa mtu.


  7. NGO's ambazo zinafanya kazi ya kuangalia Uwajibikaji wa serikali (Daraja). Hapa serikali imeshindwa kuwajibika ipasavyo - lakini inataka kuwajibika katika kuwaua watanzania wote ambao wako tayari kuchua maovu yanayofanywa na serikali. Nyie kama shirika mchango wenu ni nini kwa hili? Tena limetokea katika eneo lenu la kazi, na hii ni exception case..... na inahitaji exceptional intervention, je mnamsaidiaje huyu kijana?


  8. Kituo cha televisheni chennel 10. ( Hivi kweli kweli kumhoji Francis Godwin na kumuacha hewani ajijue, kweli mmetenda haki? Huu si wakati wa kulumbana. Sasa mnafanya nini baada kumsaidia huyu kijana ambaye ametazamwa na kusikilizwa na mamilioni ya watanzania, pongezi kubwa kwa kufanya watanzania tujue ukweli, ila tumwangalie tena huyu kijana kwa namna ya pekee. Yale aliyoyasema pale ni makubwa sana na ni kuidhalilisha serikali kupitia jeshi la polisi. Ktika nchi zingine mwandishi huyu angesafirishwa kimya kimya mara tu baada ya kumaliza kutoa ule ushahidi ktk televisheni yenu, ili kulinda uslama wake. Lakini hili halikufanyika. Alitoka nje ya studio zenu akiwa mpweke. Akarudi Iringa, mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio, baada ya kuona harufu ya kifo inamjia. Wasamalia wema wakampa tahadhari. Masikini wa Mungu Francis Godwin alichowaza na kuona kama ni suluhisho la haraka akaamua kutoroka na kukimbia makazi yake.

  Lakini hawa simba wala watu wako nchi nzima. Wala si kazi bubwa kumpata Francis Godwin alipo, wakiamua hata kesho watampata. Pia kwa sasa mapigano si tu kwa simba wala watu (polisi), bali hata yule RC ambaye alishusha kioo pale Nyololo na kumwangalia mwandishi wa habari alivyochoka na hatimaye kupandisha tena kioo chake - sasa kwa hasira anaweza kukodi vijana wavuta bangi wamtafute Francis alipo na wammalize. Pia hata ndugu zake wa yule polisi au rafiki zake wa yule askari aliyemuua Daudi Mwangosi wanaweza kufanya njama zozote. Kumbuka yale magari ya askari waliomkimbiza na kumfuata Francis hadi Kinyanambo. Ile kazi waliyopewa haiwezi kuishia pale.


  Tafadhari watanzania tuwe waungwana na wenye utu kwa hili, ninaamini kwa uwingi wetu na kwa busara tulizonazo tutaweza kulifanyia kazi hili. Tungependa sana kuwa na watanzania wengi wenye moyo wa ujasiri kama Godwin Francis pamoja na marehem Daudi Mwangosi, lakini kwa kutoionyesha jamii ambayo taasisi nyingi zaidi ya nilizozitaja hapo juu, ambazo tunapenda tuwe na nchi na serikali inayowajibika ipasavyo, basi huu ni wakati wa kushikamana na kulifanyia kazi hili. Faida za kumlinda huyu mwandishi ni nkubwa sana kwa taifa letu laaTanzania ambalo kwa sasa wote wanaangalia faida ya kusema ukweli kwa maslahi ya jamii ni nini? Jee ni kuhama mkoa wako ndio kumaliza tatizo, hapana. Kuanzia sasa watanzania wengi wataamua kukaa kimya ili kunusuru maisha yao badala ya kusimamia ukweli. Kama ambavyo Francis Godwin anasema ukiamua kuwa mkweli – jua kuwa kifo ni rafiki yako.

  Nimeandika haya kama mtanzania mpenda amani, mwenye uchungu na yaliyotokea, lakini nashindwa jinsi ya kuwafikishia ujumbe mashirika na taasisi mbalimbali nilizozitaja hapo juu, kwani hata sijui namna ya kuwapata. Hivyo ningeomba wamiliki wa mtandao huu wa Jamii forums mnisaidie kufikisha huu ujumbe. Na ninaamini kuwa mpo kwa ajili ya kusikiliza mawazo ya watu kama sisi katika jamii, na kufanya sauti zetu zisikike katika mamlaka husika. Hivyo naomba kulingana na nafasi mliyonayo mnisaidie kusambaza ujumbe huu katika vyombo vya habari ambavyo nyie mtaona inafaa.

  Nimejaribu sana kufikiria mimi binafsi, nikajiweka katika nafsi ya Francis Godwin, nikapata msukumo wa ajabu ndani ya moyo wangu, ndio maana nimeamua kuandika haya. Mpaka dakika hii bado siamini kwa yale tuliyaona kule Nyololo, kama ambavyo watanzania wengi watakuwa wamejawa na hofu na nchi pamoja na serikali yetu, basi nimeamua kutoa niliyonayo moyoni. Nitaomba mniwie radhi iwapo nimeongea visivyo, ila naomba kila mtu ajaribu kujiweka katika nafasi ya Godwin Francis.

  Asanteni sana.


  Mungu ibariki Tanzania yetu, Mungu ibariki Afrika.

  Tafakari kwa kina....... Chukua hatua sasa yenye kuleta tija.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kifo cha Daudi Mwangosi naona kila dalili badhi ya waandishi wa habari kutoka mji huo wa Iringa kuwa na uwezekano mkubwa sana wa AMA KUTAJIRIKA KWA GHAFLA SANA AU KUTOWEKA KWA GHAFLA SANA KI-WELEDI katika taaluma hii endapo watachgua tu na kujiweka na utayari huo.
   
 3. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  siku chahe zijazo utasikia Godwin Francis ama amejinyonga au amegongwa gari kaaga dunia,hivyo ndivyo itakavyokua kifo chake,jaribuni kukumbuka yule kijana askari wa morogoro wala muda haujapita mwingi watu weshamsahau.
   
 4. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Political asylum (kama nimeiandika sahihi) ingemtoa sana huyu jamaa kwa sasa.
  Wote ulowataja hapo hawawez msaidia zaidi ya balozi.
   
 5. b

  bahatil mselle Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hali ambayo nchi yetu imifikishwa na utawala huu mbovu usiojali maisha ya rai wake, ni ni vizuri mwandishi huyu shujaa asaidiwe kupata political asylum katika balozi za nje haraka iwezekanavyo. Mungu amlinde.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Francis Godwin (mzee wa matukio daima) akiwa na mkewe,
  hii ni baada ya tukio la Kifo cha Daud Mwangosi


  (Unaona T-shirt ya mke wake ikiwa na picha ya Mwangosi
  sare ambazo walikuwa nazo wanahabari katika mazishi.)

  Francis Godwin maarufu kama Mzee wa Matukio Daima ambaye ni mmiliki wa blog moja wapo muhimu hapa nchini, makamu mwenyekiti wa wanahabari Mkoa wa Iringa, na mwanahabari ambaye amebobea katika uwanja wake, anastahili kupata tuzo ya mwanahabari bora nchini mwaka huu katika tasnia ya habari nchini kutokana na ujasiri wake mkubwa usio wa kawaida wa kutoa taswira live za unyama wa jeshi la polisi nchini walipomwua Mwanahabari maarufu nchini Daud Mwangosi.

  Ujasiri wa Francis Godwin wa kujituma, kustahimili na kuondoa hofu ya mtutu wa bunduki na mabomu ulifanikiwa kuibua taswira pekee sana zilizoonyesha polisi walivyomwua Daud Mwangosi. Baada ya kushtukiwa walianza kumfuata na akaamua kukimbia, na kadiri ya maelezo yake alifukuzwa na gari ambayo haina plate number toka kijijini Nyororo hadi Iringa mjini alipofanikiwa kuwapoteza katika mitaa ya uraiani.

  Baada ya hapo ndipo tulipoanza kupata mtiririko wa tukuo zima la mauaji hayo. Hata hivyo amekuwa akifuatwafuatwa na wahusika wakiwepo polisi, kutishiwa uhai wake, na kwa usalama wake kuamua kuwa mafichoni. Anataka apate nafasi ya kutoa ushahidi wa tukio la mauaji ya kinyama ambayo polisi walimfanyia mwenyekiti wake Mwangosi.

  Kawaida katika matukio ya mauaji yanayofanywa na polisi wamekuwa wakali na kuhakikisha taswira za matukio hayo hazichukuliwi ili kukwepesha ushahidi wa uhusika wao. Jeshi hili la polisi limekuwa likiendelea na hadaa ya kuwabambikiza Chama cha Chadema kwamba ndicho kinachohusika na mauaji yaanayotokea katika maandamano na mikutano ya chama hicho.

  Habari za awali katika tukio la mauaji ya mwanahabari kijijini Nyororo mkoani Iringa, polisi iliibua habari isiyo na kichwa wala miguu kwamba hayati Mwangosi aliwakimbilia polisi na kushtukia bomu likimlipua. Lakini mtiririko wa picha za tukio zilipoanza kuonekana mitandaoni na vyombo vingine vya habari, waziri Nchimbi katika hadidu rejea za kamati aliyoweka zinaonyesha kukiri kwamba mauaji hayo yamefanywa na polisi wake.

  Matukio mengi ya mauaji yaliliyotokea sehemu mbalimbali nchini yalikosa nguvu ya ushahidi wa picha zilizopigwa katika tukio, ambapo tukio la Nyororo licha ya wengi kupiga picha hizo, huyu alikuwa kifua mbele zaidi kuibua taswiras ambazo hazina utata katika kusoma tukio lilivyoendeshwa na polisi hadi kumwua kinyama hali ambayo inatushangaza watanzania na walimwengu.

  Anastahili tuzo hiyo kwa ujasiri wake kama ilivyotokea kwa Muro ambaye alifanikiwa kutoa taswira za polisi kupokea rushwa, ambaye aliwekewa zengwe la kubambikizwa rushwa na hatimaye Mungu amekuja onyesha wazi hakuhusika na zengwe hilo sasa yuko huru.

  Francis Godwin (Mzee wa Matukio Daima) anastahili pongezi na tuzo pia kama mwandishi, mwanaharakati na mtetezi wa jamii na mageuzi nchi.
   
 7. m

  mwitu JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 857
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  usije ukafanya polisi ccm waanze kumsaka kwa kuwaumbua
   
 8. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi sina tena machozi ya kulia, yaliishia kwa Dr Ulimboka.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mpaka sasa anasakwa tangu muda ule alipotoka Nyororo na sasa ameihama Iringa kwa kuwakimbia, habari ndiyo hiyo, siyo siri ndugu yangu. Tumwombee usalama wake.
   
 10. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,920
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Amen na iwe hivyo
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Nimesikia kupitia Radioni kwamba amehama Iringa kwa sababu ya kufuatwa fuatwa na watu asiowajua hivyo anadhani wanaitaka roho yake. Amekimbia Iringa na hajulikani alipo. Kamanda Kamuhanda anasema wanafahamiana vizuri na huyo kijana angeripoti kwake hizo habari ili Polisi ifuatilie badala ya kuingia mafichoni kwa kuogopa vitisho. Sijui kama angeripoti kwa polisi kwa kuwa anasema hao hao polisi ndio wanamsaka!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unaona, sasa umeibua na kuturudisha kwa kutonesha kidonda kilichanza kupona, jamani mambo haya yanalitia aibu taifa. Tukio la Nyororo ni mwendelezo wa yale yale ya Dr. Ulimboka na yale ya kutupa jeneza barabarani kule North Mara.
   
 13. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sasa kama picha zimeshaonekana anatafutwa wa nini tena? Sijaelewa
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kimbunga,
  Huyo Kamanda Kamuhanda alikuwa katika tukio la Nyororo, aliombwa na waandishi wengine awaokoe hao waandishi alitia ngumu, na habari zisizorasmi zinasema alipoenda karibu zaidi na tukio ndipo bomu lilipolipuliwa. Je, tutafsiri kwamba ndiye aliyeridhia bomu lilipuliwe au alisogea tu kushuhudia Mwandishi atakavyolipuliwa?

  Wanaomfuatafuata ni hao hao polisi wa Iringa, Kamanda Kamuhanda akiwa ndiye wa juu, wa chini yake watamfuataje kama yeye hakutoa amri hiyo.

  Kumbuka pamoja na kuwapo katika tukio hilo la Nyororo, kamanda huyo alikana jeshi lake kuhusika na mauaji ya Mwangosi.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Chupaku, Polisi hawataki wajulikane kama ndio wauaji, ndio maana tangu awali walikana kutohusika na mauaji hayo, maana yake walitaka kuwabambikikizia Chadema kama ndio waliomwua.

  Huyu mwandishi kwa vyo vyote anachafatutwa ni kupoteza ushahidi kwa vile licha ya picha ana ushahidi wa kushuhudia ambao yeye mwenyewe anaweza kuutoa iwe katika kamati, tume, au mahakama. Polisi wanataka kupoteza ushahidi huo.
   
 16. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu wa majeshi atamlinda,
   
 17. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mungu wa majeshi ana sehemu yake na sisi tuna sehemu yetu, mara nyingi tunamsingizia Mungu hata kwa yale aliyotupa mamlaka kwayo. Imefika sasa watanzania tufanye maamuzi magumu:

  1. Kufanya maandamano ya amani kulaani mauaji na vitisho kwa ndugu zetu wanaoathirika na utawala uliopo.
  2. Kubadili serikali iliyopo madarakani kupitia sanduku la kura
  3.Kupeleka mashtaka ya mauaji katika mahakama za kimataifa, The Hague.
   
 18. B

  Bijou JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Tatizo watanzania timekuwa ni watu aw matukio, nadhani kuna haja KWENYE katiba mpya au katika kipinfi cha mpito, kuwa NA NGO ambayo kazi yake ni kufuatilia matukio NA kutoa update KWA JAMII kuhusu utekelezaji wake NA namna ya kuishughulikia
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  aliponiudhi ni pale walipokuwa wakivutana na cdm kuhusu mchakato wa mazishi ya mwangosi
   
 20. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #20
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Mh, kabla mwaka haujaisha mbona tutasikia mengi sana,
  ya kweli na propaganda ili mradi tu kunogesha mambo...
   
Loading...