Francis Garatwan Diwani: Nitakuwa mwaminifu, mtiifu na mkweli ndani ya CHADEMA siku zote za Uhai wangu na siwezi kununuliwa kama bidhaa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Ngoja niwaeleze wazi, sikuchaguliwa kuwa Diwani ili niugeuze Udiwani huu kuwa Biashara. Heshima niliyopewa na watu wangu wa Nyansurura ni heshima kubwa sana ambayo ni watu wachache sana huipata heshima hii.

Kitendo tu cha kuitwa Mheshimiwa miongoni mwa ndugu, jamaa na rafiki zako ni heshima tosha ukiachilia mbali hizo stahiki zingine.

Kuna watu walipambana kwa gharama na nguvu kazi zao ili Mimi niitwe Mheshimiwa Diwani na wasiwe wao ama ndugu na jamaa zao na kweli nikawa Diwani.

Mnavyonipa hiyo fedha mimi, wao mnawapa nini maana bila wao naamini msingetambua uwepo wangu na huenda hivi sasa ningekuwa kibaka wa kukaba watu mitaani.

Wananchi ndio waajiri wangu. Siwezi kuwapuuza kwa tamaa ya vipande vya sarafu. Nauthamini mchango wao katika maisha yangu, nafahamu na ninatambua vyema waliponitoa mimi.

Nayafahamu yalivyo Maisha ya Nyumbani kwetu nilikozaliwa, pamoja na yote Watu wangu kupitia hii CHADEMA waliamua kunibeba na kunifanya kuwa mtu wa heshima miongoni mwao, nitailinda heshima hii na kamwe siwezi kuwavua nguo.

Nitakuwa mwaminifu, mtiifu na mkweli ndani ya CHADEMA siku zote za Uhai wangu na siwezi kununuliwa kama bidhaa wala siwezi kuhama ndani ya CHADEMA.

Nikishindwa kufanya Siasa ndani ya Chama kutokana na changamoto kadha wa kadha, sitahama kutoka CHADEMA, bali nitabakia kuwa Mwanachama mtiifu wa CHADEMA mpaka siku natangulia mbele za haki.

Eee! Mungu nisaidie!
 
Mwenyezi Mungu akulinde na akusimamie utangulize maslahi ya waliokupa kura badala ya maslahi ya Procurement Officer wa CCM!
 
Muda wake ukifika atawashangaza na mtabaki mkilia na kusaga meno huku mkimtukana na kumkejeli kama kawaida yenu. Hizo kauli ailizotoa kwa mtu timamu ni dhahiri ya kuwa ANAJIUZA.
 
Msiwaamini sana watu kama hao
Hivi chadema ilipata kata ngapi juzi kai ya hizo 77?
 
Back
Top Bottom