Uchaguzi 2020 Fr. Kitima: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na vifo vingi kuliko chaguzi nyingine zote

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Tanzania (TEC), Fr. Charles Kitima ambaye aliwahi kuwa Vice Chancellor wa SAUT amekosoa wizi wa kura na kusema ni dhambi kwa Mungu kwa sababu ni uongo lakini pia inapelekea kuwa na viongozi wabaya. Amesema kwa miaka sita iliyopita, mazingira ya siasa Tanzania yameharibiwa kiasi cha kutoweza tena kuwa mfano wa nchi nyingine kuja kujifunza demokrasia nchini Tanzania.

Amekosoa suala la kuwa na wabunge wengi kupita bila kupingwa kwa wakati huu. Akiitaja hiyo kuwa ni sababu ya vijana wengi kutojihusisha na masuala ya siasa ikiwemo kupiga kura. Hivyo halihuwa ni mbaya na kupata viongozi wasiostahiki.

Aeyasema hayo katika kikao cha TCD ambacho pia amekikosoa kuwa hakuna haja ya maridhiano kwa kuwa hakuna waliokoseana. Hivyo ni jukumu la nchi kuweka mipango ya kusonga mbele na sio kuwa na maridhiano kwa sasa.

Amesema uchaguzi wa 2020 umesababisha vifo vya watu wengi kuliko chaguzi nyingine zote zilizowahi kufanyika nchini Tanzania. Amevitaka vyama kusimamia ilani zao ili kuepuka fujo. Amesisitiza Upendo haki na amani.
Huyo Kitima nimemuona bwege tu bwege tu, kazi kujisifia tu na kujiona ana hoja za maana
 
Kwa hiyo yeye kageuka kuwa msemaj wa Kanisa katoliki? Mbona kuna maaskofu wengi kanisa katoliki ushawahi kuwasikia wanaongea ujinga ambao kila siku anaushadadia huyu padri mwanasiasa! Huyu ni mjinga aliyejificha kwenye Joho! Alete ushidi ni sawa tu na Mwingira yule mzinzi!
Mkuu, unataka kila Fr.aseme ndo uamini anachokisema?
Unaijua nafasi yake ndani ya TEC? na je, majukumu yake ndani ya TEC unayajua?

Fuatilia vizuri historia ya TEC, na waliowahi kushika nafasi aliyo nayo Fr. Charles leo, mmoja wapo ni Fr. alalekuntwa, angalia wakati wake alikuwa anafanya nini then urudi kumhukumu!
 
Acha kumwamini mwandamu anaweza kuwa na hila zake tu! Asitake kutuaminisha kila hisia zake za kijinga zinazosukumwa na chuki ndani yake!
 
👏👏👏👏
 
Yeye Huyo father ameshuhudia vifo vingapi na amezika watu wangapi?

Chaguzi zote ukiacha za mwalimu hakuna hata moja isiyokuwa na dosari za kuibwa kura.

Acheni chuki binafsi walioshindwa 2020 walishindwa kama wagombea wengine kura zao hazikutosha wagombee 2025 mbona nafasi zote zipo wazi hata ya Urais
Mtafute aliyeiloga akili yako
Hivyo tu
 
akina Mdee tuliona wakituonyesha makaratasi tu ya kura bandia, hao watu wengi Kitima aliosema wamekufa, walikufa mkoa upi?

Huyu padre naye ndio maana Kagame anawafunga, kanisa katoliki liliusika sana na mauaji ya Kimbali nchi Rwanda.
Kwa hiyo wewe tatizo lako ni Kanisa, na wala siyo hayo aliyosema padre?
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Tanzania (TEC), Fr. Charles Kitima ambaye aliwahi kuwa Vice Chancellor wa SAUT amekosoa wizi wa kura na kusema ni dhambi kwa Mungu kwa sababu ni uongo lakini pia inapelekea kuwa na viongozi wabaya. Amesema kwa miaka sita iliyopita, mazingira ya siasa Tanzania yameharibiwa kiasi cha kutoweza tena kuwa mfano wa nchi nyingine kuja kujifunza demokrasia nchini Tanzania.

Amekosoa suala la kuwa na wabunge wengi kupita bila kupingwa kwa wakati huu. Akiitaja hiyo kuwa ni sababu ya vijana wengi kutojihusisha na masuala ya siasa ikiwemo kupiga kura. Hivyo halihuwa ni mbaya na kupata viongozi wasiostahiki.

Aeyasema hayo katika kikao cha TCD ambacho pia amekikosoa kuwa hakuna haja ya maridhiano kwa kuwa hakuna waliokoseana. Hivyo ni jukumu la nchi kuweka mipango ya kusonga mbele na sio kuwa na maridhiano kwa sasa.

Amesema uchaguzi wa 2020 umesababisha vifo vya watu wengi kuliko chaguzi nyingine zote zilizowahi kufanyika nchini Tanzania. Amevitaka vyama kusimamia ilani zao ili kuepuka fujo. Amesisitiza Upendo haki na amani.
Huyu mwamba ni Msema ukweli na Mungu amuweke
 
Back
Top Bottom