Kichwamoto
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 3,353
- 4,535
Huyo Kitima nimemuona bwege tu bwege tu, kazi kujisifia tu na kujiona ana hoja za maanaKatibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Tanzania (TEC), Fr. Charles Kitima ambaye aliwahi kuwa Vice Chancellor wa SAUT amekosoa wizi wa kura na kusema ni dhambi kwa Mungu kwa sababu ni uongo lakini pia inapelekea kuwa na viongozi wabaya. Amesema kwa miaka sita iliyopita, mazingira ya siasa Tanzania yameharibiwa kiasi cha kutoweza tena kuwa mfano wa nchi nyingine kuja kujifunza demokrasia nchini Tanzania.
Amekosoa suala la kuwa na wabunge wengi kupita bila kupingwa kwa wakati huu. Akiitaja hiyo kuwa ni sababu ya vijana wengi kutojihusisha na masuala ya siasa ikiwemo kupiga kura. Hivyo halihuwa ni mbaya na kupata viongozi wasiostahiki.
Aeyasema hayo katika kikao cha TCD ambacho pia amekikosoa kuwa hakuna haja ya maridhiano kwa kuwa hakuna waliokoseana. Hivyo ni jukumu la nchi kuweka mipango ya kusonga mbele na sio kuwa na maridhiano kwa sasa.
Amesema uchaguzi wa 2020 umesababisha vifo vya watu wengi kuliko chaguzi nyingine zote zilizowahi kufanyika nchini Tanzania. Amevitaka vyama kusimamia ilani zao ili kuepuka fujo. Amesisitiza Upendo haki na amani.