Fozhou China, Mkutano mkuu wa 44 wa UNESCO July 16-31: Utetetezi wetu Watanzania juu ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere

Unataka tujadili huku ukiuita msimamo wako ndio wa kizalendo. Tukihitilafiana na wewe bado tutakuwa wazalendo kwako? Pili, hivi UNESCO wamekataza bwawa au wanataka tujieleze kwa nini sehemu hiyo ibaki kuitwa urathi wa Dunia? Hatutaki kuulizwa kuhusu jambo ambalo UNESCO ina usemi nalo?


UNESCO lazima wawe matured, kwanza lazima wajue eneo hilo ni mali yetu na sisi ndio tunatakiwa tufaidike nalo kwanza kutokana na mali asili zilizopo hapo, sasa katika 100% ya eneo hilo tumechukua 3% kwa ajili ya maendeleo ya nchi nzima ie 60,000,000 citizens watanufaika kutokana na 3% ya eneo zima,

kama wapo MATURED hawawezi kuuliza swali kama hilo ikizingatiwa 97% ya ardhi tumeiacha kama urithi wa dunia, sasa hakuna haja ya kubishana nao, tuwape maelezo kwanini tumeamua kujenga Bwawa na tuwaambie wachague wao ama kuacha hiyo 97% ibaki kuwa urithi wa dunia au laa. Kwani faida za urithi wa dunia na Bwawa kwetu zinalingana? kwenye urithi tunapata nini na kwenye Bwawa tutapata nini?? Kipi kina faida kubwa kwetu?
 
Kwani kuna madhara gani kwa nchi, iwapo hiyo UNESCO italiondoa hilo eneo la Selous kutoka kuwa hicho kinachoitwa alama za turathi za dunia?
Mkuu bado utalii wetu unategemea USHAWISHI WETU wa kuvitangaza vivutio huko nchi zilizoendelea.....

UNESCO inapoondoa neno hilo katika maeneo yetu ni wazi tutaathirika KIMAPATO....WATALII WATAPUNGUA......

Mji Mkongwe Zanzibar ni eneo moja la TURATHI ZA DUNIA..ona jinsi watalii wanavyotiririka na kutuingizia fedha za kigeni....mkuu hapo hakuna SIASA....kuna BIASHARA YA KIMATAIFA....
 
Mkuu bado utalii wetu unategemea USHAWISHI WETU wa kuvitangaza vivutio huko nchi zilizoendelea....
Sasa mbona Tanzania ina vivutio lukuki vya utalii! Hata hiyo Selous yenyewe ikiondolewa huko kwenye hizo Turahi za dunia, si bado itaendelea kubakia kuwa mbuga/hifadhi ya wanyama kama ilivyo kwa Mikumi, nk!!

Au kuna mipesa mingi ya Wafadhili huletwa kupitia mgongo wa hiyo sifa nini!! Maana Viongozi wetu hugeuka Wazalendo maeneo yenye MNUSO pekee! Tofauti na hapo, huwaoni wakiipambania nchi yao.
 
..inategemea hiyo 3% ina umuhimu / unyeti gani ktk hifadhi nzima ya Selous.

..kwa mfano, moyo wa binadamu ni mdogo kuliko mguu.

..Lakini sote tunaelewa kwamba pamoja na udogo wake, moyo ni muhimu kwa mwili wa binadamu kuliko mguu

Hakuna kitu kama hicho, ni roho mbaya za mabeberu tu, wao hawataki tujitegemee katika nishati ya umeme kwani nishati ni njia moja ya kuikomboa nchi kiuchumi hilo wao hawalitaki, wanataka siku zote tuwe ombaomba kwao, hakuna athari YOYOTE ya mazingira, HEP dam ni kama dyke,

unajenga Bwawa mbele yake unaweka ukuta wenye milango katika milango hiyo ndiyo kuna Runners na maji yakipita katika hiyo milango kwa kasi ndipo hizo runners huzungushwa ili kuzungusha generators na hapo umeme huzakishwa, maji yanaingia katika Bwawa ni diversion kutoka mtoni (main stream), mimi sijafika huko lakini kimsingi mabwawa mengi huwa yapo hivyo na hatuja sikia katika hayo mabwawa mengi kitu kinachoitwa; UHARIBIFU WA MAZINGIRA, ni huku kwetu tu ndio hao mabeberu wametukomalia juu ya kitu hicho, nonsensical.

Swali; ni nani alitoa propasal UN kwamba eneo hilo liwe ni urithi wa dunia???, kumbuka mradi wa kujenga hilo Bwawa ulikuwepo toka utawala wa wajerumani (stiegler) kabla ya propasal kwamba Selous iwe ni urithi wa dunia.---- Fikiria sana hilo swali kabla hujanijibu.
 
Miaka kadhaa baadae chini ya utawala wa kipenzi chetu hayati Magufuli

#TaifaKwanza
#IdumuJMT
Umeandika vizuri ila umekosea huo mstari ulioandika "kipenzi chetu hayati Magufuli"

Naomba mtoa mada usituhusishe sote, aweza kuwa kipenzi chako lakini siyo kipenzi changu.
 
UNESCO lazima wawe matured, kwanza lazima wajue eneo hilo ni mali yetu na sisi ndio tunatakiwa tufaidike nalo kwanza kutokana na mali asili zilizopo hapo, sasa katika 100% ya eneo hilo tumechukua 3% kwa ajili ya maendeleo ya nchi nzima ie ...
Hakika mkuu....

URITHI WA DUNIA unatunufaisha kutuingizia fedha nyingi za kigeni kupitia watalii ,mfano Mji Mkongwe Zanzibar ,Bagamoyo na Kilwa!

UJENZI WA BWAWA LA NYERERE.Pia ni kwa ajili ya kuinua uchumi wetu kwa upatikanaji wa umeme nafuu, wa uhakika na wa kuuza!

Kwa hiyo serikali ya Tanzania iko sahihi zaidi kwa kufanya "TOUGH DECISION MAKING ON WEIGHING SCALE" .

Kubwa zaidi ,chama cha CDU ambacho wabunge wake walipinga sana ujenzi huo ,kwao Ujerumani kunaongoza kwa VIWANDA......VIWANDA ndivyo vilivyoifanya UJERUMANI hivyo ilivyo kwa kuwa taifa tajiri kuliko yote barani ulaya ,la kushangaza ARDHI YA UJERUMANI ni ndogo sana kuliko ya TANZANIA ,kwa hiyo BAIANUWAI yao inaathirika zaidi kuliko yetu.
 
Hakuna kitu kama hicho, ni roho mbaya za mabeberu tu, wao hawataki tujitegemee katika nishati ya umeme kwani nishati ni njia moja ya kuikomboa nchi kiuchumi hilo wao hawalitaki...
Exquisite 👊👍👍😍🙏🙏

Kama dunia inaogopa kiitwacho UHARIBIFU wa mazingira ,basi tusijenge nyumba.....kwani nao ni UHARIBIFU WA MAZINGIRA ....

Wenzetu wa ulaya ,na sisi tungeamua kuishi tu katika MAPANGO ,kuwinda na kurina asali tu..hata KILIMO ni UHARIBIFU wa BAIOANUWAI.....
 
Ni hivi watu wengi wanaandika bila kuujua ukweli.

Ukweli ni kwamba kabla ya mradi wowote mkubwa kutekelezwa lazima kifanyike kitu kinachoitwa Environment Impact Assessment.

Ukweli ni kwamba serikali iliunda team iliyojumuisha maprofesa nguli kufanya Environment Impact Assessment ambapo serikali yetu iliwalipa fedha kufanya kazi hiyo.

Ukweli ni kwamba team hiyo ilifanya kazi hiyo na kuandika ripoti yake ambayo ilieleza kwamba madhara ya kwenye mazingira kama mradi huu ukitekelezwa yatakuwa makubwa sana hivyo wakashauri mradi huu usitekelezwe na wakashauri serikali ijikite kwenye kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ambayo inapatikana mtwara kwani uzalishaji wa umeme kwa kutumia umeme hautakuwa na madhara kwenye mazingira kama mradi wa stiglers gorge.

Sasa bana ripoti hii iliwasilishwa kwanza wizara inayohusika na mazingira ya bwana January. Waziri akakubaliana na ripoti naye akaifowadi Ikulu.

Bwana kilichotokea almanusura huyu Makamba apoteze kazi. Ukweli ni kwamba jiwe alimuita akamtukana sana kwanini amekubaliana na ushauri wa hao maprofesa na kisha akamtupia ripoti yake .

Isingekuwa aibu ya jiwe akifahamu jinsi January alivyomfanyia figisufigisu ya kutengeneza matokeo yaliyomsaidia kumuweka madarakani pale kituo cha Masaki huyu Januari alikuwa afukuziwe mbali.

Sasa twende kwenye hoja, kwa nini serikali yetu inakataa repoti ya timu ya iliyoiunda na kuilipa ifanye kazi na wao wakafanya na wakashauri.

Mbona Serikali hiii hii haitoi vibali vya kuendeleza miradi ambayo environment impact assessment zimeshauri kwamba arhari za mradi ni hasi.? Kuna msemo wa kiingereza unaoheshimika sana unaosema "no research no right to speak" Research imefanyika imeeleza mradi ni mbaya kwenye mazingira watu bila hata kufanya research nyingine wanakurupuka kuukataa ushauri wa wataalamu.

Tusiwalaumu sijui bunge la Ujerumani , mimi binafsi siungi mkono kupangiwa mambo yetu na hao Wajerunani. Ukweli ni kwamba mradi huu ulikataliwa kwanza na timu yetu sisi wenyewe watanzania iliyohusisha maprofesa wataalamu ambao mwisho wa siku kama kawaida ya jiwe ukitoa mapendekezo tofauti na mtazamo wake unaitwa siyo mzalendo au sijui umetumwa na mabepari.

Aina hii ya uongozi ya kukataa mapendekezo ya wataalamu ni mojawapo ya element za utawala wa KIDIKTETA
 
bwawa lisingejengwa milele hata sgr yetu isingekua ya umeme na sijui tungepata wapi chanzo rahisi cha umeme (kwa gharama nafuu)

kwe utawala kuna mambo mengi we jua tuu Raisi ana taarifa nyingi!
 
Majeshi ni propaganda camps to help rulers rule over the citizens

Uzalendo ni conceptya kipumbavu na duniani hapa "uzalendo" umeleta vifo vingi kuliko kitu kingine chochote...
Unaongea maneno mengi kama mtu "uliyepagawa".....

Nani amekwambia HAJIPENDI?!!
Yupi yule ASIYEJIPENDA?!!

Unajipenda peke yako ?!!!

Kila kazi inacommitment......ila commitment zinazidiana......kumlinda RAIS WA NCHI ni commitment kubwa kuliko kazi yangu ya kuuza kahawa huku kwa Mtogole....

Sikushangai kwako wewe ,unaifananisha thamani ya uhai wa Rais wa nchi ya Marekani na uhai wako wewe MKIMBIZI uliye ughaibuni....

Sikushangai wewe kuona kuwa MAJESHI ni ya kipumbavu kwa kuzilinda tawala.....kwako UKOSEFU WA UTULIVU WA TAWALA ZA NCHI(particularly US) ,hakuathiri UTULIVU WAKO NA FAMILIA YAKO huko Marekani ulikokimbilia.

Suala la kulipwa mishahara kwa mtumishi halina maana kuwa KAZI ZOTE ZINAFANANA....halina maana kuwa KAZI YA RAIS wa MAREKANI Joe Biden na wewe "mbeba maboksi wa kiafrika kutoka Tanzania" INAFANANA.

Mzee punguza Stress/Sonona usije ukajinyonga nduguzo wa kichaga kule HAI wakakosa kutumiwa nawe VISENTI....ndio maana haishangazi US NA EUROPE kuongoza kwa "SUICIDE RATES"....maneno yako ya "kupogoma kizwazwa na kindwanye" yanaakisi YALIYOJAA BONGONI mwako.....
 
Hivi hawawezi kuzalisha umeme utokanao na upepo???

Maana pepo zote hizo bado nchi inalia masikini na kukomaa na maji..

Hapo sijataja gesi pia
 
Hivi hawawezi kuzalishs umeme utokanao na upepo???

Maana pepo zote hizo bado nchi inalia masikini na kukomaa na maji..

Hapo sijataja gesi pia
Sawa mkuu....

Mathalani kuweka WIND TURBINES ni ghali sana....hususani hizi nchi zetu za kiafrika....

Tusisahau pia unapoziweka huathiri UZALIAJI WA BAADHI YA NDEGE(birds)......

Na kwa kuwa utahitaji umeme mwingi ,ni lazima uwe na ENEO KUBWA lenye "consistency" ya kiwango kikubwa cha "upepo" ili ufikie malengo yako.....
 
Umeandika vizuri ila umekosea huo mstari ulioandika "kipenzi chetu hayati Magufuli"

Naomba mtoa mada usituhusishe sote, aweza kuwa kipenzi chako lakini siyo kipenzi changu.
🤣🤣Ok mkuu wangu ha ha ha ila "CHETU" huanzia na "mbili"....katika hilo tuko:

1)Jumbe Brown
2)JohntheBaptist
3)Idugunde
4)Mkaruka et al🤣
 
Nimeukubali sana uandishi wako,hasa unapotumia maneno kama Bioanuai,Turathi,Mbuga tengefu.
Naomba unisaidie tafsiri ya maneno,Dhima na Turathi.
 
Ndivyo ilivyo haswa au ni mambo tu ya kwenye makaratasi hayo?.


Ndivyo ilivyo, watu wengi hawajui kwamba utawala wa kikoloni wa wajerumani wao ndio waliplani kujenga hilo bwawa, utawala wa kiingereza haukuwa na nia ya kufuata hiyo plan ya mjerumani kwasababu mbili, 1--- Mjerumani alikuwa hasimu yao, 2--- Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini wa Muingereza baada ya kukabidhiwa na UNO, tulipopata uhuru Nyerere akaufufua huo mpanga wa kujenga hilo Bwawa kama wenzake akina Gamel Abdul Nasser wa Misri (Aswan dam) na Kwame Nkrumah wa Ghana (Akosambo dam ??), nadhani tulishindwa kulijenga kutokana na gharama kubwa wakati huo au mikopo kutoka Banki ya dunia na IMF ilikuwa na masharti magumu sijui!!--- Mabeberu wa zama hizo walijua na bado wanajua kwamba ukombozi wetu MKUBWA wa kiuchumi ni nguvu za umeme hivyo wakatufanyia hila ya kupeleka propasal huko UNO ili kutangaza Selous iwe ni urithi wa dunia ili katika eneo hilo pasifanyike any 'development" kwa kisingizio kwamba eneo hilo ni urithi wa dunia kwa maana hiyo hukutakiwa kujenga hilo bwawa tena!!, unaona hila na ujanja wa mabeberu??!!--- kweli yapo maeneo yanafaa kupata hadhi ya urithi wa dunia lakini sio kwa Selous, walifanya hivyo tu ili Stieglier isijengwe.

Umeme ndiyo maendeleo, wao wenyewe maendeleo waliyonayo yameletwa na umeme, Usafii wa umeme, viwanda ni umeme, mahospitali, majumbani kupikia nk, ni umeme yaani kila kitu wao ni umeme tena mwingi wa bei rahisi sana kuliko sisi, sasa iweje kwetu umeme iwe ni haramu???--- kitu gani kiko nyuma ya sisi tusipate umeme mwingi rahisi wa uhakika???--- lengo wanataka waendelee kutunyonya sikuzote, tuendelee kukodi mitambo yao ya gesi nk, hui ndio unyonyaji wao.
 
Nimeukubali sana uandishi wako,hasa unapotumia maneno kama Bioanuai,Turathi,Mbuga tengefu.
Naomba unisaidie tafsiri ya maneno,Dhima na Turathi.
Shukran mkuu wangu Rodwell🙏

Turathi- Urithi wa vizazi na vizazi

Hatutumii sana neno "turathi" katika URITHI wa mzazi kwa mwanaye/wanawe kwa kuwa HAUTOENDELEA SANA katika vizazi vya "damu yake" mrithiwa ,japo wako pia wanaotumia katika muktadha huo!

Dhima ni "wajibu" kaka....

Shukran!
 
Exquisite 👊👍👍😍🙏🙏

Kama dunia inaogopa kiitwacho UHARIBIFU wa mazingira ,basi tusijenge nyumba.....kwani nao ni UHARIBIFU WA MAZINGIRA ....

Wenzetu wa ulaya ,na sisi tungeamua kuishi tu katika MAPANGO ,kuwinda na kurina asali tu..hata KILIMO ni UHARIBIFU wa BAIOANUWAI.....


✔✔✔✔💯%
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom