Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,078
- 12,750
Ni UNESCO haohao walioanza kujiridhisha kipindi cha utawala wa hayati baba wa taifa mwalimu JKN kuwa ujenzi wa bwawa la kufua umeme kamwe HALITOATHIRI mazingira ya viumbe na uoto wa asili katika pori tengefu la SELOUS!!!
HAWAKUISHIA HAPO
Miaka kadhaa baadae chini ya utawala wa kipenzi chetu hayati Magufuli wakaendelea tena kujiridhisha kuwa UJENZI wa bwawa hilo halitoathiri BAIOANUAI ya eneo lile baada ya Tanzania kujieleza bayana kuwa ni 3% tu ya eneo hilo itakayomegwa kwa ajili ya kufua nishati ya umeme wa maji ambayo Wataalamu wa dunia walijiridhisha kwalo!
KIPI TENA KIMEBADILIKA
Nchi yetu adhimu imeitwa katika mkutano utakaofanyika Fozhou nchini China kujitetea ili PORI TENGEFU la SELOUS lisiondolewe kutoka ALAMA ZA TURATHI ZA DUNIA!!!
KELELE KUTOKA NJE
Walianza wanaharakati wenye mrengo wa siasa za UPINZANI hususani CHADEMA kuukataa ujenzi wa bwawa hilo kwa sababu hizihizi tulizoitiwa huko China.
Baadaye likatokea kundi la wabunge wa CDU bungeni BUNDESTAG(ujerumani) kuupinga mpango wetu wa ujenzi huo.
Ikumbukwe chama cha CDU ndicho chama rafiki cha CHADEMA.
UMEFIKA MUDA
Kama watanzania tuna dhima kubwa ya KULINDA ukweli ulioko na kuyalinda maslahi yetu ya taifa hili adhimu ili tuendelee na ujenzi wa BWAWA LA MWALIMU NYERERE na pia Pori la SELOUS lisiondolewe kutoka TURATHI ZA DUNIA.
Ninamtakia kila la heri Dr.Allan Kijazi na wataalam wetu wengine katika ushiriki wa huo mkutano mkubwa wa 44!
Je, ni yepi mawazo yako ya KIZALENDO ?!!!
#KaziIendelee
#TaifaKwanza
#IdumuJMT