Fozhou China, Mkutano mkuu wa 44 wa UNESCO July 16-31: Utetetezi wetu Watanzania juu ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
Kwa siasa za sasa ambazo JK ndiye dereva, inawezekana wakausimamisha ili kutafuta sifa! Lakini 2025 sijui
Mkuu wangu ,Mradi huo UTAENDELEA.....

Miradi yote aliyoanzisha El comandante hayati kipenzi JPM itamalizika.....

Komredi tumpe nguvu mh.Rais wetu....
 

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,434
2,000
Mkuu wangu ,Mradi huo UTAENDELEA.....

Miradi yote aliyoanzisha El comandante hayati kipenzi JPM itamalizika.....

Komredi tumpe nguvu mh.Rais wetu....
Hakuna mtu simuamini kama JK. Hivi unajua ufisadi katika madini aliuanza yeye akiwa Waziri wa Nishati na Madini? Nchi hii ilisogea kwa vile JPM alimkandamiza JK ingawa baadaye......
 

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,413
2,000
Wakati mwingine sisi Watanzania ni wapuuzi. JPM aliamua kuhakikisha anarudisha hela zilizokuwa zimechukuliwa na mafisadi na kuacha wanyonge wabaki na kidogo walichonacho. Miradi ikaenda kwa spidi ila Watu wakamlalamikia na kumuita majina ya ajabu. Sasa Samia kaingia na gia ya kutowabughudhi mafisadi, watu wakamshangilia, imagine!!!! Leo hii hakuna hela ya kuendesha serikali, akaona wanyonge wajipapase; kilio kama chote. JPM bwana, Mwenyezi Mungu amrehemu huko alipo. Inauma
Kajipange upya!! Unyang'anyi uliofanywa na Magufuli kwa raslimali za watu binafsi siyo kitu chema. Ni wizi na unyama.

Wacha tusue sue kujenga miradi lakini UNYANG'ANYI hapana
 

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,434
2,000
Ni UNESCO haohao walioanza kujiridhisha kipindi cha utawala wa hayati baba wa taifa mwalimu JKN kuwa ujenzi wa bwawa la kufua umeme kamwe HALITOATHIRI mazingira ya viumbe na uoto wa asili katika pori tengefu la SELOUS!!!

HAWAKUISHIA HAPO
Miaka kadhaa baadae chini ya utawala wa kipenzi chetu hayati Magufuli wakaendelea tena kujiridhisha kuwa UJENZI wa bwawa hilo halitoathiri BAIOANUAI ya eneo lile baada ya Tanzania kujieleza bayana kuwa ni 3% tu ya eneo hilo itakayomegwa kwa ajili ya kufua nishati ya umeme wa maji ambayo Wataalamu wa dunia walijiridhisha kwalo!

KIPI TENA KIMEBADILIKA
Nchi yetu adhimu imeitwa katika mkutano utakaofanyika Fozhou nchini China kujitetea ili PORI TENGEFU la SELOUS lisiondolewe kutoka ALAMA ZA TURATHI ZA DUNIA!!!

KELELE KUTOKA NJE
Walianza wanaharakati wenye mrengo wa siasa za UPINZANI hususani CHADEMA kuukataa ujenzi wa bwawa hilo kwa sababu hizihizi tulizoitiwa huko China.

Baadaye likatokea kundi la wabunge wa CDU bungeni BUNDESTAG(ujerumani) kuupinga mpango wetu wa ujenzi huo.
Ikumbukwe chama cha CDU ndicho chama rafiki cha CHADEMA.

UMEFIKA MUDA
Kama watanzania tuna dhima kubwa ya KULINDA ukweli ulioko na kuyalinda maslahi yetu ya taifa hili adhimu ili tuendelee na ujenzi wa BWAWA LA MWALIMU NYERERE na pia Pori la SELOUS lisiondolewe kutoka TURATHI ZA DUNIA.

Ninamtakia kila la heri Dr.Allan Kijazi na wataalam wetu wengine katika ushiriki wa huo mkutano mkubwa wa 44!

Je, ni yepi mawazo yako ya KIZALENDO ?!!!

#KaziIendelee
#TaifaKwanza
#IdumuJMT
Mbona michadema haipatikani katika hili

800C52C8-2599-49A3-9E29-E6938318E21A.jpeg
 

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
659
1,000
Shukran mkuu wangu Rodwell🙏

Turathi- Urithi wa vizazi na vizazi

Hatutumii sana neno "turathi" katika URITHI wa mzazi kwa mwanaye/wanawe kwa kuwa HAUTOENDELEA SANA katika vizazi vya "damu yake" mrithiwa ,japo wako pia wanaotumia katika muktadha huo!

Dhima ni "wajibu" kaka....

Shukran!
Thanks
 

Dr Mabuga 30

Senior Member
May 8, 2021
106
225
Ukubwa wa selous ni km za mraba 54,600, kwa hiyo sehemu iliyotumika ni Kama km za mraba 1600 ni sehemu ndogo Sana naamin wakienda na utetezi imara watashinda lazima...
Sawa mkuu....

Nami nitendee haki, katika hizo hekari 1000 unazosema ,Selous imebakiwa na hekari kiasi gani ?!
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,725
2,000
Ukubwa wa selous ni km za mraba 54,600, kwa hiyo sehemu iliyotumika ni Kama km za mraba 1600 ni sehemu ndogo Sana naamin wakienda na utetezi imara watashinda lazima...

..hoja yako ni sawa na kusema ubongo/moyo ni sehemu ndogo ya mwili wa binadamu hivyo unaweza kuuchezea-chezea vile unavyotaka na hautapata madhara.

..tuwe wakweli kuhusu athari na changamoto za kimazingira zitakazotokea na tujipange jinsi ya kuzitatua.
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
Ukubwa wa selous ni km za mraba 54,600, kwa hiyo sehemu iliyotumika ni Kama km za mraba 1600 ni sehemu ndogo Sana naamin wakienda na utetezi imara watashinda lazima...
Naam dokta....

Tumeshinda kaka....

Utetezi wetu umekubaliwa....

Kongole kwa viongozi wetu wa Serikali sikivu 👊👍👋👋💪💪

#KaziIendelee
#SiempreJMT
#NchiKwanza
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
..hoja yako ni sawa na kusema ubongo/moyo ni sehemu ndogo ya mwili wa binadamu hivyo unaweza kuuchezea-chezea vile unavyotaka na hautapata madhara.

..tuwe wakweli kuhusu athari na changamoto za kimazingira zitakazotokea na tujipange jinsi ya kuzitatua.
😲😲
Utetezi wetu umekubaliwa.....

Siempre JMT
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom