Fowadi wa Tanzania kama janga la umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fowadi wa Tanzania kama janga la umeme

Discussion in 'Sports' started by bemg, Jul 4, 2011.

 1. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  [TABLE="width: 650, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"]Mafowadi wa Tanzania kama janga la umeme-Mwanasport[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: storyheader, bgcolor: #ffffff"]KATIKA kipindi hiki ambacho Watanzania wanaumia na mgao wa umeme, Wabunge wetu wanaokutana kwenye kikao cha bajeti mjini Dodoma wameutangaza kuwa janga la taifa.

  Si mara ya kwanza kwa nchi yetu kukumbwa na majanga ya kitaifa, kumetokea ukame mkali uliowahi kusababisha njaa na hata mvua kubwa za El-Nino zilizosababisha mafuriko.

  Katika miaka ya karibuni, nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na mgao mkali wa umeme, ambao umewasababishia wananchi adha kubwa.

  Sasa wapenzi wa soka wakati huu wakipata uhondo wa Kombe la Kagame wanashuhudia timu zetu za Simba na Yanga zikikabiliwa na ukame wa mabao.

  Suala la upachikaji mabao kwa sasa limekuwa janga la kitaifa kwani klabu zetu na Taifa Stars hazina mtu wa kufumania mabao.
  Simba iliyoanza michuano hiyo kwa kutoka sare ya bila kufungana na Vital'o ya Burundi ilicheza vizuri lakini tatizo likawa umaliziaji.
  Hata hivyo, Jumatano iliyopita, iliishinda Ocean View 1-0 kwa bao lililofungwa na beki Amir Maftah.
  Yanga nayo ilipoanza michuano hiyo, ilifungana 2-2 na El-Merreikh. Mabao yote ya Yanga yalipatikana kutokana na mabeki wa El-Merreikh ya Sudan kujifunga.
  Pia hilo lilidhihirika kwenye michuano ya Kombe la Chalenji mwaka jana kwani beki wa kulia Shadrack Nsajigwa ndio aliifungia Kilimanjaro Stars mabao mengi kwenye Kombe la Chalenji.

  Hilo limethibitishwa na Kocha Mkuu wa Simba, Moses Basena, ambaye ameomba klabu yake imtafutie mfungaji wa mabao.
  Pia gazeti hili lilimkariri kocha wa zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla, Jumanne iliyopita akizungumzia ubutu wa safu za ushambuliaji wa timu za Simba na Yanga.

  Msolla alieleza kuwa suala la kufunga si mtu yeyote anaweza bali ni kipaji maalumu.
  Tatizo hilo sasa limekuwa sugu kwani lilimpa wakati mgumu hata kocha aliyepita wa Taifa Stars, Marcio Maximo na sasa Jan Poulsen.
  Kama ilivyo kwa tatizo la umeme, wadau na makocha wamekosa jibu la kutatua tatizo hili.
  Haya ni matokeo ya nchi yetu kutokuwa na mipango ya muda mrefu katika maeneo mbalimbali.
  Nchi yetu tangu Uhuru ilikuwa na bahati ya kuwa na washambuliaji wa kutisha waliotikisa si Tanzania tu bali Afrika nzima.
  Kila mtu anawakumbuka akina Hemed Seif, John Lyimo, Yunge Mwanansali, Kitwana Manara, Sunday Manara, Gibson Sembuli, Maulid Dilunga, Adam Sabu, Abdalla Kibadeni `King', Mohamed Salim, Peter Tino, Abdalla Burhan, Thuwein Ally, Makumbi Juma na Zamoyoni Mogella.
  Hata katika miaka ya karibuni wamekuwepo wengi tu akina Madaraka Selemani, Mohamed Hussein `Mmachinga', Innocent Haule, Said Mwamba `Kizota', Edibily Lunyamila, Dennise Mdoe, Hilal Hemed, Idelfonce Amlima, Juma Mgunda, Kitwana Selemani, John Makelele, Abeid Mziba, Fumo Felician, Nteze John na Ephraim Kayeta.
  Hapa ndio kazi ya Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inapokuja ya kusaka ufumbuzi wa kitaalamu wa suala hili.

  Kwa kiasi kikubwa Kamati ya Ufundi ya TFF na Chama cha Makocha Tanzania (Tafca) walipaswa kuwa na majibu muafaka ya tatizo hili.

  Tatizo kubwa ni kuwa taasisi hizi zinafanya kazi kisiasa badala ya kuandaa programu ya kutibu tatizo hili kuanzia kwenye ngazi za chini.

  Kunatakiwa kuandaliwa mitaala maalumu shuleni ili kuhakikisha vijana wadogo wanavumbuliwa.
  Tatizo ni kuwa hakuna anayejali na matokeo yake kitu kilichoanza kama tatizo dogo sasa kimekuwa `donda ndugu'.

  Ndio maana si ajabu kuona timu zetu zinatolewa mapema kwenye michuano ya kimataifa na ile ya klabu barani Afrika kwani hazina wapachika mabao.

  Imefika wakati kwa TFF kushughulikia suala hili kama janga la kitaifa kinyume chake litaendelea kutafutana soka letu.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  tatizo la mafowadi nchi hii ni janga la taifa...tatizo hao wakocha wanakazana kuwafundisha wazee mbinu mpya za ufungaji.
  msisitizo unatakiwa kuwekwa kwenye mashule.
   
Loading...