Found a real love when its too late. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Found a real love when its too late.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Causin, Jun 8, 2010.

 1. Causin

  Causin Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wanajf? hope mu wazima.
  Jamani naombeni ushauri wenu kwa hili ninalofanya kama ni sawa au nakosea.

  Mimi ni mdada ambaye bado cjaolewa ila nina mchumba ambae anakaa mbali na mimi sababu ya kazi,yani mikoa tofauti.
  Kampuni ninayofanya kazi nimetokea kuwa karibu sn na kijana mmoja ambaye pia ni mfanyakazi mwenzangu lakini sio ofisi moja,ukaribu umezidi na hatimaye tumejikuta in love,ukweli ni kwamba naweza kusema huyu kaka anajua kupenda, ananiheshimu and he real know how to care for a woman,kitu ambacho i always dream about,yupo tayari kwa lolote na muda wowote nitakaomhitaji hasa kama nina shida,ukweli ni kwamba tumependana sn utafikiri wote tumekutana tukiwa single,wakati hata yeye ana mpenzi wake ambae pia anaishi mbali na yeye.
  Naombeni ushauri wenu kwa hiki ninachofanya,je ni sawa na kama sio sawa nitafanyaje?,ukweli ni kwamba nampenda sana na siko tayari kumpoteza cause he made ma life wonderful,never knew it before.Na ninaomba nieleweke niko na mchumba wangu kwa miaka miwili na nusu sasa na sijawahi kumsaliti kwa mwanaume yoyote zaidi ya huyu.

  I wish i could knew him before,cause its like i found a real love when its too late,hata yeye pia ana apprecite sana for this love.

  Naombeni ushauri,nitaendelea hivi mpaka lini?
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  umeshaongea nae kuhusu hich kipande blue, na yeye hayupo tayari kukupoteza? mapenzi ya mbali ni magumu sana, uongo mwingi/kudanganyana tu...umesham cheat mchumba wako, na huyo kaka nae kam cheat mchumba wae, cjui hao waliopo mbali na nyie inakuwaje tena...mambo mzunguko jamani.
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Shosti you are in a fix i could say that. Mambo kama hayo hutokeaga sana inakuwa kama kipimo cha uaminifu wako kwa mpenzi wako. Ila shida inakuja pale ambapo hujui umchague nani. Lakini pia una uhakika gani kama kweli anakupenda huyo uliyempata wa sasa???
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,521
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  As human beings we are not perfect. Just follow your heart and do it IF you are both serious about your relationship.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Pole sana dada. Na ndio maana siku kadhaa zilizopita nilianzisha mada inayohusiana na hali hii.

  Ndio maana wakati mwingine ni bora kubakia mwenyewe tu kwa kuwa na mtu ni kama unajifungia milango ya fursa. Huu ni mtazamo wangu tu.

  Tatizo jingine kujua ni yupi mwenye mapenzi ya kweli haiwezekani. Labda tungeanza na kuelezea mapenzi ya kweli ndio yepi hayo?
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Lol...Bubu haya mambo ya follow your heart sijui nini wala hayasaidii. Yatazidi tu kumchanganya mwenzio. Single life is the way to go.
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mimi sijaelewa!

  1) Upo in love na nani? (a) mchumbako au huyo wa (b) ofisini?,
  2) kama jibu ni (b) je mchumbako humpendi tena?
  3) Kama unampenda, unataka kutuambia wewe unaweza kuwapenda several men bila tatizo?

  MY TAKE:
  Nyie mnajisikia mnapendana kwa sababu wenza wenu wako mbali, na mnapenda kungonoka, wote wawili mnafikishana. Kwasababu sio wachumba wala hamna commitment zozote, mahusiano yenu yana mipaka, kuna mambo ambayo kila mmoja wenu haitaji kuyafanya/kuyafikiria/kuyatolea maamuzi. Mko kwenye buffer zone, au bulwark area rather. Wote mnakutana kwa raha tu! sio shida. Hamuwezi kugombana......mtagombea nini wakati hamna mambo ya msingi ya kugombea? Kitu pekee kinachowaweka pamoja ni Kula dudu kwa bidii!! hakuna jingine.

  Hakuna Mapenzi wala ndugu yake mapenzi hapo.
   
 8. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Humpendi yule aliyeko mkoani

  haapa umeliwa dada yangu, huyo ndie mwanaume halisi, he knows how to grab your mind, akijilia ndio utaelewa kwanini nakuambia umeliwa

  wewe mgeni wa mapenzi eeh?! Unategemea awe mbali wakati bado hajafaidi tunda, hata ukitaka kwenda Brunei nina uhakika atakupeleka

  hapa bado hujashtuka tu dada mapaka upigiwe king'ora cha zimamoto:pound:

  hapa ushauri wa nini sasa kama hutaki kumpoteza? Umejichanganya

  Ndio umeshamsaliti sasa au maana ya kumsaliti kwako imekaaje dada?

  Kama hauna msimamo hata ukikaa na huyu utakuja kumpata mwingine na utasema hivi hivi, acha umbayu mbayu kuwa na msimamo

  Narudia tena weewe ni mgeni wa mapenzi jfunze kwanza kabla ya kukurupuka au kukurupushwa, utakuja juta ukose wa kumlilia, JF hatupokei vilio vya kizembe bana


  Ushauri wangu: Nakushauri uwe na msimamo na huyo wa mpenzi wako maana hakuna sababu ya msingi uliyotoa kuonyesha kuwa zinamtoa kwenye mahusiano na wewe. Kikubwa wewe ni maimuna wa mapenzi na umeghilibika na huo ukaribu na hizo caring za huto mfanyakazi wako wa karibu ambazo kwa uzoefu wangu ni za muda tu, hazina maisha ya kudumu

  Kama unataka kumuacha huyo aliyeko mkoani toa sababu zenye mashiko:A S-eek:
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,521
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Thank you NN. Mapenzi ya kumfanya mtu ajisikie kiasi hiki "anajua kupenda, ananiheshimu and he real knows how to care for a woman, kitu ambacho i always dream about " ni nadra sana kupatikana katika dunia ya leo. Ukipata bahati ya kuwa na penzi kama hili basi usililazie damu na kubaki na majuto mjukuu katika miaka ya baadaye, NN, ukipata bahati ya kuwa na penzi kama hilo "la kupendana sana" basi utavisikia vitu mwilini ambavyo hujawahi kuvisikia kama hujapata bahati ya kuwa katika penzi la namna hiyo. Mimi naamini kabisa kwamba bado kuna penzi la kupendana sana lakini ni nadra sana kulipata katika dunia ya leo.

  Tayari huyu dada katupa clue juu ya huyu mpenzi wake ni hizi hapa, "ukweli ni kwamba nampenda sana na siko tayari kumpoteza cause he made ma life wonderful,never knew it before" akaendelea "Na ninaomba nieleweke niko na mchumba wangu kwa miaka miwili na nusu sasa na sijawahi kumsaliti kwa mwanaume yoyote zaidi ya huyu."
  Kuna mapenzi megine ukibahatika kuyapata hapa duniani it is very difficult to walk away from that special feeling of being in love.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Duuh Bubu dizaini wewe umebahatika nini kulipata hilo "penzi" la kweli? Kama ni hivyo hongera bana.

  Siku hizi kila mtu msanii. Anakuambia anakupenda wewe halafu hayohayo anamwambia mwingine. Si wanawake si wanaume. Wote wasanii tu. Ndio maana sikubaliani na hii dhana potofu ya kwamba eti wanaume ndio sio waaminifu zaidi. Hayo ni mavi ya ng'ombe tu.

  Mtu yeyote mwenye mapenzi wa kweli kwa mwenzake hawezi kuwa na hisia kwa mtu zaidi ya huyo "anayempenda". Labda mniambie inawezekana mtu "kumpenda" mtu zaidi ya mmoja. Hii inaweza ikawa mada inayojitegemea yenyewe.

  Mimi bado sijajua au kuelewa penzi la kweli ni penzi gani hilo na vigezo vyake ni vipi.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Typical wanawake wa kibongo!

  NO COMMITMENT.
   
 12. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Hapo wewe kaa mkao wa kuliwa~lazima ile kwako hapo. Huyo jamaa yako mpya atakufanyia kila kitu, ukitaka kwenda msalani atakubeba, ukitaka akufulie beki zako huyo bwana atafanya, hata ukitaka pay check yake yote atakupa. Mwisho wa siku ni kwamba yeye amelengeshea kula tunda la kati~karibu kwenye man's universe!.
   
 13. Theodora

  Theodora JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  You must have said the same thing about being in love na mchumba wako, one time...Je, huyu naye akiamishiwa mkoa mwingine u will fall out of love or?

  Wkti mwingine we use excuse of distance to justify our actions. Advise, be true to yourself. I just hope history will not repeat itself, maana wewe na huyo mkaka you have the same story pattern, being in love, wachumba wako mbali etc... If it was distance, ulipaswa ubreak off kwanza na mchumba wako, lkn am sure you wanted to keep your options open. Now its 2 other people disappointed. Just do what you feel is right to you.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,521
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Hahahahahahaha I plead the fifth lol!...Ni kweli siku hizi wasanii katika mapenzi wamekuwa wengi mno ndiyo maana nikasema ni nadra sana kulipata penzi la kweli ukawasikia wapenzi wanaambiana nakupenda sana au akawaambia watu ananiheshimu sana, ananijali, ananithamini etc. Kweli inawezekana hujalijua hilo penzi la kweli lakini likikutokea utasema ahaaa hili ndiyo penzi ambalo BAK aliandika kule Jamii lol! maana utayasikia madudu mwilini ambayo hujawahi kuyasikia maishani mwako, lakini sidhani kama penzi kama hili utalipata kwa Nswia hahahahahaha

   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280


  Sign of someone who's been pussy whipped....Lol
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  spot on Theodora;

  we are really selfish creatures... Causin doenst know that she has already broken hearts of 3 people around her; her boyfriends and the mwizi na the mwizi's girlfriends

  as NN said, its better to stay single kama hutaki ku-miss mambo matamu...
   
 17. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Tunda kusa liwa wewe sema nini bana! "hajawahi kumsaliti mchumba wake kwa mwanaume mwingine isipokuwa huyu" sasa kusa jua?
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,521
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Mhhhh! :rofl: huo niliokupa ni mfano tu haimanishi kwamba ni mimi ndiye niliyelishwa limbwata, muulize Canius kama haya niliyoyaandika kuhusu kusikia madudu mwilini si ya kweli lol!...nikipata bahati ya kupendwa kihivyo nitakenua tu nakujiona nina bahati ya mtende......kama sitahamishiwa mkoani... lol!

  Ndiyo maana hujapata bahati ya kupata penzi kama hilo kama ulivyoandika hapa, "Mimi bado sijajua au kuelewa penzi la kweli ni penzi gani hilo na vigezo vyake ni vipi. " maana ukipendwa unaleta usanii in order to make sure that you are not included in that group of "pussy whipped people". Kupenda na kupendwa kuna wenyewe. :focus:
   
 19. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  You can say that again and again. Watu huwa wanasahau kabisa kuwa mapenzi cku za mwanzo ni matamu sana tena saaaaaaaaaaaaaana.
   
 20. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa ndio walewale ambao wanakutwa wamekunywa sumu au wamejitundika ndani ya room zao bila kuacha ujumbe wowote! dada chunga sana acha kuwa mshamba wa mapenzi! ushaingizwa mjini wewe hujui wanaume siku hizi nao wamekuwa wategemezi shauri yako Jamaa huyu wa ofisi ya karibu ameshapiga mahesabu akajua loo ulaji upo kama ni bachelor jioni ana uhakika wa kupata msosi na vitu vingine kwa hiyo kuwa makini! vijana wa siku hizi wanajifanya wanakupenda ili wakutumie tuu kifananciachee shauri yako...we hujiulizi hiyo miaka miwili na nusu upo na huyo mchumba wako umeweza kuvumilia kwa nini usisubiri ummalizie ngombe mkia! halafu huo uchumba wa miaka miwili mnasubiri nini kwa nini msioane au bado mnasomana tabia...shauri yako utakosa yote....
   
Loading...