Forwarded Call ni nini? Nawezaje kuzuia hili tatizo?

Vitamin K

Senior Member
Dec 2, 2017
158
168
Habari wana JF, Poleni na mihangaiko ya weekend.

Kuna tatizo hapa linanitatiza, nimeshindwa namna ya kulitatua, naombeni msaada wenu.

Katika kipindi cha likizo ya Corona nilipokuwa na mwenzangu nilikuwa naweka line yake kwenye simu yangu ili nitumie kifurushi cha MB alichojiunga kupitia line yake, kwani yeye hakuwa Smartphone.

Mbali na kutumia MB, pia tulikuwa tunapiga na kupokea simu kupitia line wakati ikiwa kwenye simu yangu, hivyo hivyo na kwa upande wa sms za kawaida

Kwa sasa mwenzangu amerudi chuo huko mkoani. Watu wakimpigia simu kupitia line yake, mimi huku napokea call ambayo ikianza kuita inaandika It is forwarded call

Yeye akipiga, hamna tatizo ila akipigiwa ndio mimi napokea forwarded call.

Wakuu, hili tatizo chanzo chake nini na nawezaje kulitatua. Naombeni msaada wenu.

Chief-Mkwawa na wanaJF wote karibuni.
 
Back
Top Bottom