Fortunes and misfortunes come and go

Patallo95

Senior Member
Feb 20, 2017
199
129
Waungwana na watu wazima salaam

Kisiasa mwanadamu anapoishi na wenzake ni muhimu sana yeye mwenyewe atambue nafasi yake.
Nafasi yake katika jamii ni kitu ambacho hujileta chenyewe na pia kinaweza kutoweka kabisa kwa muda wowote.

Natamani sana niwakumbushe tu kwqmba tunapaswa kujua kuwa hakuna kati yetu asiye weza kubadilika kutoka mtu fulani kwenda mtu fulani au hali fulani kwenda hali nyingine.

Niwapongeze wanaolikumhuka hilo kwa nafasi zao mbali mbali. Kwa mfano rais anayekumbuka kuwa anaweza kuwa rais mstaafu, mfungwa anayekumbuka kuwa anaweza kuwa huru, aliye huru anayekumbuka kuwa anaweza kuwa mfungwa na wengine wengi.

Katika hali hii ya kutokomeza kabisa madawa ya kulevya tutashinda hii vita kama kila mmoja atakuwa na kumbukumbu hii ya kuwa anaweza kubadilika na kuwa mtu mwenye nafasi nyingine tofauti na alivyokuwa nayo kwa sasa.

Waliotuhumiwa walikuwa huru na wakawa wafungwa bila kukataa kwa sababu ni waungwana na walikumbuka hilo.

Mbowe ni muungwana na ni mtu mzima kwa sababu alikuwa anakumbuka hilo. Ndio maana alienda kuitikia wito polisi ili awe mtuhumiwa na ikiwezekana hata mfungwa.
Alijua ni hali halisi kwake kutoka kuwa mwenyekiti hadi mtuhumiwa na ikiwezekana hata mfungwa.

Kwa hiyo Boethius mwanafalsafa huyu wa zamani aliyekuwa meya na baadaye mfungwa, aliyatanabaisha hayo kwenye kitabu chake cha consolation of philosophy.

SASA YANAPOKUJA KWA MKUU WA MKOA NA KAMANDA NINI KINAWAFANYA WASIKUBALIANE NA UTARATIBU HUU?
 
Back
Top Bottom