Forojo Ganze (Master), mchawi maarufu aliyeanzisha Mwenge wa Uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Forojo Ganze (Master), mchawi maarufu aliyeanzisha Mwenge wa Uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by NSWECKY, Feb 22, 2013.

 1. NSWECKY

  NSWECKY Senior Member

  #1
  Feb 22, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 141
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  "Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau"

  Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl.Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU"..... Inamaana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa? Na kwann Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge?

   
 2. N

  Ndelejha JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2013
  Joined: Dec 22, 2012
  Messages: 287
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ungeendelea kutujuza, sasa wewe unatupa somo kabla hatujajua linahusu nini unatuswalika maswali..!? ngoja waje wajuzi, mine is an ordinary mind...!
   
 3. Gogo la choo

  Gogo la choo JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2013
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 715
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sijaelewa kabisaaa..na shule ya kata hii daauuhh..!!
   
 4. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2013
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 1,988
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 180
  Mimi nimeimba UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YET ULETE TUMAINI .....

  Ingawa sijakuelewa vizuri lakini hapo maana yake ndiyo hiyo
   
 5. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #5
  Feb 22, 2013
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,153
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Safi sana lakini Story haijajitosheleza kuwekwa kuwa Historia katika Tanzania, kwani hatujamfahamu vizuri huyo Forojo Ganze jazijazia nyama kidogo
   
 6. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2013
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,527
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  'HATA' inafuata 'BAADA YA' hivyo maana hapo ni kuwa baada ya jambo halisi kufanyika ndio ziada yake itaelezewa kwa kutumia neno 'HATA'


  Kuwasha Mwenge
   
 7. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2013
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,527
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. m

  mhondo JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2013
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Alikuwa mchawi wa wapi na maarufu sehemu gani?
   
 9. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2013
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 717
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Kijue kiswahili vizuri umulike hata nje ya mip.................. maana yake unaanzia ndani hadi nje,pia Juu ya Mlima Kilimanjaro ni ndani ya Tanzania siyo Kenya hivyo unamulika ndani na nje ya nchi,pili huyo mchawi unayedai alianzisha mwenge ni ndugu yako nini? au fundi aliyeutengeneza mbona hatumjui angeweka patent right kama alivyofanya Wheel barrow kule ujerumani kwenye toroli tungemuelewa tena tafadhali usituchafulie jina la mwenge wetu wa uhuru na wachawi hiyo ni kufuru,hiyo ndiyo alama pekee inayowaunganisha watanzania iliyobaki na hakuna nyingine zilizobaki zote za kikabila,kikanda,kisiasa na kidini,hata bendera zanzibar wana yao hivi sasa.
   
 10. NSWECKY

  NSWECKY Senior Member

  #10
  Feb 22, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 141
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Huyu Forojo Ganze,alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo,walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote(Mwl.Nyerere),zindiko hilo lilifanyika bagamoyo ktk moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo,zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee.

  Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia ktk hilo shimo kwaajili ya kuuliza,alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es salaam,kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika,wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115,kisha akakata roho,baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani,baada ya hapo aliwagiza yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115.

  Kama kawaida ya shehe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38,hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115,na hii ndivyo ilivyokuwa,mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema,mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa bukoba jambo la kitaifa?,zindiko la bagamoyo linafanya kazi ,Safu hii ilikuwa ya watu 5 ambao ni. 1.mzee ramadhan,alizaliwa mwaka 1920,2.Ally tarazo(1929),3.Komwe wa Komwe(1918),4.Sheihe Yahya Hussein(1925),na 5.Forojo Ganze (1902)
   
 11. m

  mhondo JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2013
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kumbe ndiyo maana hatuendelei badala ya kumkabidhi nchi Mungu, ilikabidhiwa kwa shetani.
   
 12. NSWECKY

  NSWECKY Senior Member

  #12
  Feb 22, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 141
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Ww umeshachafuliwa tayari na huo mwenge wako,mbona hujiulizi kwann aliwasha mwenge badala ya mshumaa,nitafute nikupe historia na picha halisi za huyo Ganze,usishangilie kitu usichokijua chanzo chake
   
 13. NSWECKY

  NSWECKY Senior Member

  #13
  Feb 22, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 141
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Ndivyo ilivyo,jiulize juu ya Kenya waliokabidhi nchi kwa mungu wa wahindi ambaye ni amber,Kenya haitaendelea kuipita India sababu wanatumia mungu wao,hayo aliyafanya jomo kenyata,na akaweka kauli mbiu ya HARAMBEE,( neno HAR ni neno la Kihindi maana yake Tukuza,na AMBEE ni mungu wa wahindi,kwahiyo HAR+AMBEE=HARAMBEE yaani Tukuza Ambee),kenya imewekwa rehani india na ikiangalia nyaraka zote za serikali ya kenya zina neno HARAMBEE hadi nembo ya taifa Lao,sasa hivi HARAMBEE imeingia Tanzania kila Changizo la kuchangia chochote liwe au kidini au kiserikali wanasema tunafanya HARAMBEE ya kuchangia kitu fulani,kwahilo hatuwezi kuendelea na kuwapita kenya maana tunatukuza mungu wao waliyemtoa india hivyo hawezi kutupa zaidi tukawapita wakenya kimaendeleo,chunguza hilo
   
 14. Githeri

  Githeri JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 820
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  NSWECKY duh! Habari yako inasisimua sasa, tutathibitishaje kama usemayo ni kweli na si porojo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. mwananthropolojia

  mwananthropolojia JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2013
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  si uyamwage hapa jamvin wote tujifunze
   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2013
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  Tunajirogoroa vipi sasa? Ndio maana CDM hatuutaki huo Mwenge!
  Tulianza na Mungu tutadumu na Mungu!
   
 17. mwananthropolojia

  mwananthropolojia JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2013
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  hii stori ya mwenge niliisikia kutoka kwa mtu mwingine ingawa version yake ni tofauti kuhusu asili ya mwenge.mwenge wanasema ni ibada ya mungu wa kigiriki aitwaye hera na uliibwa na prometheus kutoka kwa mungu wao mkuu zeus ,na michezo ya olympic imepewa jina lake kutokana na eneo ilipokua michezo ya olympic ya kale inafanyika olympus.mwenge unaozungushwa ni ibada kwa mungu huyo,jaribu kulinganisha huo mwenge wa olympic unavyozungushwa dunia nzima haina tofauti na unavyozungushwa hapa tanzania
  ulifikaje tanzania?
  historia inaonyesha wakati wa long distance trade kuna watu kutoka kabila la wanyamwzi walisafiri na mungu wao ambaye alikua na nguvu sana kutoka maeneo ya tanzania interior kuja pwani,katika safari yao hiyo walipofika maeneo ya morogoro walianza kufa ,inasemekana mungu alikua mkali na kutokana na hiyo ikabid wamgawanye ,na kumwacha maeneo ya miliman ya uluguru ,ni mizimu maarufu sana nimeshahau jina wanalomwita kwa anayejua jina anaweza kunisaidia,basi katika kusafiri nae walifika mpaka bagamoyo na wakapigana vita kuwasidia wenyeji wa pale dhidi ya wakamba waliokua wametoka kaskazin,baada ya vile vita wakaloea hukohuko bagamoyo
  , na najua kwamba amani ya nchi hii kwa kiasi kikubwa imeletwa na hao wazee wa bagamoyo walioenda shimoni na huo mwenge ndivyo ulivyopatikana, sema sikupata hiyo stori zaidi na ningependa kujua zaidi connection ya hizi stori 2 kwani ibada zinafanana
   
 18. T

  Tetra JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2013
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Da,,kweli elimu haina mwisho.
   
 19. Mr Q

  Mr Q JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2013
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 5,230
  Likes Received: 5,702
  Trophy Points: 280
  Daa! Amazing! Kwanini mwananthropolojia na NSWECKY Msikae chini na kutunga/kuandika kitabu ambacho mnaweza kukipa jina la HISTORIA ILIYO SAHAULIKA au jina jingine lolote lile? Binafsi nimependa masimulizi yenu ingawaje yanahitaji ushahidi kidogo. Nawasilisha
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Travic

  Travic JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 298
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 80
  jf ni pahala pa kupunguza stress..
   
Loading...