Forodhani ZNZ yauzwa kwa wageni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Forodhani ZNZ yauzwa kwa wageni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Dec 9, 2008.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kuwa Forodhani Zenji imeuzwa kwa AGHAKHAN. Je wenzetu mlio visiwa vidogo vidogo mna nyeti yoyote kuhusu hili? maana naona main forum ya wazanzibari ya ZANZINET hairuhusu wasiojuana kwa vilemba kujoin


  Najua kuwa SHADIYA KARUME aka MKEWE RAIS KARUME ameshachukua kwa nguvu open space zote na kawapa wataliii including Nyumba ya mayatima ....Huko Pemba nasikia ndio anaiba kwa mile wala si kwa Acre

  Wana JF znz tunaomba input zenu kwenye hili
   
  Last edited by a moderator: Dec 10, 2008
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Soma vizuri hapa chini:
  [​IMG]
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Basi leo nilienda kununua GOMBA pale Romford road kwa jamaa wa Kimombasa nikaikuta hiyo...yaani hapa nilipo natafuna hili GOMBA huku nanywa Coca cola hata hayo maandishi hapo juu yashanshinda kuyasoma
   
 4. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Zenj kuna tatizo kubwa kuhusu Open spaces na hasa katika Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar.

  Halmashauri hii imeundwa na sehemu mbili kubwa, Mji Mkongwe na Ng'ambo. Katika Mji Mkongwe kuna asasi mbili zinazo simamia maendeleo yake, ambazo ni Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe na Halmashauri ya Manispaa.

  Katika Mji Mkongwe kuna open kadhaa ambazo ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya Uendelezaji wa mji Mkongwe huku zikipata huduma toka katika Manispaa. Open space hizo ni pamoja na Kelele Square, Jamhuri Gardens, Forodhani Gardens, Mnazi Mmoja Playgrounds na Donge Gardens.

  Kelele Square, baada ya Serena Hotel kuingia Zenj walikubaliana na Manispaa kuifanyia matengenezo, na sasa ipo katika hali nzuri na inaendelea kupata huduma toka katika Manispaa na hoteli hiyo. Aidha dhumuni lake la kuwa public open space lipo palepale na sasa inatumiwa zaidi na madereva teski na mapapasi. Umiliki wa eneo hili upo chini ya Mamlaka ya Mji Mkongwe.

  Jamhuri Gardens, imeendelea kuwa bustani nzuri kwa wanafunzi wa skuli jirani, aidha ni njia ya mkato wa wakaazi wa Wireless, Kikwajuni na Kisimamajongoo. Mapema mwaka 2000 ilifanyiwa matengenezo ikiwa na kuongezwa kwa mnara wa saa na yule mfadhili maarufu wa Malindi sport club. Umiliki wa eneo hili una utata kidogo kutokana na baadhi ya eneo kuwepo katika eneo la Ng'ambo.

  Forodhani Gardens, Ni bustani maarufu na yenye kutumiwa na mamia ya wakaazi katika mji huo. Hii imesababisha kuchakaa kwa haraka sana kwa bustani hiyo. Mashirika na asasi mbalimbali mara kwa mara wamejaribu kuchangia katika kuifufua bustani hii na mafaniko hayakuwa ya uendelevu.

  Mojawapo ya asasi hizo ni Zayadesa ambayo iliweza kidogo kufanya matengenezo wakati wakisubiriwa Agha Khan kuja na project yao. Agha Khan walianza kuonyesha hamu ya kuifanyia matengenezo bustani hiyo tokea mwaka 1994. Matengenezo yao ilikuwa ni pamoja kuitanua bustani hiyo kwa mita kadhaa kuingia baharini.

  Chini ya Sheria za Mji Mkongwe na Wizara ya Ardhi na Mipango Miji, sio rahisi kwa bustani hiyo kuuzwa. Zaidi ikumbukwe kuwa Agha Khan wamekuwa wakishirikiana kwa muda mrefu na Mamlaka ya Mji Mkongwe katika kuendelea kuifadhi na kuendeleza mji huo ambao sana una hadhi ya Heritage City
   
  Last edited: Dec 10, 2008
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
   
 7. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 8. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 9. S

  Stone Town Senior Member

  #9
  Dec 10, 2008
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  asalamu alaykum.

  nakubaliana na mtoa ufafanuzi kuhusu bustani ya forodhani kwamba haiwezi kuuzwa kwa kuwa ni eneo la wananchi kwend akujipumzikia.

  lakini tatizo kubwa linaloikabili afrika kwa sasa na hasa hapa kwetu tanzania ikiwemo zanzibar wakubwa kutumia nafasi zao kukumba maeneo ya ardhi kwa ajili ya baashara ama hoteli au nyumba za kuishi na wengi wao huwa wanawatumia watoto wao kufanya hivyo.

  kuna malalamiko mengi yanalekezwa kwa familia ya rais kuhusu kutumia vyeo kuchukua ardhi na ukenda katika mahakama za ardhi utakuwa hizo kesi na zaidi maam wa rais na watoto wake ndio wanalalmikiwa sana kuchukua lakini kama mnavyojua zanizbar hakuna vyombo vya habari binafsi vilivyopo ni fm za kupiga miziki ya fleva tu gazeti serious ndio halitakiwi kabisa.

  kini bado tunaishi na mwisho wa yote mtu atakufa ataiwacha ardhi hapa hapa. mfahamu kuwa waziri wa ardhi wa zanzibar ni ndugu yake huyo mke wa rais mama shadya sasakitaka ardhi atakoseshwa na mnajua kuwa zanzibar mambo ya kutengua sheria ni kitu chepesi sana hasa kuwatengenezea njia wakubwa kama kula mkate wa bakhressa kwa siagi.

  sisi tunakaa katika nyumba za udongo kwa hivyo wala hatujali maana tukifa pia tutakwend ahuko huko kwenye udongo wenye kutaka magorofa ndio watajiju....

  kila la kheri ndugu zangu.
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kuna matatizo katika kusimamia sheria ya Ardhi ya mwaka 1985, ambayo inatamka bayana kuwa ardhi yote ya Zenj ni mali ya serikali. Hapo hapo SMZ hiyohiyo inakuwa tayali kurudisha ardhi kwa baadhi ya watu(ardhi zilizotaifishwa baada ya mapinduzi). Sasa hapa unajiuliza ni nini maana ya Sheria ya ardhi ya mwaka 1985?

  Kuna suala la eka tatu, hizi walipewa wananchi kwa ajili ya kilimo, baadhi ya eka tatu hizi ziliingia kwenye masterplan ya mji wa zanzibar ya mwaka 1982. na zikapimwa kwa ajili ya viwanja vya kujengea nyumba za kuishi, shule, na maeneo ya biashara. Wengi wa wenye eka hizi walikubaliana na SMZ kupima viwanja hivyo na SMZ kuchukua asilimia fulani ya viwanja hivyo na kumwachia mwenye eka asilimia fulani ya viwanja, ambapo vinakuwa ni vyake na ni hiari yake kuviuza, kuvigawa au kuviendeleza yeye mwenyewe. Kule ambako masterplan haikufika na ni bado ni jirani na mji ikawa ni dili kubwa ya kuuza eka hizo. Ukirudi nyuma katika sheria ya Ardhi hairuhusu kwa mwananchi yoyote kuuza ardhi. Ardhi ni mali ya serikali na ni vipando tu ambavyo mwenye ardhi anaweza kuviuza.

  Hapo hapo kuna Idara ya mambo msige ambao hawa kazi yao kubwa ni kutambua mashamba na nyumba za watu na kutoa hati ya umiliki ambayo inatambulika na SMZ.... Mchezo unaofanywa hapo ni kuuza ardhi na kujenga msingi fasta na kukimbilia Mambo Msige kupata hati ya umiliki, ambayo unaipeleka huko wizara ya Ardhi ili wakupatie hati ya ardhi... (hii sio lazima).

  Kesi nyingi za ardhi katika Zanzibar zimetokana na udhaifu mkubwa uliopo kati ya wizara ya Ardhi na Idara ya Mambo Msige.Zaidi kuna hii habari ya Wafku...Ambayo kwa upande mmoja imechangia kuwepo na migogoro isiyo kwisha ya ardhi. Kupitia kasoro hizi wengi wameuza ardhi zao kinyume na taratibu na kusababisha kesi nyingi mahakamani na hadi kufikia kwa SMZ kuwa na mahakama ya malalamiko ardhi pekee.

  Kutupa lawama kwa familia ya Prez kuwa imetwaa ardhi zote za ufukweni sio pasipo kutaja hayo maeneo ni majungu tu. Ni vema kuja na malalamiko yenye kujitosholeza ili kuona kama yana ukweli wowote, kwani Zenj hakuna siri licha ya kutokuwepo kwa vyombo vya habari huru unavyodai wewe.

  Mfano wajungu ni matengenezo ya Bustani ya Forodhani, Mama Karume(festi leidi) ni Mwenyekiti wa Zayadesa, na walipopewa Bustani hiyo kuifanyia matengenezo wengi waliokuwa nje ya bustani hiyo walianza kudai kuwa tayali eneo hilo limeuzwa. Hata kile kipindi maarufu cha Mawio kiliamua kufanya uchunguzi juu ya hilo na kukuta hakuna ukweli wowote.

  Sehemu ya Nyumba ya mayatima(ilikuwa haitumiki zaidi ya kuwa makaazi ya panya buku) ambayo imefunguliwa Kibaa, nayo ilizua kizazaa kuwa watoto wa prez wamejichukulia nyumba la mayatima.
   
 11. u

  under_age JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2008
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  mnashangaaa kuuzwa ardhi?, hao wazanzibari wenyewe washauzwa ,wengi wao wamekuwa wasomali. aakh mie naona acha tusubiri kiyama tu, mabadiliko hususan kule zanzibar ni ndoto ya nzi kuambukiza ukimwi!
   
 12. E

  Engineer Mohamed JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2008
  Joined: Jul 27, 2007
  Messages: 461
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  GT

  nakukumbusha tena yule ni HAJJAT SHADYA KARUME mke wa rais wa znz Dr Amani Abeid Karume,umemsikia juzi alivyonguruma ktk BARAZA LA EID.

  kibunango

  ahsante kwa ufafanuzi wako maridhawa.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ardhi, usomali na mabadiliko yanaendana vipi na ukarabati wa Forodhani Park?
   
 14. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ama kuuzwa kwa Forodhani sina hakina na sijui kama kitu hicho kitawezekana lkn mbali ya majungu ambayo sishangai kuwa Zenj ndio utamaduni hata hivyo kuna ukweli fulani kuwa "First Family" ya Znz pamoja na Mansour inajihusisha na uchukuaji wa ardhi zote za maeneo ya wazi. Mfano ni eneo liliokombele ya nyumba za Kwamchina ambalo liko sehemu ya wilaya ya Magharibi Mansour amejigawia viwanja 18 vya biashara na anauza kwa milioni 10 kila kiomoja kupitia kwa mawakalawake wa siri.

  Hizo ni tips na kama kuna mfatiliaji afatilie kwani mimi nilipoona ujenzi pale niliulizia ili kutaka kupata sehemu hiyo lakini niliambiwa shika adabu yako na baada kufatilia ndio nilipata habari hizo.

  Mfano mwengine ni mbele ya kiwanda cha maziwa Maruhubi - alipouziwa Bakhresa alidai hadi hiyo sehemu na aliambiwa hivi hivi kama hataki atarudishiwa pesa zake lakini sehemu ile hapewi kwani ya Mama wa Dr/Alhaj/ Mheshimiwa/Rais wa Znz.

  Hawa jamaa sasa wameshageuzwa majina hadi wanaitwa 'hapa pangu'.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Eneo hilo kimipaka ya Halmashuri za Miji ya mwaka 1995 lipo katika halmashauri ya wilaya ya Magharibi, hata hivyo Halmashauri hiyo haina uwezo wa kupima na kugawa ardhi ama kutoa vibali vya ujenzi katika eneo hilo, kwani lipo chini ya sheria ya Ardhi ya mwaka 1985 na maendelezo yake yanafuta master plan ya mwaka 1982, huku ujenzi katika eneo hilo unapata baraka za UDCA ambayo inajengwa na wajumbe toka Idara ya Ujenzi, Idara ya Mipango Miji, Idara ya Ardhi, Idara ya Mazingira na Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar ambayo hutoa katibu na mwenyekiti.

  Awali kulikuwa na chombo kilichoitwa JBA(Joint Building Authority) ambacho mwenyekiti wake alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi. Chini ya JBA eneo hilo lilipigwa marufuku kwa ujenzi. Hii ilikuwa ni katika mwaka 1995-96 na tayali eneo hilo lilikuwa limeshapimwa kwa ujenzi wa nyumba za biashara na kugawiwa kwa waendelezaji. Wapo ambao waliwahi kujenga na Majengo yao yapo nayatumika na kufanya sehemu hiyo kuwa yenye ushawishi mkubwa wa kibiashara na hasa katika miaka hii kuliko ilivyokuwa miaka kumi iliyopita.

  Kusema kuwa Waziri Mansour amejitwalia sehemu hiyo sito shangaa sana na ninaweza kushangaa vile vile, kwani ni eneo ambalo lilizuiwa kufanyika kwa ujenzi ilhali watu wakiwa wameshagaiwa viwanja hivyo. Mansour kama Waziri wa Ardhi anao uwezo wa kisheria wa kufuta umiliki wa ardhi. Na iwapo amefanya hivyo siwezi kushangaa.

  Ikumbukwe kuwa ni Mansour huyuhuyu ambae alitishia kuvunja nyumba zote zilizojengwa katika eka tatu bila hata kuangalia kama zilijengwa kihalali ama la. Kauli yake ilikwenda kinyume na wizara yake anayoisimamia, kwani kuna eka tatu ambazo zipo ndani ya masterplan na wizara yake imeshirikiana na wenye eka hizo kutoa viwanja vya ujenzi wa nyumba. Hapa sikujua agenda yake ni nini, zaidi ya kudai ni hatua ya kuzuia ujenzi holela, ambao umekithiri zaidi nje ya maeneo yasiopimwa!

  Iwapo una nafasi ni vema kwenda katika Idara ya Mipango miji hapo Gizenga na kujaribu kuangalia eneo hilo, kwani ramani zake zipo wazi kwa yeyote kuziona, na unaweza kupata ukweli wa hizo shutuma zako.

  Kuhusu eneo la mbele ya kiwanda cha maziwa ambalo nalo ni eneo la kupimwa ni vema kujua iwapo huyo Bakhresa alilipata kwa namna gani. Kama ni moja kwa moja toka Idara ya Ardhi au kanunua kupitia madalali. Kama ni kupitia kwa madalali basi hana ubavu nalo tena na ni vema aktatafuta sehemu nyingine.
   
 16. Ntaramuka

  Ntaramuka Senior Member

  #16
  Dec 12, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu Shadia Karume aka HAPA PANGU kwa ujumla ndiye mwenye sauti juu ya uendeshaji wa serikali ya watu wa zanzibar. Kwa kutumia style yake ya hapa pangu amejichukulia maeneo mengi sana ya zanzibar akishirikiana na mtoto wake Amani Karume.

  Huko shamba Kaskazini Unguja wamejichukulia ardhi kubwa. Kuhusu forodhani imechukuliwa na Shadia Karume kwa style ileile ya hapa pangu. Na huu ulikuwa mpango ulioanza mapema walianza kwa kuchukua jumba la watoto yatima lililoko katika eneo hilo la forodhani sehemu ambayo awali ilikuwa rahisi kupata misaada kutoka kwa wasamalia kwani ni mjini na watoto hao masikini ya Mungu wamehamishiwa Mombasa nje kidogo ya mji ambapo hawaonekani kirahisi
   
Loading...