Formulae inayotumika kumlipa haki zake mtumishi aliepunguzwa kazi serikalini ikoje?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Nakumbuka zoezi la kupunguza wafanyakazi (redundancy) liliwahi fanyika serikalini miaka ya 90 mwanzoni wengine wakati huo tukiwa bado vijana wadogo ila tunaoweza kukumbuka hali iliyowakumba watumishi wa serikali enzi hizo za mzee Mwinyi.

Nakumbuka watu walipewa nafasi ya kuomba kwa hiari yao kupunguzwa kabla ya zoezi hilo kufanywa kwa lazima bila kujali uko tayari kupunguzwa au laa.

Sasa mliokuwa watumishi miaka hiyo kama mpo humu tunaomba mtupe uzoefu wenu hapa na hata maafisa utumishi mlioko humu nanyi pia mtusaidie ni namna gani malipo ya mtu anaepunguzwa kazini yanafanywa.

Mwenye standing order nae ajaribu kuipitia maana huenda utaratibu huo ukawa umeelezwa katika kitabu hicho.

Wengine tuko private ila tuna ndugu zetu huko serikalini wanaotaka kujua jambo hili.

Ahsanteni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom