Formula Mpya ya uhakika: Kuhusu kumaliza tatizo la Wapalestina na Waisrael

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,952
2,000
Napendekeza formula Mpya itakayoweza kumaliza kabisa mzozo wa waisrael na wapalestina. Formula hii inazingatia :
1. Msingi wa tatizo
2. Ukweli wa kihistoria
3. Kanuni za urithi
Ninaamini ikifanyiwa kazi italeta matokeo chanya na jumuia ya kimataifa italazimika kunipa tuzo ya Nobele (Nobel Prize)
Ufafanuzi: 1. Msingi wa Tatizo. Msingi wa tatizo ni kugombania mahali pa kuishi ambapo kila taifa kati ya Israel na Palestina anaona anastahili kuwa hapo. Wapalestina wanaona nchi yote inayoitwa Israel ni yao na inapaswa kuitwa Palestina na mji wake mkuu ni Yerusalemu!
Hali kadhalika, Waisrael wanaona nchi yote wanayokaa wao kwa sasa na ile sehemu wanayokaa wapalestina ni nchi yao ambayo walipokonywa kwa nguvu na kupelekwa uhamishoni! Na wanaona wana haki na wajibu wa kuirejesha yote hatua kwa hatua na Yerusalemu ni mji wao mkuu! Hilo ndilo tatizo la msingi!
2. Ukweli wa kihistoria: Wapalestina na waisrael wote wanagombea nchi moja kutokana na ukweli wa kihistoria unaofahamika wazi. Asili ya wote hawa ni pale pale wanapopagombania! Hii ni kwa sababu waisrael na wapalestina ni ndugu wa damu! Wote baba yao ni mmoja anaitwa Ibrahimu! Ibrahim alizaa watoto wawili wa mwanzo, lakini kwa mama wawili tofauti. Wa kwanza ni Ishmael. Huyu ni mtoto wa haram kwa msingi kuwa alizaliwa nje ya ndoa! Ibrahimu baada ya kuona kuwa mke wake wa ndoa Sara ni tasa na mzee sana alisikiliza ushauri mbaya wa mke wake aliyemtaka aingie kwa mjakazi wake Hajiri ili apate mtoto! Kwa hiyo Ibrahim akazaa na mjakazi wa Sara na akazaliwa Ishmael.
Uzao wa Ishmael ndo ulizaa waarabu wote wakiwemo wapalestina!
Lakini baadaye Mungu alifanya muujiza Sarah akapata mimba katika uzee sana wa miaka 90 na akamzaa mtoto halali wa kwenye ndoa akaitwa Isaka! Isaka alizaa watoto wawili mapacha, Mkubwa Esau, na mdogo wake Yakobo. Yakobo baadaye alibadilishiwa jina akaitwa Israel. Uzao wa Israel ndo ulileta waisrael wote na taifa lote la Israel. Sasa uzao wa Israel unaotokana na Isaka mtoto halali wa Ibrahimu na uzao wa Ishmael mtoto haramu wa Ibrahimu, wote wanataka urithi kwa mzee wao Ibrahimu kwa maana ya ardhi aliyokuwa anamiliki Ibrahimu, seke seke liko hapo!
3.Kanuni za urithi: Kanuni za urithi za waisrael hazipishani na za waarabu. Mtoto wa haramu hana haki ya kurithi, sana sana baba akiwa hai anaweza kumpa chochote kama sehemu ya uwajibikaji wa matunzo ya mtoto/ mwana wake, lakini haihesabiki kuwa ni urithi!
Kwa maana hiyo uzao wa Ishmael hauna sehemu ya urithi kwa Ibrahim, bali uzao wa Ishmael ambao ni waarabu wakiwemo na wapalestina wana haki ya kurithi kwa Ishmael! Mungu alimpa Ishmael ardhi kubwa na utajiri mkubwa sana! Kwa bahati mbaya waarabu wamewatenga ndugu zao na waarabu wenzao waitwao wapalestina kwenye kurithi kwa mzee wao Ishmael. Lakini wanamsukumiza akarithi mahali ambapo ni mtoto wa haramu huku wakijua kabisa hata kwa mujibu wa dini yao wenyewe kuwa huko wanakomsukumizia hana urithi kwa sababu ni mtoto wa nje ya ndoa. Kwa mujibu wa uislamu mtoto wa nje ya ndoa huwa harithi. Kwa hiyo hawa waarabu wenzake ndo wamewadhulumu wapalestina urithi walioustahili kwa Ishmael maana ndiye baba yao wote!
Formula ya suluhisho: (A) Wapalestina kama walivyo waarabu wengine wanastahili kuwa na taifa lao kama walivyo wasaudia, wairan, wasyria nk. Itafutwe/zitafutwe nchi za kiarabu ambazo zina eneo kubwa zaidi kuliko waarabu wengine! Hawa wenye eneo kubwa zaidi ya wenzao ndio waliowapunja wenzao kwenye kurithi toka kwa mzee wao Ishmael! Hawa waambiwe wamege kipande muafaka cha ardhi ili wapewe ndugu zao wapalestina! Kwa nini wao warithi sehemu kubwa kuliko wengine wakati watoto wana haki sawa ya kurithi toka kwa baba yao Ishmael?
Kwa maana hiyo, Iraq, na Syria zitoe sehemu hiyo ya ardhi. Na ninapendekeza ile sehemu iliyokuwa imetekwa na IS (Islamic State) ya Syria na Iraq wapewe wapalestina kama urithi wao halali kwa baba yao Ishmael waliokuwa wamedhulumiwa na ndugu zao waarabu.
(B) Baada ya wapalestina kupewa eneo hilo, kila taifa la kiarabu liwachangie USD 5 bilioni (isipokuwa Iraq na Syria waliotoa ardhi), kama fidia kwa ndugu zao waliokuwa wamewatenga kwenye urithi! Kwa bahati nzuri hiyo ni pesa ndogo sana kwa mataifa ya kiarabu! Halafu hiyo sehemu tayari ina visima vya mafuta na Palestina litakuwa taifa kubwa na lenye nguvu na uchumi mzuri sana ndani ya miaka 5 tu! Mji wake mkuu napendekeza uwe Allepo!
Kama kila taifa LA kiarabu likichachangia hivyo, miji yote iliyoharibiwa kwa vita dhidi ya IS itajengwa upya! Na taasisi za kielimu kama shule na vyuo vitajengwa upya!
Kama waarabu wakikataa, basi wakome kulaumu na kulalamika! Kama wao wameshindwa kumsaidia ndugu yao, kwa nini wanategemea akakaribishwe na kupewa urithi ambako ni mtoto wa kambo? Nawasilisha na karibuni kwa michango!
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,995
2,000
Sijapata kuona kufuru mbaya namna hii! Kwamba mwanaharamu arithi sawa sawa na mwana wa haki! Jerusalem ni moja; haigawanyiki; wala haichangiwi! The City of God; the City of Jacob. Jerusalem haifananishwi na nwingine wowote ule; sio Vatican, sio Mecca!
 
mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
19,760

Nadhani Tatizo Lao ni la ki-deen
IMG_20171211_210814_019.jpg
unataka kulitatua kihivyo haiwezekani...hiyo ayat ni Kauli haqi ya allah na anae iishi atapata thawab duniani na kesho pepo...hawatakubaliana na wewe na kukiuka maagizo ya Mungu wao...
 
Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,918
2,000
Hakuna jambo baya na la dhambi kubwa kama Kumsingizia UZINIFU BABA WA IMANI ABRAHAM, Yaani ni hatari, acheni kabisa kutamka maneno hayo, maana yule ni kipenzi cha Mungu!

Ukisoma Genesis( kitabu cha mwanzo), Sara alimtwaa Hagar na Kumpa Abraham ili AWE MKE , sasa umewahi kuona wapi Mtu akazini na Mkewe? (Soma Genesisi 16:1-4)

Ndugu yangu, kuwa makini sana na ushabiki maandazi wa kidini, lakini jua tu kuwa kuna watu ni vipenzi wa Mungu, ukiwasimanga Mungu anawatetea, na Ibrahim ni mmojawapo!

Scenario ya uzao wa Ishmael haina tofauti na Uzao wa mtoto mmoja wa Yakobo aitwaye Dani, ambaye kutokana na Rachel mke wa Yakobo kutokubeba mimba akamtwaa Bilhah kijakazi wake akampa Yakobo awe mke wake ambaye hatimaye alimzaa Dani, Dani ni mwanzilishi wa kabila la Dani ktk yale makabila 12 ya wana wa Israel. Soma Genesis (30:2-6 na 30:9)

Kitu kingine unachotakiwa kujua ni hivi: Ishmael siyo asili ya waarabu wote, bali ni asili ya makabila machache ya waarabu.
Ishmael alivyoenda Arabia, alikuta kuna waarabu wanaishi huko, kwa hiyo naye akaishi nao na kuanzisha vizazi vyake ambavyo baadhi ya makabila ya waarabu miaka ya baadae walioriginate
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,952
2,000
mbona bandiko lako limekaa kinadharia zaidi,
Siyo kinadharia! Huo ndio ukweli ambao watu wanakwepa kuukabiri! Ni ukweli wa kihistoria na kiutamaduni! Vinginevyo ni unafiki usiozingatia ukweli wa historia! Hakuna mwarabu anayeweza kuthubutu kuupinga ukweli huu walioamua kuufumbia macho. Tatizo Mpalestina mwenyewe hajawahi kujaribu kudai haki yake anakostahili kuidai! kwa ndugu zake waarabu!
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,952
2,000
Duh mkuu utakuwa na hallucinations wewe..
Maana kitu ulichoandika yakiwezekani dunia hii.
Huu ni ukweli ambao waarabu wote wakiwemo wapalestina wanaufahamu! Waulize waislamu kama mwana wa nje ya ndoa huwa ana haki ya kurithi! Waarabu wote wakiwemo wapalestina wanajua kuwa baba yao na Ishmael. Na wanajua Ishmael ni mtoto wa nje ya ndoa! Asiye na haki ya kurithi Mali ya Ibrahimu ikiwemo nchi ya Israel (ilikuwa inaitwa kanaani,) walipoirithi ikaitwa kwa jina lao Israel!
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,952
2,000
Nadhani Tatizo Lao ni la ki-deen View attachment 648833 unataka kulitatua kihivyo haiwezekani...hiyo ayat ni Kauli haqi ya allah na anae iishi atapata thawab duniani na kesho pepo...hawatakubaliana na wewe na kukiuka maagizo ya Mungu wao...
Niambie dini yako inaruhusu mtoto nje ya ndoa kurithi? Niambie je Ishmael si mtoto wa nje ya ndoa? Niambie je wapalestina na waarabu si uzao wa Ishmael? Inakuingiaje akilini mtoto wa haram arithi pamoja na mtoto wa halali?
Tatizo waarabu wamemdhulumu ndugu yao, halafu wanamsukumia ambako wanajua kabisa hana uhalali wowote wa kurithi! Walijaribu kupora kwa nguvu ardhi ya Israel walipoivamia Israel kwa kushtukiza mwaka 1967! Kinyume chake akapoteza zaidi kwa kichapo kilichisababisha rais wa Misri Nasser afe kwa kihoro, aliposikia ndege zake zote zimeteketea tena zikiwa bado Mpya!
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
17,879
2,000
Umeelezea vizuri sana hasa katika historia ya tatizo.

Watafute pa kwenda wakikosa waende bara la Atlantic
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,952
2,000
Hakuna jambo baya na la dhambi kubwa kama Kumsingizia UZINIFU BABA WA IMANI ABRAHAM, Yaani ni hatari, acheni kabisa kutamka maneno hayo, maana yule ni kipenzi cha Mungu!

Ukisoma Genesis( kitabu cha mwanzo), Sara alimtwaa Hagar na Kumpa Abraham ili AWE MKE , sasa umewahi kuona wapi Mtu akazini na Mkewe? (Soma Genesisi 16:1-4)

Ndugu yangu, kuwa makini sana na ushabiki maandazi wa kidini, lakini jua tu kuwa kuna watu ni vipenzi wa Mungu, ukiwasimanga Mungu anawatetea, na Ibrahim ni mmojawapo!

Scenario ya uzao wa Ishmael haina tofauti na Uzao wa mtoto mmoja wa Yakobo aitwaye Dani, ambaye kutokana na Rachel mke wa Yakobo kutokubeba mimba akamtwaa Bilhah kijakazi wake akampa Yakobo awe mke wake ambaye hatimaye alimzaa Dani, Dani ni mwanzilishi wa kabila la Dani ktk yale makabila 12 ya wana wa Israel. Soma Genesis (30:2-6 na 30:9)

Kitu kingine unachotakiwa kujua ni hivi: Ishmael siyo asili ya waarabu wote, bali ni asili ya makabila machache ya waarabu.
Ishmael alivyoenda Arabia, alikuta kuna waarabu wanaishi huko, kwa hiyo naye akaishi nao na kuanzisha vizazi vyake ambavyo baadhi ya makabila ya waarabu miaka ya baadae walioriginate
Ibrahimu alikubaliana na Sara kuingia kwa Hajiri na kumfanya awe mke! Hakuwa halali kwa mujibu wa mila za wayahudi! Myahudi huwa haozeshwi na mkewe! Walikubaliana kitu ambacho hata Sara alikuwa anajua kuwa huyo si mke. Ukitaka kuelewa mawazo ya Sara usiishie kuyasoma kwenye sura hii tu, yasome pia kwenye kitabu cha Mwanzo 21:9-11. Nanukuu yote kwa faida ya wasomaji: "Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye Alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, mfukuze MJAKAZI huyu na mwanawe maana mwana qa MJAKAZI HATARITHI pamoja na mwanangu Isaka. Neno hili likawa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe, MUNGU akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana na huyo MJAKAZI wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake , kwa maana katika ISAKA uzao wako utaitwa". Mwisho wa kunukuu!
Sura ile ya 16 lazima isomwe pamoja na sura ya 21 ili kulielewa jambo hili katika muktadha wake! Mchezaji mkubwa hapa katika kuzaliwa kwa Ishmael ni Sarah! Ndiye aliyekuwa anajua anachokitafuta! Kabla, kwenye, na baada ya sura ya 16 Hajiri ni mjakazi, katika sura ya 16 Ibrahimu anagilibiwa na mkewe kuwa anapewa Hajiri awe kama mke, wakati Ibrahimu anajua kabisa utaratibu wa kiyahudi wa kuoa siyo huo, na moyoni Sara alijua anamgilibu tu ili apate mtoto lakini kiukweli na kiuhalisia kwa Sara na kwa Mungu ni kuwa Hajiri hajabadilisha nafasi, bado ni MJAKAZI na siyo MKE. Hata Ibrahimu mwenyewe hakuwa anamnena Hajiri kama mke kwenye sura hii ya mwanzo 16:6 nanukuu "Naye Ibrahimu akamwambia Sarai, tazama MJAKAZI wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa naye akakimbia kutoka mbele zake". Mwisho wa kunukuu. Unaona hata Ibrahimu hakuwahi kumwita Hajiri kama MKE! Anamnena kama mjakazi. Baada ya sura ya 16 Hajiri aliendelea kuitwa mjakazi na Sara kama nilivyonukuu hapo juu kwenye sura ya 21:9-12. Tumeona hapa Sara anamwambia Ibrahimu amfukuze MJAKAZI na siyo MKE! Lakini funga kazi ni huu mstari wa 12 ambapo Mungu mwenyewe anasema Hajiri ni MJAKAZI hasemi ni MKE! Nanukuu tena: Mwanzo 21:11 "Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako kwa ajili ya huyo mwana na huyo MJAKAZI wako. Kila akuambialo Sara , sikiza sauti yake kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa" Kama Mungu anasema Hajiri ni MJAKAZI, Sara anasema Hajiri ni Mjakazi, na Ibrahimu mwenyewe kwenye hiyo sura ya 16 anasema Hajiri ni MJAKAZI , ni nani wewe uweze kusema ni mkewe? Sana sana umeshindwa kuyaelewa maandiko kwa mujibu wa muktadha (context).
Hitimisho: Hajiri ni mjakazi kabla, wakati na baada ya kumzaa Ishmael na aliendelea kutoa huduma kama mjakazi mikononi mwa Sara mpaka alipoondoka alikuwa ni MJAKAZI, na wahusika wote: Sara, Ibrahimu na Mungu mwenyewe walimwita hivyo. Kwa hiyo hana urithi kwa Ibrahimu! Hana urithi kwa Israel.
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,952
2,000
Vp na uzao wa papii kocha utarithi nini?
Hao waulize wadau wa mziki labda wanafahamu! Mimi nimejikita kindakindaki kwenye suala la wapalestina kutaka kurithi pamoja na wana halali wa ndoa wakati wenyewe wanajua kabisa ni wa nje ya ndoa! Walizaliwa na mjakazi! Lakini Mungu mwenye haki alishawapa urithi! Tatizo wamedhulumiana! Waarabu wamemdhulumu mwarabu mwenzao mpalestina! Nataka jumuia ya kimataifa iingilie kati kuwataka waarabu wamgawie pia mpalestina kipande cha ardhi kama stahili yake ya urithi!
 
msabillah

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
3,659
2,000
Kwanza futa wazo lako potofu kuwa Ishmael ni mtoto wa haramu je unaijua vizuri historia ya Ibrahim?
Kwa kifupi ni kuwa sara alimuomba mume wake tena Kwa kumbembeleza amuchukue kijakazi wake huenda atawazali mtoto awe mlisi.
Tuludi kwenye uharamu nikwamba mke kamruhusu mume kumuoa Hajra (kumuingilia) hiyo tayari ni ndoa au wewe ulitaka wakafunge kanisa gani au msikiti upi au ni nani aliyekuambia Sarai alifunga ndoa chini ya mchungaji Nani au shekh yupi!
Kitendo cha mke kulidhia mume kumchukua mke mwingine ni ndoa tosha, ndiyo maana Mungu akamwambia Ismail kuwa nawewe kilio chako nimekisikia utakuwa juu yawalio juu....
Ukweli ni kuwa hawa ni ndugu ila hakuna cha haramu wala nini. Kikubwa wagawane maeneo kwisha kazi ikiwezekana waigawe Jerusalem na wajenge ukuta kama ulikokuwa Ujeruman mashariki na magharibi.
 
Soma post yangu#12 nimeeleza vizuri sana! Ibrahimu hakuwahi Kumwita Hajiri kama mke, aliendelea kuhudumia kama mjakazi , na Sara alikuwa anamwita mjakazi si mke mwenza, n Mungu alikuwa anamwita kama mjakazi! Huo ndio ukweli! Mwana wa haramu kurithi ni ndoto isiyotekelezeka hata huko kwenye dini yenu! Lakini mnalazimisha hawa watoto wa haramu warithi, haiwezekani, hata wakitumia nguvu haiwezekani! Na waarabu wote wanajua haiwezekani! Wao waarabu ndio wamemdhulumu ndugu yao! Hata kipindi waisrael walipokuwa hawajarudi, Yerusalemu haikuwa chini ya wapalestina bali ilikuwa chini ya Yordan!
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,995
2,000
Ibrahimu alikubaliana na Sara kuingia kwa Hajiri na kumfanya awe mke! Hakuwa halali kwa mujibu wa mila za wayahudi! Myahudi huwa haozeshwi na mkewe! Walikubaliana kitu ambacho hata Sara alikuwa anajua kuwa huyo si mke. Ukitaka kuelewa mawazo ya Sara usiishie kuyasoma kwenye sura hii tu, yasome pia kwenye kitabu cha Mwanzo 21:9-11. Nanukuu yote kwa faida ya wasomaji: "Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye Alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, mfukuze MJAKAZI huyu na mwanawe maana mwana qa MJAKAZI HATARITHI pamoja na mwanangu Isaka. Neno hili likawa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe, MUNGU akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana na huyo MJAKAZI wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake , kwa maana katika ISAKA uzao wako utaitwa". Mwisho wa kunukuu!
Sura ile ya 16 lazima isomwe pamoja na sura ya 21 ili kulielewa jambo hili katika muktadha wake! Mchezaji mkubwa hapa katika kuzaliwa kwa Ishmael ni Sarah! Ndiye aliyekuwa anajua anachokitafuta! Kabla, kwenye, na baada ya sura ya 16 Hajiri ni mjakazi, katika sura ya 16 Ibrahimu anagilibiwa na mkewe kuwa anapewa Hajiri awe kama mke, wakati Ibrahimu anajua kabisa utaratibu wa kiyahudi wa kuoa siyo huo, na moyoni Sara alijua anamgilibu tu ili apate mtoto lakini kiukweli na kiuhalisia kwa Sara na kwa Mungu ni kuwa Hajiri hajabadilisha nafasi, bado ni MJAKAZI na siyo MKE. Hata Ibrahimu mwenyewe hakuwa anamnena Hajiri kama mke kwenye sura hii ya mwanzo 16:6 nanukuu "Naye Ibrahimu akamwambia Sarai, tazama MJAKAZI wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa naye akakimbia kutoka mbele zake". Mwisho wa kunukuu. Unaona hata Ibrahimu hakuwahi kumwita Hajiri kama MKE! Anamnena kama mjakazi. Baada ya sura ya 16 Hajiri aliendelea kuitwa mjakazi na Sara kama nilivyonukuu hapo juu kwenye sura ya 21:9-12. Tumeona hapa Sara anamwambia Ibrahimu amfukuze MJAKAZI na siyo MKE! Lakini funga kazi ni huu mstari wa 12 ambapo Mungu mwenyewe anasema Hajiri ni MJAKAZI hasemi ni MKE! Nanukuu tena: Mwanzo 21:11 "Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako kwa ajili ya huyo mwana na huyo MJAKAZI wako. Kila akuambialo Sara , sikiza sauti yake kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa" Kama Mungu anasema Hajiri ni MJAKAZI, Sara anasema Hajiri ni Mjakazi, na Ibrahimu mwenyewe kwenye hiyo sura ya 16 anasema Hajiri ni MJAKAZI , ni nani wewe uweze kusema ni mkewe? Sana sana umeshindwa kuyaelewa maandiko kwa mujibu wa muktadha (context).
Hitimisho: Hajiri ni mjakazi kabla, wakati na baada ya kumzaa Ishmael na aliendelea kutoa huduma kama mjakazi mikononi mwa Sara mpaka alipoondoka alikuwa ni MJAKAZI, na wahusika wote: Sara, Ibrahimu na Mungu mwenyewe walimwita hivyo. Kwa hiyo hana urithi kwa Ibrahimu! Hana urithi kwa Israel.
Kiongozi; umemjibu vyema sana Gamba la Nyoka. Sitapunguza wala kuondoa yodi wala nukta moja ya ulichoelezea. Jamaa anashindwa kuelewa hayo maneno machache aliyonukuu kwa hila - "ILI AWE MKEWE"; ni kweli inawezekana mwanzoni lengo la Sara (kwa tatizo la ugumba alilokuwa nalo) ni ili Hajiri awe mkewe Ibrahimu lakini ilikuwa hivyo? Haikuwa hivyo kama ulivyofafanua kwa reference murua za kimaandiko.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,995
2,000
...
Tuludi kwenye uharamu nikwamba mke kamruhusu mume kumuoa Hajra (kumuingilia) hiyo tayari ni ndoa au wewe ulitaka wakafunge kanisa gani au msikiti upi au ni nani aliyekuambia Sarai alifunga ndoa chini ya mchungaji Nani au shekh yupi!
Kitendo cha mke kulidhia mume kumchukua mke mwingine ni ndoa tosha,....
Taratibu za wapi hizo? Tatizo unadhani tamaduni zako zina-apply kwa kila jamii. Nioneshe mstari hata mmoja unaoonesha Hajira ni MKE wa Ibrahim!
 
mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
19,760
2,000
Niambie dini yako inaruhusu mtoto nje ya ndoa kurithi? Niambie je Ishmael si mtoto wa nje ya ndoa? Niambie je wapalestina na waarabu si uzao wa Ishmael? Inakuingiaje akilini mtoto wa haram arithi pamoja na mtoto wa halali?
Tatizo waarabu wamemdhulumu ndugu yao, halafu wanamsukumia ambako wanajua kabisa hana uhalali wowote wa kurithi! Walijaribu kupora kwa nguvu ardhi ya Israel walipoivamia Israel kwa kushtukiza mwaka 1967! Kinyume chake akapoteza zaidi kwa kichapo kilichisababisha rais wa Misri Nasser afe kwa kihoro, aliposikia ndege zake zote zimeteketea tena zikiwa bado Mpya!
Hizo ni hoja nyingine...nilicho andika Mimi sababu ya usuluhishi kuwa mgumu hapo ni deen Iman sababu mapalestine wanaamini kwamba hii
IMG_20171211_210814_019.jpg
ni Kauli ya Mungu wao na ukiikiuka na kupatana na Yahudi unakufuru hivyo ni kaafir na makazi yako motoni...usione kitendo cha Iran kulenga kuifuta Israel ni maskhara ilaha wanatekeleza Agizo la Mungu wao na wakifanikiwa utekelezaji watapata thawab na kufuzu kwenda sardaus...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom