Form ya Medical Examination ni kichaka cha rushwa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,553
44,722
Ukiwa unajiunga na shule,Chuo au ukiwa unareport katika ajira mpya Kuna form tunapewa tukajaziwe na daktari lengo ni upimwe ijulikane Hali yako ya kiafya ndio taratibu inawataka hivyo lakini kwa miaka mingi tabia zetu sisi watanzania sijui Kama na mataifa mengine Wana hio tabia ya ku forge.

Mtu hupimwi chochote unaenda tu masjala unapigiwa muhuri unairudisha form.

Usalama wa taifa mko wapi muishauri Serikali kwamba utaratibu uangaliwe upya na Kama lengo ni kugawana posho au kuongezea mapato vituo vya afya Basi ijulikane na Sina uhakika Kama hizo 5000 au 10000 huwa zinaingia kwenye mifuko ya watu au kwenye mfumo wa mapato ya hospital.

Taifa limefikia hatua hii kweli udanganyifu wa aina hii ndo unafanya rushwa ionekane ni kitu cha kawaida. Kwanini kama lengo ni kujua Hali ya kiafya kwanini tusipimwe kweli? Kosa hapo ni la nani ni letu sisi wananchi au ni la kwao?
 
Back
Top Bottom