Form VI 08 Exam Results | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Form VI 08 Exam Results

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Invisible, May 5, 2008.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  May 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Najua wengi mlikuwa mnatafuta kitu hiki.

  Check this link out...


   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
 3. A

  Advisor Member

  #3
  May 5, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila information ninazojaza inasema "Sorry..."
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  I see hadi uweke centre number na student name? ya mwka huu yamekuwa siri!
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  May 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Ndilo balaa lake mkuu... Kama mwanao kakuficha namba basi tena!
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ukiweka centre no. ya shule, unayapata yote.
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kuna ambaye anaijua centre number ya St' Francis Mbeya.....please?
   
 8. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nani anaweza kunipa center number za shule, kuna shule nataka kuzicheki, kama kuna mtu anayo copy ya matokeo yenye namba za shule aniwekee hapa please
  Thanks!
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Unaweza kuzipata hapa chini kwa zile shule ambazo zilikuwepo mwaka jana.

  http://www.necta.go.tz/matokeo/acentres.htm
   
 10. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ogah,

  Kama sikosei hii ni O-level tu, sijui kama tayari wana A-level.
   
 11. E

  Engineer Mohamed JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2008
  Joined: Jul 27, 2007
  Messages: 461
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  mbona jina la SHY sioni,vile alifanyia shule gani???
  any way thanx mkulu.
   
 12. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Sijaona statements za kusema ni shule zipi zimefanya vizuri, na zipi zimeboronga. Hawataki tena ushindani?

  Ushindani ndio unainua kiwango cha Elimu Tanzania. Kama kuna mtu anataka kuua ushindani uliokuweko, basi anatutakia mabaya sana.

  Mmi nitamshukuru Mungai daima kwa kujenga ushindani katika Elimu Tanzania. Matokeo ya huo ushindani ni makubwa kuliko wengi wanavyoweza kuelewa. Na hao wasioweza kuelewa labda ndio wanataka kuondoa ushindani.

  Augustine Moshi
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mtanzania
  ....shukrani kwa kunielewesha.....nilipitiwa...Ni Loyola
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,766
  Trophy Points: 280
  engineer
  shy angalia mwanakijiji sec school
  kiburugwa.aana div IV
   
 15. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Matokeo kidato cha sita: Wasichana waendelea kushika rekodi


  *Kifungilo,Kibosho,Mzumbe, Kilosa vinara
  *Potatlal, Maswa, Fidel Castro,Esacs zavuta mkia

  Reuben Kagaruki na Said Mwishehe

  BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Februari mwaka huu, ambapo wasichana wameongoza tena kwa kufanya vizuri kuliko wavulana.

  Akitangaza matokeo hayo Dar es Salaam jana Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Joyce Ndalichako, alisema ingawa idadi ya wasichana waliofanya mtihani ni ndogo, ikilinganishwa na wavulana, bado wameweza kufanya vizuri hali inayodhihirisha kuwa wakiongezeka watakuwa na nafasi ya kuwazidi wavulana.

  Alisema kati ya watahiniwa 47,464 waliosajiliwa kufanya mtihani huo ni watahiniwa 45,054 waliofanya mtihani. Alisema wanafunzi wa kike waliofaulu ni 14,426 na wavulana ni 25,496 kati ya wote waliofanya mtihani.

  "Takwimu hizi zinaonesha kuwa japo wasichana ni wachache lakini wamefanya vizuri kuliko wavulana ingawa idadi yao ni ndogo," alisema Dkt. Ndalichako.

  Kuhusu ubora wa kufaulu kwa kuangalia madaraja, alisema takwimu za mwaka huu zinaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,415 wamefaulu katika ngazi ya daraja la kwanza hadi la tatu.

  Wasichana waliofaulu katika madaraja hayo ni 8,603 na wavulana ni 14.812. Kutokana na matokeo hayo alisema idadi ya wanafunzi waliofaulu kwa madaraja hayo kwa mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 5.83.

  Aliongeza kuwa idadi ya watahiniwa katika shule za serikali waliofaulu mtihani huo mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 5.42 huku asilimia ya walioshindwa ikiwa imeshuka kwa asilimia 1.03.

  Kwa upande wa shule za Jumuiya alisema kiwango cha kufaulu katika madaraja hayo kimeongezeka kutoka asilimia 57.21 hadi asilimia 71.55 wakati asilimia ya watahiniwa walioshindwa imeshuka kwa asilimia 7.09 kutoka aslimia 13.70 ya mwaka jana

  Katika shule za binafsi alisema kiwango cha ufaulu katika madaraja hayo kimeongezeka kwa asilimia 5.03, wakati kiwango cha walioshindwa kimepungua kwa asilimia 0.16 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana.

  Pia alisema kiwango cha kufaulu katika shule za seminari katika madaraja hayo kimeongezeka kwa asilimia 0.72 wakati kiwango cha walioshindwa ikipungua kwa asilimia 0.58.

  Alisema kiwango cha kufaulu katika shule za Zanzibar kwa madaraja hayo kimepungua kwa asilimia 0.78. Kiwango cha walioshindwa kimepungua kwa asilimia 3.62.

  Kwa upande wa shule bora kuanzia zenye watainiwa 25 na kuendelea ambazo idadi yake ni 264, Dkt. Ndalichako alisema Kifungilo ya mkoani Tanga ndio imeoongoza ikifuatiwa na shule ya wasichana Kibosho (Kilimanjaro) na Mzumbe na Kilosa zote za Morogoro.

  Nyingine ni Sanu Seminari (Manyara), Maua Seminari (Kilimanjaro), Uru Seminari (Kilimanjaro) Swilla (Mbeya) shule ya wasichana Marian (Pwani) na Nyegezi Seminari (Mwanza).

  Kwa upande wa shule kumi za mwisho katika kundi hilo na mikoa zilipo kwenye mabano ni, Popatla (Tanga), shule ya wasichana Maswa (Shinyanga),Fidel Castro (Pemba), Esacs (Dares Salaam), Muslim College na Zanzibar Commercial zote za Zanzibar.

  Zingine ni Lake (Mwanza),Rungwe (Mbeya)Ifunda (Iringa) na Shamiani (Pemba). Shule kumi bora zenye watahiniwa chini ya 25 kundi hilo limeongozwa kwa kiwango kikubwa na shule za seminari.

  Shule 10 bora katika kundi hilo na mikoa zilipo kwenye mabano ni St. Jemes Kilema seminari (Kilimanjaro), Kaengesa seminari (Rukwa), St. Joseph Kilocha seminari (Iringa)Dungunyi seminari(Singida),Likonde seminari (Ruvuma), Boabab (Pwani), Kaisho (Kagera), Hagafilo (Iringa), Katoke Seminari (Kagera) na Bangala Lutheran Junior (Tanga).

  Shule za mwisho katika kundi hilo, Dkt. Ndalichako alizitaja kuwa ni Tweyambe ( Kagera), Mvumi (Dodoma)Dodoma Central (Dodoma), Mount Kilimanjaro (Kilimanjaro), Sunni Madressa (Zanzibar), Besha (Tanga), Dongobesh (Manyara) Arusha Modern (Arusha)EDP Royal (Dar es Salaam) na Mairiva (Arusha.).

  Kwa upande wasichana kumi bora na shule watokazo kwenye mabano , Dkt. Ndalichako aliwataja kuwa ni Lulu Edward (Marian), Noelah Lugongo (Mbeya),Wema Kessi (Marian), Haika Malleko (Jangwani)Mercy John (Weruweru),Florencia Kimario (Marian),Zahara Nagri (Shaban Robert), Matilda Kululetera (Marian), Isabela Matandiko (St. Methew) na Jebby Gonza (Kifungilo).

  Walioongoza kwa upande wa wavulana katika kundi la kumi bora, Dkt. Ndalichako aliwataja kuwa ni Hussen Hamedu (Feza wavulana), Hajjy Abdul (Mpwapwa), Ibrahimu Shafi (Feza wavulana), Abraham Ambise (Mzumbe), Amani Mwazela (Ilboru),Quizelimana Bwenge (Mzumbe)Dominic Mwita (Pugu)Samson Mwita (Mwenge), Christian Charles (Kibaha) na Ilago Mabelya (Mzumbe).

  Alitaja wanafunzi kumi bora katika makundi yote kuwa ni Huseen Hamidu (Feza) huku nafasi ya pili na ya tatu zikishikiliwa na wasichana ambao ni Lulu Edward (Marian) na Noelah Lugongo (Mbeya).

  Nafasi ya nne imechukuliwa na Haji Abdul (Mpwapwa) huku msichana mwingine, Wema Kessy (Marian) akijitokeza kushika nafasi ya tano.

  Wengine ni Ibrahimu Shafi (Feza wavulana), Abraham Ambise (Mzumbe), Amani Mwazela (Ilboru),Quizelimana Bwenge (Mzumbe)Dominick Mwita.

  Alisema NECTA imefuta matokeo ya wanafunzi 54 waliobainika kufanya udanganyifu kati yao 49 ni wa kujitegemea na watano wa shule.

  Mbali na hiyo alisema NECTA imesitisha kutoa matokeo ya wanafunzi 170 ambao hawajalipa ada ya mtihani. Alisema baraza limesitisha kutoa matokeo ya watahiniwa wanne wa shule ya Rosemaria kutokana na mkuu wa shule hiyo kutolipa ada ya watahiniwa pungufu ya 25 hivyo yatatolewa baada ya ada hiyo kulipwa.

  Katika hatua nyingine, Dkt.Ndalichako alitangaza matokeo ya wanafunzi waliofanya mtihani wa stashahada ya ualimu ambapo watahiniwa 3,282 sawa na asilimi 90.19 kati ya 3,639 wamefaulu masomo yao yote huku wengine 335 wakishindwa baadhi ya masomo hivyo wanatakiwa kurudia. Alisema watahiniwa 22 hawakufaulu kabisa.


  majira
   
 16. T

  The Truth JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2008
  Joined: Oct 21, 2007
  Messages: 618
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  How come there are so few students with 'A' scores? I know CSEE and ACSEE exams are difficult but I would expect to see more 'A' and 'B' scores than what I saw from looking at few schools. Can someone post the papers/exams these students took for their ACSEE? I am interested to see what science (chemistry, physics, biology) and math papers looked like.
   
 17. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  A very valid request, Mr.(or Ms) Truth. It would be interesting to see what the papers look like. I am astounded to see that the following grades yielded DIVISION I (I saw these grades at center number P0110. That is Ilboru)

  Gen – S, HIST – B , KIS – A, ENG – E

  Is that top division performance?

  Let us see and analyze the papers, if it is possible. We can make valuable contributions to NECTA through JF

  Augustine Moshi
   
 18. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Naona mwaka huu vijana wengi hawajafaulu sana as it used to be. What is the problem? au ni utandawazi? in any case matokeo naona siyo mazuri sana as I was made to expect...
   
 19. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  nimejitahidi niyaone nimeshindwa nnaomba msaada wa maelekezo ya ziada
   
 20. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Nenda kwenye post No. 9 ya Mtanzania kwenye hii thread kuna link ya shule na centre namba zake ya mwaka jana. Uki-click utaenda moja kwa moja kwenye shule zote na namba zake..then you can chose any school you want to know of na kuendelea..Thats what I can offer..Iam not good in IT!
   
Loading...