FOREX! Ondoka sasa tuachie JF yetu

Mshana Jr,

Huu uzi ndo kwanza nauona kwa hisani yako!

Kwanza niseme jambo moja. Nilisoma uzi wa ONTARIO lakini nilikuta umefika mbali sana!

The guy is so good in influencer marketing... SO GOOD!

Anyway, sie wengine tumekuwa tukiishi kiujanja ujanja tu na kwahiyo vitu kama hivi sio vigeni kwetu. Nimefanya forex trading online na offline (was a banker back then). Nikipata pesa ya "kuchezea", hadi sasa nimekuwa niki-trade!

Kupitia uzi wa ONTARIO nilitaka kuongea mawili matatu kutokana na uzoefu wangu! Lakini kama nilivyosema, the guy is gifted in influencer marketing! Wadau hawakutaka kusikia lolote linaloenda kinyume na kile anachosema ONTARIO!!

Ilikuwa ni GET RICH SOON program!!!

And by the time, ONTARIO alikuwa hajataka chochote in exchange toka kwa wadau!! Mara nyingi alikuwa akisisitiza kutoa fursa tena huku akitumia pesa zake na yeye "hakuna chochote anachopata!"

Tunaofahamu hizi mambo tulijua it's a matter of time... Nilishafahamu alichokuwa anafanya by the time ni kutengeneza trust for future program... Referral Marketing program!!

Nishafanya sana referral marketing kwahiyo there's no way mtu anaweza kuni-trick! Hata 2011 hapa hapa JF niliendesha aggressive referral marketing program hadi nikapigwa permanent ban!! Si unajua JF wasivyo na uvumilivu kwenye referral links!!!

So, nikajua tu anachofanya ONTARIO ni maandalizi for referral marketing na madai kwamba yeye hapati chochote ni danganya toto!

And of course, siku chache baadae nikasikia jamaa anawapangia watu Broker wa ku-trade nao... ndo referral yenyewe!

But all in all; je, kuna lolote haramu kwenye shughuli ya ONTARIO?!

In a Cyber World, the answer is NO. Nchi nyingi, online forex trading ni legal. Hata US nako ni legal lakini ili kuwalinda US traders; wao wana orodha yao ya licensed brokers!

Hata hivyo, haimaanishi kila Broker asiyeruhusiwa ku-trade na US customers ni fraud. XM kwa mfano, ni moja ya respected brokers in Europe & Australia lakini hawana mandate ya ku-trade na US customers labda iwe wameanza miezi ya karibuni!

Nimetaja US kwa sababu jamaa wapo very sensitive na haya mambo!

Lakini pamoja na kwamba sioni UHARAMU wowote kwenye shughuli za ONTARIO, lakini kwa upande mwingine alikuwa anakiuka MIIKO ya forex trading.

Hapa anaweza kujitetea kwamba yeye sio broker na kwahiyo hana wajibu wa kufuata miiko husika!

Miiko ninayoongelea hapa ni kutosema wazi kuhusu risk ya forex trading. Alitakiwa kuwa professional kwa kuzungumzia na upande wa pili wa forex trading kwamba ni TOO RISK!!

Forex Trading ni money losing machine!

Kinyume chake, yeye alikuwa anazungumzia sana upande wa mavuno wakati probability ya mavuno is only 5%.

Tafiti nyingi zinaonesha 95% ya forex traders; hususani amateurs wanaunguza!

So, Brokers always wanawahitaji watu kama akina ONTARIO kwa sababu, theoretically, in every batch of new traders; 95% wataunguza na hiyo ndiyo inakuwa faida ya key players!
Mmh Chige asante sana kwa elimu na ufafanuzi huu.. Nimejifunza kitu hatimaye kuhusu FOREX.... Na ndio maana sikutaka kuwa na upande kwenye sakata zima la hii biashara.. In near future nitakutafuta kwa mawili matatu
 
Mmh kivipi mbona kama ndio wahanga wakuu au sijakuelewa?
Ukiangalia thread kama hizi wanaopinga ni wale ambao hawafanyi Forex. Na wanaofanya Forex wakija kutetea wanaongea au wanaonesha wao huwa wanafanikiwa tu. Yaani wanapata faida kila siku kitu ambacho mimi kinanishangaza, kwamba wafanya Forex wa JF ndio watu wenye akili kuliko wote duniani, wao ndio FOREX IS FOR THEM while the rest ndio wale 'forex is not for everyone'?
 
Back
Top Bottom