Forex : Mirejesho imepungua mno kulikoni?

Mpelijr

Member
May 17, 2010
89
11
Salaam Wadau,

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mada mbalimbali zinazokuja humu JF hasa za biashara na uwekezaji na nyingine nimechukua hatua moja mbele na kwenda kuzitekeleza...matunda si haba,ukiwekeza muda,nguvu na mtaji kiasi ikiambatana na maombi ahh faida utaiona.

Hapa karibuni pametokea uwekezaji mpya wa FOREX ambao umejizolea mashabiki,watafiti na wanachama wengi sana hadi kupelekea ile thread ya Ontario kutapika jinsi replies zilivyokuwa nyingi.Chochote kizuri huja na maswali mengi hasa kama ni kipya kwenye soko la watumiaji.Mimi kama mfuatiliaji mzuri ningependa kujikita zaidi kwenye mirejesho iliyokuwa inakuja kwa wingi sana hapo mwanzoni na yote ikiwa ni yenye habari chanya na zikihubiri mafanikio na hata zikashawishi wengine kufikiria kuacha kazi zao na kujikita zaidi kwenye hii biashara mpya.

Napenda kuwauliza wale waliokuwa wanaleta mirejesho mbona hapa karibuni imekuwa michache na ni baada ya muda mrefu ??? Au ile nadharia ya kwamba hakuna mshindi wa siku zote na biashara yenye boom wakati wowote imeanza kupata uhalisia ??

Chonde chonde msinipovushe...900 tu inapendezaaa :):)

Featured-Image-785x442.jpg
 
Mkuu ni kweli hii kitu wakati ule hata mm nilipata hamu ya kujiunga ila muda ulibana sasa HV wapo kimya sana wadau
 
''Watu tunanunua magari na majumba kupitia forex, we unauliza maswali ya mirejeshe, we zubaa watu tunapiga pesa we umelala naona uende ukafuge kuku na mbuzi tu''. ALISIKIKA MDAU MMOJA WA FOREX AKIMJIBU JAMAA FULANI KWENYE NYUZI FULANI.

Tukutane kwa Wazee wenzangu wa kuweka mzigo, jukwaa la michezo, mambo ya forex na mimi nangoja mrejesho.
 
Hahahaaaah hii kauli naikumbuka kabisaaaaa...mwe!! siku hizi hawaleti ndo maana tunashangaa.Maybe kwa sasa wangekuwa wanawekeza hata kwenye SGR !!
 
dah mm na ushiriki wangu wote wa betting forex roho ilikataa 100%
kwanza mirejesho yake ilikua sio ya kiuhalisia mtu anakuja tu "oooh nimepata mshahara wangu kwa siku 3 najuta kwann nimeajiriwa" hii nilijua tu lugha ya biashara

2.nilifatilia watoa mirejesho ndo wale wale kila comment na ndo hao hao wanao wa-attack ambao walikua wakidoubt

3. mm hua siamin kitu ambacho unashawishiwa tu kwa upande mmoja(faida) yan kila aliekua akichangia yy anapata faida tu hakuna hata mmoja aliekula loss

4. hili ndo la msingi
Hakuna tajiri duniani atakaekupa straight njia aliyoitumia yy kutajirika wao watakupa mawazo ambayo yatawasaidia wao wazidi kutajirika kwa kukunyonya ww
alibaba anashawish watu wajiajiri kwa kufanya online business(yy aendelee kupiga faida)
billgate anahamasisha dunian matumiz ya kompyuta ili yy aongeze wateja wa cd zake za window)

wengi wanaficha mf
bakheresa daily anadanganya watu alikua fundi viatu

sasa Ontario kuja humu na straight idea yake inayomtajirisha eti anataka kila mtu atajirike mm Sikuamini 100% sijajua tu hw yy amewapiga vipi wajinga wake

Najua mtakuja na mapovu karbuni nna nguo nying za kufua povu lenu litanisaidia
 
wajinga wake amewapiga kwenye hela za mafunzo zile laki laki..

ile ndio ilikuwa main goal ya ontario..

dogo ni motivational speaker ana kipaji na ushawishi sana.. toka thread yake ya trekta, mara ufugaji mara forex yeye haongelei hasara zaidi ya faida tu ili akuteke akili... alianzia mbali sana kuwavuta watu wajae kwenye 18 ndipo akawapiga na forex training

dah mm na ushiriki wangu wote wa betting forex roho ilikataa 100%
kwanza mirejesho yake ilikua sio ya kiuhalisia mtu anakuja tu "oooh nimepata mshahara wangu kwa siku 3 najuta kwann nimeajiriwa" hii nilijua tu lugha ya biashara

2.nilifatilia watoa mirejesho ndo wale wale kila comment na ndo hao hao wanao wa-attack ambao walikua wakidoubt

3. mm hua siamin kitu ambacho unashawishiwa tu kwa upande mmoja(faida) yan kila aliekua akichangia yy anapata faida tu hakuna hata mmoja aliekula loss

4. hili ndo la msingi
Hakuna tajiri duniani atakaekupa straight njia aliyoitumia yy kutajirika wao watakupa mawazo ambayo yatawasaidia wao wazidi kutajirika kwa kukunyonya ww
alibaba anashawish watu wajiajiri kwa kufanya online business(yy aendelee kupiga faida)
billgate anahamasisha dunian matumiz ya kompyuta ili yy aongeze wateja wa cd zake za window)

wengi wanaficha mf
bakheresa daily anadanganya watu alikua fundi viatu

sasa Ontario kuja humu na straight idea yake inayomtajirisha eti anataka kila mtu atajirike mm Sikuamini 100% sijajua tu hw yy amewapiga vipi wajinga wake

Najua mtakuja na mapovu karbuni nna nguo nying za kufua povu lenu litanisaidia
 
Wako busy wanatengeneza pesa, mirejesho watakuwa wanaposti maisha yao yote?
 
Vyuma vimekaza balaa.
Hakunaga kitu rahisi katika maisha.

Forex ni biashara ya Akili kubwa, sio issue ya kuunga unga, kama kuna mtu alidandia hiyo biashara lazima tu itakula kwake.
ni kweli hii ni biashara ya akili kubwa,watu kama mimi hii kitu kwangu imekua mteremko,mpk sasa nimesoma vitabu 8 vya forex,nimesoma articles 56,nimesikiliza youtube kibao kutoka kwa website bora zaidi duniani,nimepiga 1 week training,nimepata quality education,nimeielewa ins and out na sasa nipo kwenye mentorship na mentor bora zaidi,MR CRE na sasa nimeanza kua mtaalamu.soon nami nitakua mwalimu wa wengine.ninasoma sana.
Hii kitu ukiimaster utakua unapiga pesa,ila inahitaji uinvest time kupata elimu yake na kujifunza zaidi,Forex is simple.
TMT
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom