Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,551
- 19,419
Zamani sana ile miaka ya themanini kulikuwa na wimbo ulioimbwa na Cosmas Thobias Chidumule wa mlimani Park usemao "Mtoto Akililia Wembe." Nadhani wimbo huu ulikuwa umeelekezwa na akina Muhudin Gurumo na wenzake waliohama Mliman Park kwa mpigo na kujiunga na Safari Sound ya Hugo Kisima. Bwana huyu Kisima alikuwa anajulikana kwa kuwabana sana wanamziki wake (kwa wale vijana wa siku hizo mtakumbuka yale yalichomkumba Mwanamuziki Skassy Kasamabula aliposhindana na Hugo Kisima). Lakini bado aliwarubuni akina Muhudini kuwa angewafanyia mambo mengi mazuri kuboresha maisha yao, lakini walipofika kule wakakutana na moto: walisaini mkataba ule bila kuangalia fine prints.
Na sisi tuliahidiwa mengi kutoka kwa kaburu tukaingia mkenge; leo tunaanza kuipata. Viongozi wetu hawakuangalia fine prints na matokeo yake ndiyo hivyo: shirika letu la ndege hoi, kiwanda chetu cha kibuku hoi, mazingira ya kazi kwa watu wetu wengi ni hoi, the list goes on.
Wakati nia yetu ya kuwaleta hawa investors ilikuwa ni kuboresha maisha ya raia wetu kwa kuwapatia ajira, na vile vile kuongeza pato la serikali kwa kulipa kodi, sidhani kama tumeyapata hayo. Kuna kazi nyingi zimebaki kwa wasouth afrika ikiwa hata kazi za uhudumu; hii ni hatari kweli kweli. Kazi nyingi zinazotolewa kwa watu wetu zimekuwa za manyanyasonyanyaso tu.
Tulililia wembe