Forbes yaitaja Tanzania kuwa Nchi ya Pili Duniani inayofaa kutembelewa mwaka 2021

Habari Wana Bodi!
Tanzania imeendelea Kung'ara na kusemwa Sana katika anga za Kimataifa.
Bila kupoteza twende kuona namna inavyozidi Kung'ara;

1. Jarida la Forbes limeitaja Tanzania Kama ndio nchi ya pili ulimwenguni inayofaa kutembelewa mwaka 2021 habari kamili soma hapa chini

Jarida la Forbes limetaja orodha ya nchi 21 duniani zenye maeneo mazuri zaidi ya kutembelewa kwa mwaka 2012. Maldives kisiwa kidogo kilichoko kwenye bahari ya Hindi imetajwa ya kwanza kwenye orodha hiyo, na Tanzania hasa mbuga ya wanyama ya Serengeti imetajwa kuwa ya pili inayofaa kutembelea. Nchi nyingi ya Afrika Mashariki iliyopo kwenye eneo hilo ni Rwanda ambayo iko kwenye nafasi ya saba.

Orodha ya kumi bora ni pamoja na
1. Maldives
2. Tanzania (Serengeti)
3. Antarctica
4. Ziwa Powell katika jimbo la Utah Marekani,
5 Bonde la Jackson, Wyoming
6.Cucso Peru
7. Rwanda
8. Denali National Park, Alaska
9. Porto Cervo, Italy
10. Sonoma County, California.

Chanzo cha Habari CRI Kiswahili.

2. Tanzania imeteuliwa kuongoza Kamati nyeti ya Umoja wa Mataifa. Habari kamili soma hapa chini;

"Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya hati za utambulisho ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Newyork kwa mwaka 2020/2021, uteuzi huu ulipendekezwa na ofisi ya Rais wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa na kuteuliwa kwa kauli moja na wajumbe wote wa kamati hiyo" Millard Ayo.

Ni Mara ya kwanza Tanzania kushika nafasi ya kuongoza Kamati hii nyeti ya Umoja wa Mataifa.

3. Tanzania ndo nchi pekee duniani iliyotangazwa na Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa chini ya WHO inayohusiana na takwimu za korona Kama Taifa pekee ambalo halina maambukizi Wala athari za virusi vya Corona kwa wiki46. Na ikaongeza kwa kusema hata wananchi wa Taifa Hilo wapo salama na maisha yanaendelea Kama kawaida.

My take; Mungu anaipenda Tanzania na Watanzania wake hivyo naomba Tuendelee kuliombea Taifa letu lizidi Kung'ara zaidi na zaidi.
#Mungu ilibariki Tanzania na Watanzania wake
#Mungu wajalie hekima na busara Viongozi wetu katika kuliongoza Taifa lako hili teule.
I love my country 🇹🇿.
 
Pia Tanzania iliandika historia ya kipekee kuwahi kutokea duniani kwa kupanda kiuchumi kutoka Uchumi wa chini(Masikini) Hadi uchumi wa kati, kipindi ambacho mataifa mengi duniani yalikuwa kwenye anguko la kiuchumi kutokana na madhara ya virusi vya Corona.
 
Mlima kilimanjaro.
serengeti.
Mikumi.
Ngorongoro.
Lake Manyara.
Vyura,Jiwe linalocheza, maji ya moto.
Kijungu, kisibha, ziwa ngozi,
Bahari ya Hindi.

NA MENGINE YOOOTE.

HIVI VYOTE NI MBWEMBWE TU HAVIJATUSAIDIA CHOCHOTE NDIO TUNAZIDI KUWA MASIKINI.

LAANA YA RASLIMALI eg CONGO.
 
Kama Si Mungu, Tanzania na Waseme sasa!!!

Asante Mungu, mbali na yoote maovu ambayo tunajua kabisa kwamba yapo nchini mwetu,

Kwani Sisi ni binadamu tu kama watu wa mataifa mengine, ni watenda dhambi kama watu wa mataifa mengine, Hatustahili kama ilivyo Kwa waovu!!

Umetupendelea bule Mungu wetu, Asante Kwa kutuponya na maradhi ya Corona, Umetupendelea Tu, hatujivuni, Bali wewe mwenyewe tenda Kwa ajiri yako wewe

Kama umetulidhia Mungu, basi tutenge mbali na maadui wa nje na ndani, uwafedheheshe Kwa kila shali zao, waaibishwe na zao shali!!
Pigana nao wasioitakia mema nchi yetu Kwa ajiri ya utukufu wako Jehova shamma

Mungu ibariki TANZANIA, Mungu bariki Africa
 
Habari Wana Bodi!
Tanzania imeendelea Kung'ara na kusemwa Sana katika anga za Kimataifa.
Bila kupoteza twende kuona namna inavyozidi Kung'ara;..
Hiyo ya 3 kwa kweli itawanyima Lissu na Zitto usingizi.....sijuwi wataipokeaje uko walipo.
 
Forbes yaitaja Tanzania kuwa nchi ya pili duniani inayofaa kutembelewa mwaka 2021...
Hatukawii kuwasikia Kenya wakidai Serengeti ipo kwao kama ilivyo Kilimanjaro na Tanzanite.

Wakiendeleza chokochoko tutajenga Ukuta Serengeti Wanyama wasihame kwenda Kenya na Kilimanjaro wasipande Mlima 🤣🤣🤣🤸‍♂️
 
Kuuliza si ujinga hivi ofisi ya makao makuu chadema ile kama banda la kuuza mkaa imeshawahi pokea mgeni toka nje hata mmoja?
 
Back
Top Bottom