For serious & single ladies: Nipo kwenye harakati za kutafuta mke mwema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

For serious & single ladies: Nipo kwenye harakati za kutafuta mke mwema

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Taluma, Jan 22, 2011.

 1. Taluma

  Taluma Senior Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu mabibi! Nipo kwenye harakati za kutafuta mwanamke wa kuishi naye hapa Tanzania: Sifa za mke ninaye mtafuta ni kama ifuatavyo;
  • Awe na umri kati ya miaka 25 hadi 32
  • Asiwe amewahi kuolewa kwa ndoa ya aina yeyote ile
  • Asiwe amewahi kuishi na mume kama mume wake (zile za kuvutana kimya kimya bila ndoa)
  • Awe na umbo linalovutia (si bonge sana, si mwembamba sana) ie good looking ...wale wa mkorogo au mawigi....no please...!ninapenda natural beauty!
  • Elimu angalau form four na kuendelea
  • Awe mfanyakazi au mjasiliamali
  • Awe ni mkristo -RC au kama ni dhehebu lingine (sio ulokole) awe tayari kuwa RC
  • Asiwe na kuburi kabisaaaa
  • Asiwe na hasira, jaziba au vuvuzela
  • Asiwe mchafu, awe anapenda usafi wa mwili wake, nyumba, mazingira anayoishi, viwalo vyake etc
  • Awe mke mwenye hekima, busara na adabu kwa wakubwa wake
  • Awe mke anayeheshimu mila na desturi za kiafrika...asiwe adicted kwenye western culture tu.
  • Awe tayari (if god wishes) kuzaa watoto wasiozidi wawili tu
  • Awe tayari kupima VVU -wakati ukiwadia
  • Awe mtanzania wa kabila lolote
  Sifa zangu;
  • Elimu chuo kikuu -na professional certificate
  • Umri miaka 34
  • Kabila Mnyalu
  • Mfanyakazi na mjasiliamali
  • Nina huruma sana for the ''needy'' people
  • Nina kunywa ....hasa weekends!
  • Nina watoto wawili - mama yao tuliachana (hakukuwa na ndoa yeyote) baada ya kushindwa kuelewana
  • Niko rafu (kuvaa, kula) lakini napenda mke asiwe rafu kama mimi
  • Nina jiamini
  • Ni mrefu - 1.67m
  • Uzito 84kgs
  • Occassionaly huwa naenda club
  • Ni mweusi ila kidogo maji ya kunde
  • Napenda muziki - wa dini na uraiani
  Tafadhali kwa anaye endana na wasifu huo na ambaye hupo tayari kuishi na mimi pamoja na wasifu wangu hapo juu, naomba tuwasiliane kwa njia zifuatazo;
  Tafadhali naomba kwa wale walio serious tu ndo wanitumie PM au email, hakuna mzaha au utani ninamaanisha niliyoyaandika!

  Asante na Mungu awabariki sana!
   
 2. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  Akitokea mwenye sifa kama zako hapo kwenye red?
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ama kweli unamaanisha.
  Kila la heri.
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi siku hizi mapenzi mpaka CV.....? kweli haya ni maendeleo......
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmmhhhhh
  kwa kweli
  all the best dear...
   
 6. Taluma

  Taluma Senior Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...ukweli na uwazi utafanya watu kuishi kwa furaha na amani mkuu!
   
 7. Taluma

  Taluma Senior Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Babaubaya,

  Nafikiri kuna sehemu nimesema asiwe aliwahi kuolewa au kuishi na mume hata kimyakimya.....! kama amezaa watoto wawili hii itakuwa ngumu....kama mtoto mmoja na hakuwahi kuishi na huyo baba mtoto hiyo powa tu tutaelewana!
   
 8. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Vijana vituko haviishi.... siku hizi kutafuta mke mpaka tunatangaza :kev:
   
 9. Taluma

  Taluma Senior Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Babua,

  Siku hizi wakoloni wanatubana sana kwenye uwanja mmoja, tunakosa nafasi za kupanua uwanja wa kuwindia, si jumamosi si jumapili unatumika....kwa hiyo hii nayo ni njia mdala na nzuri ya kuongeza wigo unakoweza patia wachumba na marafiki! Zamani nyie hamkuweza kutumia njia hii kwa sababu haikuwepo, ingekuwepo na nyie mngetumia tu.....!
   
 10. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Vuvuzela ndo wapi tena,naona kama nina vigezo ila sijui hao vuvuzela ndo wapi nisije kuwa mmoja wao???
   
 11. s

  shosti JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hii si haki,wewe una watoto unataka asiye na watoto aje mlee watoto wako,kwanini usitafute mwenye mtoto mlee watoto wenu
   
 12. Taluma

  Taluma Senior Member

  #12
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Michelle,

  kama Vuvuzela imekuchanganya utanisamehe, lakini hii ina maanisha ni mwanamke anayeongea sana/anachonga sana/anapayuka sana hata bila mpangalio...hope umenipata sio?
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hii CV si mchezo utapata tu ndugu usijali
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hapo na mimi sijaelewa ila ngoja tumuachie mwenyewe bwana
   
 15. Taluma

  Taluma Senior Member

  #15
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...shosti, kuna post mmoja hapo juu nimejibu nafikiri ya babaubaya kwamba....kama atakuwa amezaa basi isiwe zaidi ya mtoto mmoja! Ili mimi na yeye tuzae mmoja tu jumla wanne....huyu mmoja ni wakuimarisha ndoa tu! unajua mambo yetu ya kiswahili mama asipozaa inakuwa balaa kweli kwenye ukoo....nadhani upo hapo!
   
 16. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Asante Taluma,

  Sasa hao watoto, mkeo utakayemuoa ndo atakuwa anawalea au mama watoto mwenyewe we unatunza tu????
   
 17. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Kuna mmoja ana sifa zoote lakini ana matatizo ya kuwahurumia watu.... sijui kama atakufaa
   
 18. s

  shosti JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mwenzio hatanii huyo huoni kama anakufaa wewe,dharau tu kwa wadada.
   
 19. Taluma

  Taluma Senior Member

  #19
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tulikubaliana mama yao atakaa nao mpaka wafikishe miaka 7, then nitawachukua wote so pia nategemea mke nitakaye mwoa awe tayari kunisaidia kuwalea pia....! asante kwa kuuliza hili swali ilibidi niliweke wazi!
   
 20. Taluma

  Taluma Senior Member

  #20
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Bora useme wewe......! humu hakuna usanii kabisa very serious na huu mchakato!
   
Loading...