For Great Thinkers only: Zitto Kabwe huchukua wapi 'imprest' ili kufanyia 'retirement'?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,173
25,446
Leo Bungeni Dodoma,Spika wa Bunge Ndugu Job Ndugai alisimama na kuzungumzia mambo mbalimbali kuwahusu Wabunge Zitto Kabwe na Tundu Lissu.

Kuhusu Zitto,Spika Ndugai alikemea vikali tabia ya Zitto kutoa taarifa za uongo na kuupotosha umma kupitia mitandao ya kijamii hasa twitter. Alitolea mfano wa twit ya Zitto iliyoshutumu Ofisi ya Spika kukalia Ripoti ya CAG.

Spika Ndugai alionyesha kushangazwa na namna Zitto anavyopata taarifa za siri na nyeti na kuwaasa Wabunge kutomchora vibaya Spika kwenye jamii. Pia,aliwaasa Wabunge kuacha kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji.

Katika hali isiyo ya kawaida,Spika Ndugai alisikika akisema kuwa yawezekana tabia ya Zitto kusema uongo ni katika 'kuretire' imprest bila kutaja ni wapi na kupambanua kwa kina.

For you JF great thinkers, dongo la Spika kwa Zitto lilimaanisha nini? Zitto huchukua wapi imprest anazolazimika kuziretire kwa namna yoyote iwayo?
 
Zitto ni agent wa mabeberu. Kwa Tanzania ya sasa iliyogawanywa kati ya wao na sisi ni nafuu kuwa upande wa mabeberu.

Mabeberu ndio wanaweza kusema na sisi huku hohehahe tukakaa na kusikiliza. Walisema turudishe watoto waliopata ujauzito shule tukakalishwa. Wakasema turekebishe sheria ya kizalendo ya takwimu iloyopitishwa na bunge letu la kizalendo tukakubali (kimya kimya), rais akakaa. Na sasa hata hii sheria ya mfalme wa vyama vya siasa wataikataa na tutakalishwa tena.

Serikali hii inawatambua wanaume walipo. Tuliwaona wakwepa matrilioni ya kodi walikuja, mfalme wetu akaingia nao chumbani, akatoka akatuambia watanzania wote HAWA NI WANAUME.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyinyi mkikosolewa kosa ,mbona mnawalaumu wabunge wanaowakosoa tu .mmekosa kwenye target zenu zote mpaka za uchawi ndio mnamchukia kweli zitto , waganga wenu wa kanda ya ziwa wameshindwa na ziwa Tanganyika
 
Leo Bungeni Dodoma,Spika wa Bunge Ndugu Job Ndugai alisimama na kuzungumzia mambo mbalimbali kuwahusu Wabunge Zitto Kabwe na Tundu Lissu.

Kuhusu Zitto,Spika Ndugai alikemea vikali tabia ya Zitto kutoa taarifa za uongo na kuupotosha umma kupitia mitandao ya kijamii hasa twitter. Alitolea mfano wa twit ya Zitto iliyoshutumu Ofisi ya Spika kukalia Ripoti ya CAG.

Spika Ndugai alionyesha kushangazwa na namna Zitto anavyopata taarifa za siri na nyeti na kuwaasa Wabunge kutomchora vibaya Spika kwenye jamii. Pia,aliwaasa Wabunge kuacha kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji.

Katika hali isiyo ya kawaida,Spika Ndugai alisikika akisema kuwa yawezekana tabia ya Zitto kusema uongo ni katika 'kuretire' imprest bila kutaja ni wapi na kupambanua kwa kina.

For you JF great thinkers, dongo la Spika kwa Zitto lilimaanisha nini? Zitto huchukua wapi imprest anazolazimika kuziretire kwa namna yoyote iwayo?
Sasa jitu limeshazibitika ni liongo kuna haja gani kujadili alichosema?
Labda kwa mbulula wenzake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zito ni haraka tu ya mambo ndo humponza
Kwa kauli ya spika kua barua kaipata tarehe 16 wakati kauli ya zito ilikua tateh 8 lakini ni ukweli usiopingika kuwa barua ndo hiyo hiyo aliyopokea tareh 16 uongo wa zito ni tofauti ya upokeaji wa barua tu lakini ni ukweli barua ndo hiyo..
Kwa maana hiyo zito anawatu wanampa taarfa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto anajua mengi na ndio maana anajiamini.
Licha ya kejeli zisizo na tija endelevu hata kwa CCM, taifa la Tanzania linahitaji sana, sasa kuliko wakati mwingine wowote katika historia, watu wengi zaidi kama ZZK na TAML.

Ninachoomba ni kuwa MUNGU awalinde dhidi ya "wasiojulikana" ambao yawezekana kiu yao ya damu haijakidhiwa (quenched).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom