food supplements (?)

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,745
7,781
Leteni Maswali ya Kiafya Niwasaidie

--------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwa julisha wana JF kuwa nakaribisheni maswali mafupi mafupi yanayohusu tatizo lolote la kiafya.Maswali yote yatajibiwa mara moja kwa wiki iwe ni tatizo ulilonalo wewe binafsi au ndugu,jirani,rafiki au mtu yeyote unayemfahamu,Kumbuka yawe mafupi ili watu wengi zaidi wapate nafasi ya kushauriwa na mimi.Nitakupa ushauri kadri ninavyoweza.Usiwe na wasiwasi niko ktk profession hii
__________________
Machozi ya Masikini ni dhambi za MAFISADI
NANI ATAMLILIA FISADI SIKU AKIFA?-FISADI MWEZAKE!!

...Mkuu shukrani kukaribisha maswali,

kwa sababu fulani fulani zilizo nje ya uwezo wangu, naamini sipati balanced diet. Mnanishauri nini kuhusu advantages na disadvantages za matumizi food supplements (tablets/Capsules na Drinks)... mfano Multi Vitamins, Cal mag, codliver oil, etc...

Kwanini baadhi ya watu wana opt kwenye GNLD products, hasa jijini Dsm ambako naamini fresh products zipo za kutosha kukidhi mlo kamili? kama 'nawe' ni mwanachama wa GNLD, waweza toa adnantages a hizo products bila kugusia faida (points) zitokanazo na wewe kuwa intemediatery?

...
 
Swali zuri sana: Kwa nini watu wana opt kwenye food supplements za GNLD. Jibu halisi la swali lako linapatikana katika swali kwa nini tunakula chakula?

Tunakula ili miili yetu iweze kupata virutubisho, miili ivitumie hivyo virutubisho kuupa mwili nguvu uweze kufanya kazi yake vizuri. According to World Health Organization (WHO) Tunapaswa kula kama ifuatavyo:

1. nafaka ambazo hazijakobolewa (lipids and sterols)
2. mboga na matunda (fruits and vegetables) 5 to 9 types a day
3. protein
4. mafuta yasiyoganda kwa urahisi (unsaturated fats)
5. carbohydrates (sukari)

Mpangilio huo hapo juu unaashiria umuhimu wa chakula, yaani sehemu kubwa ya chakula chetu inapaswa kuwa lipids, ikifuatiwa na fruits and veg, protein, unsaturated fats na sukari.

Lakini asilimia 99 ya watu hula kinyume: sehemu kubwa tunakula sukari na mafuta yanayoganda, protein, matunda na mboga kidogo sana, nafaka zisizokobolewa ndio hatuli kabisa.

Nini matokeo ya kula kinyume na maagizo ya WHO? MAGONJWA:
1.Uchovu
2.Kisukari
3.Blood pressure
4.Cancer
5.Impotency
6.Heart attack
7.Stroke etc.

Magonjwa haya yote hayatibiki hospitali.

Kwa nini watu wasile fresh food? Ukweli ni kwamba ni vigumu mno kupata virutubisho vyote vinavyotakiwa mwilini kwenye vyakula vya siku hizi. Kwa nini? Sababu ni nyingi sana mfano uharibifu wa mazingira umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza uwezo wa ardhi. Pili muda wa kuvuna vyakula shambani mpaka kumfikia mlaji unachangia kwa kiasi kikubwa sana upotevu wa virutubisho. Chukulia chungwa ambalo lina vitamin c nyingi sana, dakika 15 tu baada ya kuchumwa vitamini c yote inakuwa imeondoka na kubaki fructose tu! Sasa piga hesabu wewe mwenyewe uone chungwa linalotoka Tanga kuja Dar es Salaam litakuwa katika hali gani? Na hii ni hivyo hivyo katika vyakula vyote.

Suluhisho ninini?

Solution ni kupata vyakula mbadala (food supplements za GNLD)! Kwa nini? Kwa sababu ni vyakula halisi vimetengenezwa kwa technologia ya hali ya juu kuhakikisha mwili unapata exactly unachotakiwa kupata (natural, hakuna chemical hata moja). Kinachotenganisha GNLD na wengine ni Scientific Advisory Board (SAB) ambayo husimamia utengenezwaji wa supplements hizi. Ubora wa SAB, umepelekea serikali ya marekani kuwapa kazi ya ushauri kuhusu mambo yote ya kilimo na chakula.

Kuna mis conception kuwa supplements ni dawa, sio dawa! Bali watu wanapoumwa wakizitumia wakapona wanaamini wamekula dawa, ukweli ni kwamba mwili unapopata unachohitaji sio rahisi kuumwa.
Pia watu ufikri kuna chemicals, katika GNLD products hakuna chemikali hata chembe moja, kwa sababu supplements hizo hutengenezwa kwa mimea halisi.

Kama unataka maelezo zaidi juu ya Bidhaa za GNLD wasiliana nami kwa kupitia email hii professionaleagle@gmail.com

Knowledge is not power rather the use of knowledge is POWER
 
...Ssebo nawe ni mwanachama pale kwa mama Juma nini? Thanks. Sasa je? food supplements gani hizo ninazohitajika kula kila siku? je, kila siku nikila kidonge cha multivitamin tofauti yake itakuwa nini na kunywa mfano vita square au cal-mag?
 
There is a documented concern that food supplements in the form of pills containing vitamins and minerals are not properly digested and absorbed by the body leading to most of the nutrients to be urinated.

Do your research before engaging in needless consumption.There is no true substitute for the real thing.
 
Mchongoma,
Kweli mimi ni mwanachama haswa tena pale kwa mama Juma you are right.Kwenye swali lako kuna maswali mawili:
1. Supplement gani unazohitaji kula kila siku?
2. Tofauti kati ya mult vitamini na vitasquare na calmag

Majibu:
1. Kama ukiangalia katika post yangu ya mwanzo nilisema WHO wana recomend tule kama ifuatavyo:
1. Lipids and Sterols from whole grain (tumia tre en en grain concentrate)
2. Fruits and Vegetable (tumia carotenoid complex)
3. Protein ( pata nutrishake)
4. Unsaturated fat ( pata Omega 3 fatty acid)
5. Sugar and carbohydrates ( hii hakuna haja ya supplement maana tunapata katika vyakula vingi.

2. Tofauti ya mult vitamin na Vita square, calmag
Mult vitamin sitaizungumzia maana siijui. Ila vita square ndio lipids anad sterols ya watoto. Calmag ni kifupi cha calcium na magnesium, haya ni madini muhimu sana mwilini kwa ajili ya mifupa na uzalishaji wa damu.
 
Pundit,
Nakubaliana na wewe kuhusu baadhi ya supplements za makampuni mengine kuwa na kasoro kama uliyoitaja, lakini kinachoitofautisha GNLD na kampuni zingine ndio hilo suala la ubora, thats why it has been around for over 50 years!
Nakushauri na wewe ufanye uchunguzi wako find the credibility of Scientific Advosory board you will know the science behind Gnld product. It is based in nature backed by science
 
Ssebo,

Yaani hapa umeongea kama unatetea chama tu bila kutoa a scientific reason.

Sababu niliyoitoa mimi ya ku diss multivitamins ni kwamba ukinywa vidonge mwili haubreak down na ku absorb nutrients, hivyo unaishia kuzikojoa tu.

Sasa tuelezee wewe bidhaa za GNLD zinawezaje kuondokana na tatizo hili?

Nichukulie mimi kama potential mteja, huwezi kumwambia mteja anayekuuliza swala hilo kwamba "kampuni yetu imekuwa katika biashara miaka 50 hivyo bidhaa zetu ni nzuri" kwa hiyo kafanye research mwenyewe.

Aristotle aliwachuza watu kwamba dunia ipo katikati ya ulimwengu na kila kitu kinaizunguka siyo kwa miaka 50, bali kwa miaka 1800.While the longevity of an establishment may be indicative of its industriousness, it is by no means an absolute guarantee of quality.

Mwaga data, kama huna sema.
 
Hivi unajua Ssebo na Mchongoma ni mtu mmoja au lao moja?

Wanaleta michongo ya Ki-Nigeria. Hata hawajui targeted market yao ni watu wa aina gani. We JF hapa utamdanganya mtu na salemanship ya kuulizana maswali unayajijibu mwenyewe. Halafu unatoa contact info ya kuuza supplements hapo hapo!

Wangejaribu ku take advantage ya unwary people vijijini huko ningeona kweli wame tafiti market niche yao. Lakini kwenye tech-savvy demographics kama JF unataka ulete U doctor Maji Marefu hapa!

Duuh, umewakamata. Halafu ulivyo anza nao, wala huku challenge profession yao au veracity ya madai yao. Umemshauri Ssebo awe makini bila kujua ni wale wale. Wakaanza kujitetea ovyo, yakaibuka mengine.

Hawarudii tena!
 
...Mkuu shukrani kukaribisha maswali,

kwa sababu fulani fulani zilizo nje ya uwezo wangu, naamini sipati balanced diet. Mnanishauri nini kuhusu advantages na disadvantages za matumizi food supplements (tablets/Capsules na Drinks)... mfano Multi Vitamins, Cal mag, codliver oil, etc...

Kwanini baadhi ya watu wana opt kwenye GNLD products, hasa jijini Dsm ambako naamini fresh products zipo za kutosha kukidhi mlo kamili? kama 'nawe' ni mwanachama wa GNLD, waweza toa adnantages a hizo products bila kugusia faida (points) zitokanazo na wewe kuwa intemediatery?

...

..ushauri ni kuwa ujitahidi kula vyakula halisi. mungu si mjinga alipomfanya bin adamu achimbe ardhi na kupanda mimea!

..hiyo iwe ni dharura tu.
 
..ushauri ni kuwa ujitahidi kula vyakula halisi. mungu si mjinga alipomfanya bin adamu achimbe ardhi na kupanda mimea!

..hiyo iwe ni dharura tu.

Lakini ushauri wa thread ulikua uwaandikie email wakuuzie supplements. Ilikuwa ni racket!
 
Pundit,

Hivi unajua Ssebo na Mchongoma ni mtu mmoja au lao moja?

Wanaleta michongo ya Ki-Nigeria. Hata hawajui targeted market yao ni watu wa aina gani. We JF hapa utamdanganya mtu na salemanship ya kuulizana maswali unayajijibu mwenyewe. Halafu unatoa contact info ya kuuza supplements hapo hapo!

Wangejaribu ku take advantage ya unwary people vijijini huko ningeona kweli wame tafiti market niche yao. Lakini kwenye tech-savvy demographics kama JF unataka ulete U doctor Maji Marefu hapa!

Duuh, umewakamata. Halafu ulivyo anza nao, wala huku challenge profession yao au veracity ya madai yao. Umemshauri Ssebo awe makini bila kujua ni wale wale. Wakaanza kujitetea ovyo, yakaibuka mengine.

Hawarudii tena!

...Naam kuhani Mkuu,

kuna watu wangu wa karibu ambao ni wanachama wazuri wa GNLD products, lakini mimi si mtumiaji. Hapa nilipo kuna maduka makubwa tu ya natural remedies kina Holland and Barret etc etc, nao wanauza vitu kama Zinc, Cod liver oil etc etc... kwa sababu fulani fulani na huu umri wangu nikaona aah, acha nami nijaribu kutumia food supplements, ndio maana nikalileta swali hili...

Ni haki yako kutoa maoni yako, hata kama sio sahihi lakini umetumia demokrasia yako, lakini usiipotoshe jamii kwamba Ssebo na mchongoma ni mtu mmoja au lao moja, hapo kiukweli umekosea Mkuu na kututaka radhi ni hiari yako, sikulazimishi.

Uungwana ni vitendo, au swali langu likumekukwaza Mkuu? si ungeacha kujibu tu ukaenda ku post mengine kwenye threads nyingine? Nyakati nyingine ni bora kunawa mikono kwanza kabla ya kumnyooshea mwenzio kidole!

Shukran.
 
Mult vitamin sitaizungumzia maana siijui. Ila vita square ndio lipids anad sterols ya watoto. Calmag ni kifupi cha calcium na magnesium, haya ni madini muhimu sana mwilini kwa ajili ya mifupa na uzalishaji wa damu.

naam ndugu yangu; haka kakopo hapa kanaitwa MULTIBIONTA Probiotic Multivitamin;

Nutrition Information zake ina vitamin A, D, E, C, B1, B2, B6, B12, Niacin, Folic Acid, Biotin,, Panothenic Acid, Calcium, Phosphorus, Iron, Magnesium, Zinc, Iodine, Manganese, Chromium, Molybdenum, Selenium, Chloride, na Pottasium.

Yule dakitari wetu humu naye sijui kaenda wapi, aaah, mimi acha niendelee kuzitumia bana, so long as si exceed the reccomended intake najua nafidia lishe bora niloiacha africa.
 
..ushauri ni kuwa ujitahidi kula vyakula halisi. mungu si mjinga alipomfanya bin adamu achimbe ardhi na kupanda mimea!

..hiyo iwe ni dharura tu.

ushauri mzuri mkuu, nitaufanyia kazi ingawa yule mtaalamu wetu humu naye ningefurahi zaidi naye angeleta ufafanuzi wake.

shukran.
 
Mchongoma, ulipo anzisha thread ume quote daktari akialika maswali. Ume quote kutoka thread gani? Na kwa nini hukwenda huko kuuliza maswali yako?
 
...never mind nimeipata wapi hiyo thread, uki search utaipata, na kwanini nimeanzisha thread nyingine hilo ni uamuzi wangu kama mwanachama huru wa JF kama ulivyo wewe na haki ya kuanzisha thread unayoona itaeleweka zaidi, au kwakuwa nawe ni Moderator humu ndani.

Kwangu mimi, la msingi ni hoja yako kuwa mimi ndio ssebo au letu moja, na kwamba hapa tunacheza racket kama za ki Nigeria. Mkuu hapo umefika mbali sana ndugu yangu, kama ni mpambano wa masumbwi naweza sema it's just below the belt.

Anyway, ukubwa jaa, mkono usoweza ukata ubusu

alamsiki.
 
Pundit, swali lako ni zuri na nitakupa majibu sahihi baadae kidogo maana kuna shughuli inabidi niimalizie kwanza na pia unataka scientific reasons mzee kama unautaka ukweli tu hapa ndio umefika.

It is very true many nutrients ambazo hazina ubora zinaishia kukojolewa hili halina ubishi na sababu inayochangia hilo ni kampuni husika kutowekeza kiasi cha fedha za kutosha kwenye R&D ya products zake. And this has every thing to do with the reasons why the company was established in the first place.

Unapokuwa katika biashara kwa muda mrefu maana yake una pata results, results katika biashara ni profits, profit inatokana na ku solve needs za target market yako! My point was you can not be in business for over 50 years without meeting the needs of your consumers! The basic of any business is to make peoples' lives better, if there is no improvement in their lives they wont buy from you! ( in marketing we call it repeat purchase or sustainable/ competitive advantage) It is as simple as that broo.

Mimi binafsi nilifahamu kuhusu supplements kwa kuwa nilikuwa na tatizo la fatigue, distributor wa gnld akaniambia moja ya sababu ni kuwa cell membrane zangu zimekuwa hard and impermiable, meaning food nutrients cannot get in, and waste matter cannot get out. Hivyo nakosa lipids and sterols, ambazo kazi yake ni kulainisha cell membrane ili ziweze kuruhusu vyakula na uchafu utoke. Akaniuzia TRE EN EN, nikatumia tatizo la uchovu likaisha. Sasa mkuu leo uniambie eti nilikojoa nutrients zote, wakati tatizo langu lime kuwa solved!? No way! Huo ndio ulikuwa mwanzo wangu wakuzichunguza na kuzitumia zote.

Sina cha kuficha mimi mi mgavi na nimedhamiria kuwaelimisha watanzania kupata elimu juu ya afya zao kupitia gnld. It is not what you eat (food) that is important rather it is what gets into your cells(nutrients).

Kuhani Mkuu
siweze ku comment chochote kuhusu post yako maana uwezo wako wa kutafakari kabla ya kufanya conclusion umenitia mashaka. Yaani mtu mwenye busara hawezi kutoa conclusion kama hiyo eti Ssebo na Mchongoma ni wamoja!

Nimesema explanation nitakupa muda si mrefu
 
There is a documented concern that food supplements in the form of pills containing vitamins and minerals are not properly digested and absorbed by the body leading to most of the nutrients to be urinated.

Do your research before engaging in needless consumption.There is no true substitute for the real thing.
Pundit,

I agree with you there is no true substitute for a true thing! gnld food supplements are not substitutes, they are the real things! Just think wewe mahindi unakoboa unatupa kiini (lipids), gnld wanalima mahindi wanatoa hicho kiini wanaki pack katika form ya pill wanakwambia ukila hiyo pill unakuwa umepata lipids, JE WAMEFANYA SUBSTITUTION? Pill ni package tu, cha muhimu ni content ya hiyo pill kaka!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom