Food For Thought: What to Eat to Boost Your Memory Kuleni matunda ili kuongeza memory | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Food For Thought: What to Eat to Boost Your Memory Kuleni matunda ili kuongeza memory

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Mar 28, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]I know I’m not alone in often forgetting names of close friends, or recalling the name of the book that I recently read, or heck, that I’mcurrently reading. Occasional memory lapses are a normal part of aging and the decline of estrogen that puts us into menopause in our 40s and 50s contributes to the “brain fog” that’s typical for women during this chapter of our lives.

  But, like most boomer-aged women, I worry that these occasional memory lapses could worsen down the road. Is there something that we can do, or take, to improve our chances of avoiding age-related memory deficits?
  In his book, “The Most Effective Ways to Live Longer,” nutritionist Jonny Bowden PhD makes his case for the need to consume more antioxidants in our daily diets. Antioxidants are

  vitamins and minerals that protect and repair cells from damage caused by free radicals.
  Specifically, he recommends an eating strategy that involves consuming foods that have been tested for antioxidant power and found to be outstanding performers. Fortunately, the government has compiled a database of foods that fall into this category. It’s called the ORAC Scale.

  What is the ORAC Scale?


  ORAC stands for Oxygen Radical Absorbance Capacity and The ORAC scale is a standardized test used by the USDA to measure the Total Antioxidant Potency of foods and nutritional supplements. Thus, this test reveals a food’s true age-fighting potential. Jonny Bowden

  calls them “superstar foods.”
  The top rated ORAC fruits are prunes, raisins, blueberries and strawberries; and the top rated ORAC Vegetables are Kale, Spinach, Yellow Squash and Brussel Sprouts. Spices such as Marjoram, Oregano, and Peppermint are winners too and should be used in your cooking as often as possible, according to Bowden.

  A Prescription for Blueberries


  Bowden writes that ORAC foods have a particularly powerful effect on the brain, and recommends eating one cup of blueberries three times a week for a memory boost. Personally, I eat half a cup daily for an extra boost.“Blueberries are the ultimate memory food,” he writes. “They’re loaded with compounds that fight both oxidation and inflammation.”He offered three other nutrition-related recommendations for boosting brain power:

  Eat cold-water fish at least twice a week.


  Cold-water fish such as salmon contains Omega 3s, which are particularly important for cognitive function.

  Follow the Mediterranean Diet.


  This way of eating emphasizes the consumption of vegetables, fruits, legumes, fish and olive oil.

  Add Turmeric to Your Food.


  If you love curry, this won’t be hard for you. Its active ingredient, curcumin, has been found to reduce oxidative damage and prevent inflammation in the brain. Bowden also suggested that we “shop so your grocery basket looks colorful. You’ll automatically be eating a ton of high-antioxidant (high-ORAC) foods.”

  Tujitahidi kula Matunda ili tuongeze kumbukumbu ya akili jamani nchi yetu ni tajiri sana kwa matunda tuleni kwa wingi na tuwape watoto zetu matunda kwa wingi asanteni.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Nikizungumza kwa tajiriba binafsi, matumizi ya bizari [au binzari kama wengine wanavyoita] yamepungua hususan kwa wakazi wa mijini. Sijui kama inatokana na ile fikra kuwa bizari inatumiwa na watu wa kipato cha chini ambao hawamiliki pesti ya nyanya au nyanya ya kopo ya kufanya mchuzi upate rangi, lakini si aghlabu sana kuona watu wakipikia bizari mijini kwa watu wenye kipato cha kati.

  Hii ni hasara kwetu kwa sababu kuna tafiti za kisayansi zinazoashiria kuwa sababu kuu ya wazee nchini India kutopatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ni kutokana na ulaji mwingi wa bizari

  *Kwa wale wasiopenda ladha yake, wanaweza kuila katika njia ya vidonge vinavyopatikana katika maduka ya tiba asili ya nchi za Asia, kama wazee wengi katika nchi za Asia wanavyofanya
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Vyakula vyengine ambavyo ni vizuri vinavyopatikana kwa wingi Tanzania ni pamoja na
  Nyanya
  Broccoli
  Karanga
  Mbegu za maboga
   
 4. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Na ulaji wa vyakula visivyo koborewa na hasa utumiaji wa ngano ,ulezi,mtama na nafaka zingine zisizo koborewa.

  Pia nanasi nalo huhusika sana na mambo ya kumbukumbu bila kusahau ASALI nayo ni mchawi mwingine.
   
 5. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Ok, na nliwahi kuskia lozi pia nzuri kwa kuongeza memory
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280


  mbegu za maboga............ kwetu tunaungia mboga, sijui zinakuwa na ubora ule ule?
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  hivi binzari mbichi inapatikana? naitafuta sana......si tu kuwa ni lishe bali ni dawa pia
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ubora wake haubadiliki hapo. Ningefurahi kama ungenifundisha namna zinavyotumiwa kuungia mboga. Recipe ya mboga moja please

  Inapatikana kwa wingi sokoni Kariakoo. Ukifika huwezi kuikosa. Au kama una nyumba yenye upenu unaweza kuotesha mwenyewe au hata kwenye pot tu
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Gee mbegu za maboga matumizi yake kwenye kuungia mboga ni kama karanga vile, zinakaushwa, zinatwangwa vizuri zilainike kisha unapika mboga yako kama ni majani ya maboga, mnafu, majani ya kunde, basi weye wauingia kama nazi vile...lol

  ...unaleta mambo ya recipe hapa mie najua wapi basi, nikwambie fungu la mchicha, pinch ya unga wa mbegu za maboga:hand:
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hehehe nataka useme kwa mchicha kicha kimoja, basi robo kikombe zitatosha
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  bht amejibu
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Gaijin bizari kwa kimombo inaitwaje?
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  curry powder, turmeric
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]
  curry powder, turmeric Bizari au manjano
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mbali ya faida hiyo; bizari inaweza kutumika katika kulainisha na kuleta mng'aro kwenye ngozi

  Matumizi

  Changanya unga wa bizara na maji kidogo, kutengeneza rojo zito. Pakaa rojo hilo usoni na wacha hivyo kwa kiasi cha dakika kumi, hadi ianze kukauka

  Osha kwa maji baridi.

  *Face pack hii inaweza kutumika kiasi cha mara mbili au tatu kwa wiki kwa ajili ya matokeo bora

  Tanabahi
  Kwa watu weupe pee, mchanganyiko huo, unaweza kusababisha ngozi yako kuonekana ya njano
   
Loading...