Fomu za viwanja mabwepande kutolewa leo lakini ni nutata mtupu

Yule

Member
May 4, 2012
14
5
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni leo inaanza kutoa fomu kwa ajili ya upimaji wa viwanja katika eneo la Mabwepande huku ikiwataka wananchi kujitokeza wauziwe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na manispaa hiyo kupitia kitengo chake cha mawasiliano, jumla ya viwanja 247 vinatarajiwa kupimwa kwa awamu ya kwanza, lakini leo Halmashuri ya Manispaa ya Kinondoni ime toa fomu 700 kwa viwanja 247. Huu ni mwendelezo wa mpango wake wa kuvipima viwanja zaidi ya 10,000.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Fortunatus Fwema, alisema viwanja hivyo vitauzwa kwa mwananchi yeyote mwenye kuhitaji endapo atazingati taratibu za ununuzi wake.

Alisema fomu za viwanja hivyo zitauzwa kwa gharama ya Sh 20,000 na kwamba baada ya hapo taratibu zingine za upimaji zitafuata mara mchakato wa kuzipitia fomu hizo kukamilika.

Alisema mwananchi atauziwa kiwanja kulingana na matakwa yake huku umakini ukiwepo ili kuepuka wadanganyifu wanaoweza kuharibu utaratibu mzima wa mchakato huo.

Fwema alisema lengo la kupima viwanja hivyo, ni kupunguza msongamano wa watu katika maeneo ya mjini huku akisisitiza kuwa eneo hilo litajengwa katika mpangilio maalumu utakaoufanya mji kuvutia.

“Hatutaacha pia kupima maeneo mbalimbali kwa ajili ya huduma za jamii katika eneo hili jipya tutahakikisha tunatenga eneo kwa ajili ya hospitali, shule, masoko ili kumfanya mwananchi kutokwenda mbali kwa ajili ya kutafuta huduma,” alisema Fwema.

Upimaji wa eneo la Mabwepande, ni mwendelezo wa manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam kuwa katika mchakato wa kupima viwanja zaidi ya 20,000 kwa lengo la kuwawezesha wananchi wake kuwa na makazi bora.

Lakini Mkurugenzi amewshindwa kuwaeleza wananchi kama mtu hakikosa katika awamu hii, maombi yake yale yale yatatumika nkatika awamu ya pili. Hii maana yake ni kama wakitangaza tena itakubidi ununue tena fomu.
 
Tuliokosa kule gereza ulole kigamboni basi watupe huko mwabepande,,!wanaopataga hiv viwanja sijui niwatu wa aina gani ufisadi mtupuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom