Foleni ya Tabata - Tazara imeanza kuwa tishio kwa uchumi wa nchi, nini kifanyike?

Napendekeza wajenge flyover juu ya Tazara flyover ili zinazotokea Buguruni kwenda bandarini nazo zipite juu. Nakaribisha maoni
Foleni kubwa ni sababu ya malori, sasa hivi wangekuwa wanapeleka mizigo ya mikoani kwa train kwenye dry port chalinze
 
Wew geography of jiji la hulijui vizuri fikria idadi kubwa ya watu dar 2050,hakuna unataka niseme wavunje majengo kupanua barabari njia 8. Hata malaika angeshuka hawezi solve tatizo. Nje ya kupunguza gari ndogo na kuleta gari ndogo. Ndio maana JPM Amepunza foreni dar kuhamia dodoma(amepunguza magari)
 
Njia ya kumpuza gari sio tu kodi .nikuhamisha huduma,dar kwenda mikoa mingine,kuongeza bandari tanga,mtwara, kuongeza viwanja ndege nje ya dar, mikoa mingine,kujenga mikoa mingine, treni za umeme, magari zitapungua kuja
 
Njia rahisi ya kupunguza foleni kwenye majiji, ingawa itaumiza wengine, ni kuwepo na kodi au tozo ya kila mwezi kwa magari yote binafsi yasiotoa huduma kwa umma, pamoja na kuongeza tozo maeneo ya kupaki hayo magari; Mfano, kama utatumia usafiri binafsi ndani ya jiji na ukawa unatozwa shilingi milioni 1 kwa mwezi, na sehemu yoyote utakayopaki au kusimama kutozwa kodi...hapo lazima magari mengi binafsi yatabaki majumbani, na hapo utakuwa umepunguza foleni kwa asilimia kubwa...kwa sababu kwenda katika shughuli zetu tutatumia usafiri wa umma.
🚮🚮🚮
 
Pesa ya kufanyia maendeleo watu wanataka wakanunulie chanjo ya majaribio,si uwendawazimu huu?
 
Njia rahisi ya kupunguza foleni kwenye majiji, ingawa itaumiza wengine, ni kuwepo na kodi au tozo ya kila mwezi kwa magari yote binafsi yasiotoa huduma kwa umma, pamoja na kuongeza tozo maeneo ya kupaki hayo magari; Mfano, kama utatumia usafiri binafsi ndani ya jiji na ukawa unatozwa shilingi milioni 1 kwa mwezi, na sehemu yoyote utakayopaki au kusimama kutozwa kodi...hapo lazima magari mengi binafsi yatabaki majumbani, na hapo utakuwa umepunguza foleni kwa asilimia kubwa...kwa sababu kwenda katika shughuli zetu tutatumia usafiri wa umma.
Duh
 
tunajenga haya mastructure bila kufanya research ya kutosha, jiji linahitaji nini kwanza...

Jiji la Dar es salaam linahitaji mipango miji anayoendana na population iliyopo + ukuaji wa mji...Ni wakati wa kupiga marufuku ujenzi majumba wa watu binafsi baadala yake miji ijengwe na agencies maalum au serikali watu wakopeshwe nyumba...

Baadhi ya huduma zitolewe katikati ya mji zipelekwe nje kama kibaha au bagamoyo....mfano Soko la Kariakoo linaweza kumegwa likaenda Mlandizi au Vigwaza huko...Biashara ya used pale Ilala na gerezani inapaswa kutoka iende mbali huko hata Msata... Soko la samaki feri linaweza kutolewa likaenda Bagamoyo...Kufanyike mgawanyo wa mahospitali makubwa baadhi yatoke katikati ya mji yahamie nje hata Chanika au kisarawe huko.... Serikali ifikirie kujenga miji ya kisasa kigamboni huko kuelekea Mbutu, Miji mingine ijengwe bunju, madale, Goba, Bagamoyo, Chalinze, Msata nk.. Kile chuo cha Ifm na vyuo vingine vitoke katikati ya mji viende hata msata huko... jijengwe express way kutoka mjini kati kuelekea Msata kupitia chalinze mpaka Morogoro na nyingine zipite Bagamoyo to msata...
 
Njia rahisi ya kupunguza foleni kwenye majiji, ingawa itaumiza wengine, ni kuwepo na kodi au tozo ya kila mwezi kwa magari yote binafsi yasiotoa huduma kwa umma, pamoja na kuongeza tozo maeneo ya kupaki hayo magari; Mfano, kama utatumia usafiri binafsi ndani ya jiji na ukawa unatozwa shilingi milioni 1 kwa mwezi, na sehemu yoyote utakayopaki au kusimama kutozwa kodi...hapo lazima magari mengi binafsi yatabaki majumbani, na hapo utakuwa umepunguza foleni kwa asilimia kubwa...kwa sababu kwenda katika shughuli zetu tutatumia usafiri wa umma.
Hizo nchi zilizoendelea na wao wanatumia mbini hii?
 
Back
Top Bottom