Foleni ya Magari ya barabara ya Nyerere kuelekea Uwanja wa ndege inavyolitia aibu taifa

Mar 10, 2020
24
150
Wana jamvi,

Kwa kweli katika jambo ambalo linashangaza ni namna ambavyo kuanzia mida ya saa kumi na moja jioni kutoka maeneo ya posta kuelekea airport foleni ilivyo kubwa.

Yani kwa mgeni/mtalii au mtanzania anaesafiri kwa usafiri wa anga alafu ndege yake iwe inaondoka saa tatu usiku ni lazima aondoke posta saa nane mchana au saa tisa mchana.akijichanganya akiondoka hotelini posta saa 10 jioni imekula kwake labda apande boda boda.

kuna foleni ya aibu mpaka juu ya flyover unakuta magari yamepangana mwanzo mpaka mwisho.

Kipande cha kilomita 10 unaendesha masaa mawili.Hii ni aibu kwa taifa kwa njia muhimu na ya kimkakati kama ya kwenda kiwanja kikubwa cha ndege kama JKNIA.

Serekali imejitahidi kujenga flyover tazara lakini ni wazi kua imezidiwa mno.
Nashauri yafuatayo ili kuondokana na aibu hii kwa taifa

1.Ile barabara inayotumika na wajenzi wa reli ya standard gauge....isiwe tena temporary road kwa wajenzi....iwekwe lami na iwe barabara rasmi ambapo watu wanaotoka posta na ubungo wanoelekea ukonga na gongo la mboto watapita njia hiyo na hawatalizimika kupita nyerere road.
 
Mkuu, upande huo mkilalamika, na wale wanaotokea temeke huko watasemaje??!! Kifupi hilo daraja limesaidia kupunguza foleni kwa kiasi kidogo sana, tofauti na tulivyoaminishwa kipindi linajengwa!!!! Mala mia mnaokwenda/kutoka airport
 
Urban planning tumefeli tangu enzi za Nyerere 80 percent ya miji yetu ni squatter
 
Ujenzi wa daraja sio mbaya ni moja ya hatua, ila kinachoonekana ni kama kurahishisha gari zipite kwa kipande kile tuu halafu zinaenda kukwama mbele, mfano

Mandela road: Junction kubwa za Buguruni na Tabata pia zingefikiriwa ( hii ya Serengeti,sio sana)
,ile ya Ubungo tayari ujenzi unaendelea.

Nyerere road: Junction kubwa ya Keko Mataa nayo ingefikiriwa

Maana kwa sasa kama unatokea temeke kwenda ubungo unaona kuwa unaweza kupita Mfugale kwa urahisi halafu unaenda kula block Buguruni

Kama unatoka Gombz kwenda mjini unaweza pota vizuri mfugale halafu ukala block Keko,

Na hizi block zinavyokuwa kubwa kuzidi hasa hasa asubuhi na jioni basi zinafanya folen mpaka eneo la darajani.

Alexander The Great
 
Urban planning tumefeli tangu enzi za Nyerere 80 percent ya miji yetu ni squatter
By 2100 (80 yrs from now), Dar-es-Salaam is expected to be among the world's three most populated cities along with Kinshasa and Bamako with over 70 million people. Wahusika wamelala tu wakisubuiria zimamoto muda utakapofika. Hawajui mipango ya 50 yrs ni leo.
 
Wenzio hiyo foleni tushaizoea ukichelewa kupita hapo utajua mwenyewe nyumbani utafika saa ngapi hata hiyo barabara ya reli ya standard gauge ikiwekwa lami bado foleni ipo palepale tu nchi karibia zote duniani zinafoleni we zoea tu.
 
Maisha ya dar ni sheeda....Rush hour imepita hadi za miji mikubwa duniani... Kuna kipindi niliishi mbagala halafu mara nyingi nilihitaji kwenda kariakoo.... Nilikuwa nikivuka kwa azizially au sometimes mtongani shida zinaanza...kufika kariakoo nishachoka tayari... Kurudi jioni sasa hapo sitii neno...ukitumia usafir binafsi shida zilezile.... Japo boda naziogopa ila kuna muda ilinilazimu kuzitumia.... Kaeni na dar yenu tu Aiseeh.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom