Foleni Ubungo ni Janja ya Traffic na Bodaboda, wapokea 20 kwa siku

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,753
7,075
ile foleni kubwa inayotokea nyakati za asubuhi , kumbe dili kati ya matrafiki na waendesha piki piki a.k.a. bodaboda, nikiwa nimebebwa nilijaribu kudadisi nikapata ukweli wake. Dili liko hivi, bodaboda uchanga elfu moja mpaka mbili , umpelekea traffic aliye zamu, hapo ndipo kimbembe kinapoanza, ataruhusu upande mmoja kwa muda mwingi ili wale wote waliochelewa makazini washuke wapande piki piki, pikipiki moja upanda kuanzaia elefu saba hadi kumi, inafuatana mapatano kati ya yeye na abiria. Hivyo ndio umekuwa mchezo wao wa kila siku. Hivyo chunguzeni nanyi mtujulishe
 
nilisikia hata mimi, hata namimi huwa nashangaa! inakuwaje magari ya kutoka town kwenda mbezi, kimara au toka riverside yanagandishwa kama dk 30 hadi 45 na akiruhusu ni magari kama kumi na tano then anazui! mhh mjini hum kila na mtu na ujuzi wake ndo mkono unaenda kinywani! silaumu mtu ila mfumo wa viongozi wetu!ama kweli timbwili likianza hapa mjini hadi panya watatoka shimoni!
 
Hii ni bola waambiwe TAKUKURU maana Issue nyingine hizi ni michosho tu, ........ Ila kumbukeni kila mtu analia Ofsini kwake, ilo hata mkuu wa kaya analijua aiseee!!
 
Kwani foleni ilianza bodaboda zilipoanza tu biashara? Kabla ya bodaboda hakukua na foleni ubungo? Kwa upande wangu napata shida kuamini hili suala kidogo. Kwa hiyo foleni ya pale njia panda ya kinondoni pale stanbic napo ni dili la matrafic na bodaboda (manake pale sioni bodaboda)?
 
Kwani foleni ilianza bodaboda zilipoanza tu biashara? Kabla ya bodaboda hakukua na foleni ubungo? Kwa upande wangu napata shida kuamini hili suala kidogo. Kwa hiyo foleni ya pale njia panda ya kinondoni pale stanbic napo ni dili la matrafic na bodaboda (manake pale sioni bodaboda)?
Sio suala la kipi kilianza, ni suala la ku-take advantage ya kazi yao pamoja na hali halisi iliyopo kwa wakati uliopo sasa!
 
ugumu wa maisha hufanya watu kuwa wabunifu ktk kazi za6 ili kujiongezea kipato, huu sio wizi
 
sometimes ubunifu unatakiwa.....hata ningekuwa mie ngefanya hivyohivyo,bigup bodaboda
 
naona tangia wasome hii thread sijui wameambiwa maana wamejirekebisha, au ule nchango wa aliyetaka takukuru iwafuatilie?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom