Foleni Ubungo - Mbezi - Kibamba ilivyo kero.

Hili limeshakuwa tatizo la kudumu kila siku.

Imeshawahi tokea saa 10 alfajiri nimekutana na hii foleni.

Jana nimetoka kibaha nikakuta foleni imeshafika kimbamba njia panda ya shule, ikabidi nipite service road mpya nilivyopita pale kibamba darajani.

Nimekuja nayo mpaka mbezi mwisho round about.

Kumbe tatizo ni lile daraja pale mbezi. Limekuwa dogo kiasi cha kutoweza mudu magari mengi kwa wakati mmoja.

Limeshakuwa tatizo sugu sasa.

Leo nimepita tena hiyo njia, foleni toka mbezi mpaka ubungo tena.

Hata kama serikali imesitisha ujenzi wa hii barabara, ihakikishe madaraja yote yamewekwa sawa.
Unalosema nikweli aisee unaweza juta kwanini ulijenga kibamba,na sijawahi sikia hata siku moja waziri akiwakemea wakadarasi kuboresha njia za mchepuko wakati ni jukumu lao. Hata RC wetu hajawahi zungumzia hii kero. Leo nimeacha gari kimara nimechukuwa boda boda mpaka kibamba na ndio nafika saizi. Mungu tunusuru na hii adha, nawahurumia sana ndugu zetu wanao funga mwezi mtukufu na zile gari za wagonjwa ni taabu tupu.
 
Yani kama umepanga kimara- mbezi bora kuhama tu.
Inategemea, wapo wapangaji huko, wana familia, watoto wameandikishwa shule za maeneo ya huko, unahama kwa jambo la muda tu. Ila kwa Single sio shida sana. Hata hivyo mpangaji mwingine hapendi kuhama hama kama anapokaa pana amani, mpaka ahamie kwake.
 
Ujenzi Wa Hii Barabara Ya Kimara - Kibaha HAUJASITISHWA

WAMESITISHA Ujenzi Wa Dar - Chalinze Ambayo Design Yake Ilikuwa Express Highway!!

NAOMBA WENYE VICHWA VIGUMU KUELEWA MUELEWE

Narudia Tena, Cyo Kimara- Kibaha, Ni Express Highway Ya Dar - Chalinze!!

Nimeeleza Vizur Hpa Ila Watakuja "Failure " au wale Walioshia "Diploma" Kuanza Kuhoji Upuuzi

MTAONA
kumbe aisee
 
Back
Top Bottom