keizerjohn
Senior Member
- May 12, 2013
- 113
- 13
Wadau, hivi mbona foleni ya Morogoro Road haitafutiwi ufumbuzi wa haraka. Kweli mpaka barabara ikamilike miaka miwili ijayo, tutakuwa katika hali gani? Kutoka mbei hadi Stand ya Mkoa mtu unatumia zaidi ya masaa manne wakati ni km 13 tu.
Huu ni ujenzi gani wa kutojali watumia barabara? TANROADS mpo wapi? Serikali nayo ipo wapi? Viongozi wetu mpo wapi, hata wapinzani na nyinyi mpo wapi?
Licha ya watu wote kuathirika, wagonjwa, wanafunzi, wakina maama wana hali mbaya zaidi! Haya ni maendeleo au ni kurudishana nyuma?
Kama Serikali ipo kimya, basi vyama vya hiari vihamasishe maandamano ili tuishurutishe Serikali ije na mbinu mbadala ya haraka ya kupunguza foleni hii wakato ujenzi unaendelea.
Haiingii akilini Kampuni inabomoa kila mahala halafu haitengenezi, inaziba ziba kila mpenyo na kutuacha tunahangaika.
Wadau tujadili hili tufanyaje?