Foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela road kuanzia Tabata hadi Buguruni

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,626
Foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela Road kuanzia Tabata hadi Buguruni.

Wakuu foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela Road.

Sasa hivi hayo maeneo yana foleni muda wote unakuta foleni inakaa mpaka masaa 2.

Kwa kweli tunahitaji kuwaza sana jinsi ya kutokomeza hizo foleni.
 
Wanatakiwa wa re-set traffic lights za pale Buguruni na Tazara kuelekea bandarini na vice versa kwa kuziongezea muda zaidi.
Kumbuka hiyo ni bottle neck effect na lilitarajiwa, ilikuwa ni suala muda tu.

Barabara mbadala za kutosha zingesaidia kutatua tatizo hilo ambazo kwa sasa hivi hazipo.
 
Foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela Road kuanzia Tabata hadi Buguruni.

Wakuu foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela Road.

Sasa hivi hayo maeneo yana foleni muda wote unakuta foleni inakaa mpaka masaa 2.

Kwa kweli tunahitaji kuwaza sana jinsi ya kutokomeza hizo foleni.
Solution ni barabara za juu au uhame dar. Interchange kazi yake ni kuhamisha jam ya magari eneo Moja na kupeleka jam kwingine.
 
Wataalamu walishasema interchange haiwezi kutatua changamoto za foleni bali inaondoa msongamano kwenye makutano ya barabara ilipowekwa tu.

Interchange ya Ubungo itaondoa msongamano pale Ubungo mataa tu lakini inaongeza msongamano makutano ya barabara ya Shekilango kuja mjini, Buguruni kuja Tazara na Survey kuelekea Mwenge.

Foleni kwa jiji Dar itazidi kuongezeka na kuzidi kuongezeka. Kwanini? Watu wanazidi kuongezeka, Magari mapya mengi yanayoingizwa Tanzania (inakadiriwa kuwa kuna magari mapya karibu 200 yanaingizwa barabarani kwa matumizi binafsi hapa Dar kutokea bandarini kila siku)
 
Foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela Road kuanzia Tabata hadi Buguruni.

Wakuu foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela Road.

Sasa hivi hayo maeneo yana foleni muda wote unakuta foleni inakaa mpaka masaa 2.

Kwa kweli tunahitaji kuwaza sana jinsi ya kutokomeza hizo foleni.
Serikali hii haijui kutatua matatizo bila kusababisha matatizo mengine makubwa zaidi.
 
Foleni ya kuelekea Buguruni ilikuwepo siku zote, ndio maana wengi tulishangaa walipojenga daraja la level moja badala ya madaraja ya level mbili pale Tazara
 
Foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela Road kuanzia Tabata hadi Buguruni.

Wakuu foleni iliyokuwepo Ubungo sasa imehamia Mandela Road.

Sasa hivi hayo maeneo yana foleni muda wote unakuta foleni inakaa mpaka masaa 2.

Kwa kweli tunahitaji kuwaza sana jinsi ya kutokomeza hizo foleni.
Tatizo ni kwamba huwa hatuwazi zaidi ya kimo cha macho yetu
 
Unashangaa hayo ya barabara wakati kuna mhandisi anashauri kila siku mito ya mjini ipanuliwe kila uchwao badala ya kuichimba ikawa na kina ikibidi ijengwe isizidi kutanuka!
 
Solution ni barabara za juu au uhame dar. Interchange kazi yake ni kuhamisha jam ya magari eneo Moja na kupeleka jam kwingine.
Unapanua mtaro wa maji pale yanapoanzia lakini yanapoelekea panabaki padogo. Kama hayatavuka kingo zake, basi yatajaa hadi kule yanakotokea, Usishangae hiyo foleni ya Tabata Buguruni ukakuta imefika hadi ubungo!
 
Tabata relini pale pamekua Jipu,
Mimi hua nashuka.
Hivi ukishuka halafu ukafika mbela ukitaka kupanda tena inakuaje?
 
Back
Top Bottom