Foldable smart phones: Simu janja zenye uwezo wa kukunjika kirahisi

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Dunia inakwenda kwa kasi sana! Teknolojia ya mawasiliano nayo inazidi kubadilika kila kukicha. Miaka kadhaa iliyopita, hakukuwa na simu janja! Smart phones.

Wajanja wote walikuwa wanatumia simu za ‘buttons’, na ili uonekane mjanja zaidi, unaivaa kiunoni! Mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano yakaja kutokea baada ya kugunduliwa kwa ‘smartphones’, simu za ‘buttons’ zikashuka thamani na sasa ni kama zinaenda kabisa kutoweka, kila kitu ni ‘ku-touch’ tu.

Hivi sasa watu hawashindani kumiliki ‘smartphones’ pekee, bali mjanja ni yule anayemiliki ‘smartphone’ kali zaidi, yenye vitu vingi na inayouzwa bei kubwa kuliko nyingine.

Sasa wakati hayo yakiendelea, wanasayansi wanaendelea kuumiza vichwa na habari ya mjini kwa sasa, ni foldable martphones, yaani smartphones zenye uwezo wa kujikunja!

5.jpg

Galaxy Fold ndiyo simu ya kwanza kuingia sokoni ikiwa na teknolojia hii! Kwa kuitazama, inakuwa haina tofauti na smartphones za kawaida, ina mwonekano wa kwanza ambao ni kama simu za kawaida.

Lakini mwonekano wa pili, ni kwamba unaweza kuifungua simu hii kama kitabu, ule upande wa nyuma nao ukafunguka na kuwa kioo kingine, kwa hiyo unakuwa na simu moja ambayo ina vioo viwili vya ukubwa uleule ambavyo vinaweza kuungana na kuwa kioo kimoja kikubwa zaidi, mara mbili ya vioo vya kawaida vya smartphone.

Wakati Samsung wakiwa wameshaingiza Galaxy Fold sokoni kwa majaribio, kampuni nyingine za Huawei na Motorola nazo zinakimbizana kuhakikisha zinaingia sokoni ifikapo 2020, Motorola wakiwa na toleo lao liitwalo Razr huku Huawei wao wakiwa na toleo liitwalo Huawei Mate X.

Tetesi ni kwamba Apple nao wapo mbioni kuingiza Foldable iPhone sokoni! Kwa kifupi mtafutano ni mkubwa sana kwenye makampuni haya makubwa ya simu duniani.

33.jpeg

Malengo ya kampuni hizi ni kwamba simu hizo tayari zingeshakuwa zimeingia sokoni lakini changamoto kubwa ambayo inawasumbua vichwa kwa sasa, ni tatizo la kioo kuchoka haraka na kuanza kupasuka kutokana na kukunjwa mara kwa mara pamoja na betri kuwahi kuisha kutokana na ukubwa wa ‘screen’ unapoikunjua simu.

Kwa wale wapenzi wa kutazama muvi kwenye simu au kutazama muziki Youtube, simu hizi zitawafaa zaidi kwa sababu ‘screen’ yake ikikunjuliwa inakuwa na ubora wa hali ya juu wa kuweza kuonesha picha na video kwa kiwango cha High Definition (HD).

Uhitaji umekuwa mkubwa lakini kampuni hizo zinasita kuachia simuhiyo kuingia sokoni mpaka kwanza zirekebishe mapungufu yaliyopo.

Hivi karibuni, bosi wa Samsung, DJ Koh alinukuliwa akisema kwamba uzinduzi wa Galaxy Fold unawasumbua sana kichwa chao na wanahisi wamewahi kuingia sokoni kwa majaribio kimakosa kutokana na dosari zilizobainishwa.

1.jpg

Gharama ya simu moja ikiwa ni wastani wa dola 1980, sawa na takribani shilingi milioni 4.5 za Kibongo na ukiachilia mbali dosari za kioo kupasuka na kuwahi kuisha chaji, tatizo lingine limetajwa kuwa ni uchafu kuingia kwneye eneo kioo kinapojikunja na kusababisha simu ishindwe kurudi kwenye muundo wake wa awali pale inapokunjuliwa.

Uimara wake ni kwamba kwamba kioo kikifunguliwa, kinafikia ukubwa wa nchi 7.3, huna haja ya kufungua upya kile ulichokuwa umekifungua kwenye ‘screen’ moja kwa sababu kitajirekebisha chenyewe kwenda kwenye kioo kikubwa na unaweza kutumia apps hadi tatu kwa mpigo kwenye ‘screen’ iliyokunjuliwa.

Ni suala la muda tu lakini tayari ‘foldable smart phones’ zipo njiani! Ama kwa hakika yajayo yanasisimua.

Hash Power!
 
View attachment 1283426

View attachment 1283425

View attachment 1283429

Nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu uimara wa kioo hicho kumbe nilikuwa sawa.
 
Yaani ni toe million 4.point kununua simu inanini zaidi hiyo simu upuuzi tu kwanza simu za haina hii hata sizikubali yatima wanakufa kwa njaa mi nitoe million NNE kununua hiyo taka taka kwa muundo huu acha tuzidi kuonekana washamba tumsubirie tecno aje atoe take ya laki mbili tununue
 
Ndugu yake na Pablo Escobar
Roberto Escobar ametoa Escobar Fold 1 unbreakable gold smartphone na anavyosema kuwa ni bei rahisi na haivunjiki kama hizo zingine kwani imetengenezwa kwa plastic ngumu na bei yake $349 tu
Hatua y pili ni kuwashtaki Apple hapo ndio patamu
IMG_1591.jpg
IMG_1592.jpg
 
Kila wanachotengeneza, kina wateja wake, kuna watu hiyo hela haiwafukilishi, Na ndiyo wateja wao.

Wewe na mimi tumenunua simu ya bei mbaya ni 700,000 hata kwenye magari, wewe na mimi size yetu ni gari ya ml 20 kushuka chini.

Ila wapo watu Tanzania hii hii wanatembelea magari ya ml 100 na zaidi.
Yaani ni toe million 4.point kununua simu inanini zaidi hiyo simu upuuzi tu kwanza simu za haina hii hata sizikubali yatima wanakufa kwa njaa mi nitoe million NNE kununua hiyo taka taka kwa muundo huu acha tuzidi kuonekana washamba tumsubirie tecno aje atoe take ya laki mbili tununue
 
Kila wanachotengeneza, kina wateja wake, kuna watu hiyo hela haiwafukilishi, Na ndiyo wateja wao.

Wewe na mimi tumenunua simu ya bei mbaya ni 700,000 hata kwenye magari, wewe na mimi size yetu ni gari ya ml 20 kushuka chini.

Ila wapo watu Tanzania hii hii wanatembelea magari ya ml 100 na zaidi.
Umenena vyema mkuu! Ni sahihi kabisa, mkono unajikuna pale unapofikia, wengine mikono yao mirefu
 
Hawa jamaa walileta ESCOBAR FOLD 1 NA 2 ni wahuni sana. Kumbe wamechukua SAMSUNG GALAXY FOLD wakaweka sticker ya GOLD na yenye jina la ESCOBAR FOLD na jina la kampuni yao.

1591196729818.png

1591196764362.png

1591196833330.png

Marques amereview hapa.

Back
Top Bottom