Focus Saanane: Ninamtaka Mwanangu Ben akiwa hai, amlaumu Mbowe

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
image.jpg

BABA WA BEN SAANANE AFUNGUKA

UPENDO MOSHA NA SAFINA SARWATT – MOSHI

SAKATA la kupotea ghafla kwa aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bernard Saanane, limechukua sura mpya, baada ya familia yake kumjia juu mwajiri wake, Chadema, kwa kile inachodai chama hicho kimeshindwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kumtafuta.

Akizungumza na MTANZANIA jana, baba mzazi wa Saanane, Focus Saanane, alisema anashangazwa na hatua ya Chadema kushindwa kujitokeza hadharani kumtafuta mwanae ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

“Tangu mwanangu Ben amepotea, hatujawahi kumuona (Freeman) Mbowe ambaye ndiye mwajiri wake kama amechukua hatua yoyote ya kukutana na familia yangu, tukashauriana namna ya kumtafuta. Ukimya huu umenistajabisha mno.

“Nilitegemea angekuwa mtu wa kwanza kuja kwangu, tuone njia gani ambayo tunaweza kutumia kumpata Ben. Naumia mno ndugu yangu,” alisema Focus.

Alimtaka Mbowe ajitokeze na kuipa familia taarifa za mahali alipo Ben, kwani wao wametawaliwa na hofu kubwa kutokana na kijana wao kutoweka akiwa mikononi mwake.

“Ninamtaka Mbowe aniletee mwanangu Ben akiwa mzima, nashindwa kujua yupo wapi na nini kinaendelea mpaka sasa kati yake na Ben, haiwezekani mwajiri ashindwe kujua mfanyakazi wake alipo mpaka sasa… bado haliniingii akilini mwangu… suala hili halileti taswira nzuri kwa jamii kama anaendelea kukaa kimya na hazungumzi chochote, si haki,” alisema.

Akizungumza kwa jazba, Focus aliiomba Serikali na vyombo vyake vya dola isaidie kumtafuta Ben kwa nguvu zote kutokana na juhudi za familia kugonga mwamba.

Pia alikanusha vikali taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, kuwa Ben amefariki dunia. Kwamba familia yake imeitwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwenda kutambua maiti moja iliyochomwa moto maeneo ya Uru Ongoma. Kata ya Uru Kaskazini wilayani Moshi.

CHADEMA

Akijibu malalamiko hayo, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene, alisema si kweli kama Mbowe ameamua kukaa kimya, bali wao wameiachia Serikali kufanya uchunguzi wa kina na kutoa taarifa.

“Wakati jambo hili linatokea, mwenyekiti wetu (Mbowe) alikuwa nje ya nchi, naelewa presha aliyonayo mzazi wa Ben katika suala hili, tunaendelea kuhangaika nalo na kutaka vyombo vya dola vichukue hatua.

“Tunaitaka Serikali ifanyie kazi mambo matatu ambayo yako ndani ya uwezo wake, iseme wapi alipo Ben, mara ya mwisho aliongea kwa simu yake na nani na wapi na itumie kila aina ya uwezo wa kumleta kwa sababu si mtuhumiwa,” alisema Makene.

RPC

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana, kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kuhusu mwili uliookotwa eneo la Uru Ogoma, si wa Ben kama ambavyo iliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

“Uchunguzi uliofanywa umebaini aliyefariki ni Steven Kimario (55), mkazi wa Sanya Juu wilayani Siha, ambaye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira, baada ya kukutwa akifanya jaribio la kubaka mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka tisa.
 
Sasa Kama unamuuliza Mbowe nyie mna polisi,usalama wa taifa na jeshi na nyie bado mnalalamika na kumlaumu Mbowe,Kama mmeweza kwa Lema mkamweka ndani Leo mwezi na ushee mnashindwa nini kumkamata Mbowe.kama mliweza kumtumia Hakim SMS na kubadili mawazo ya kumpa Lema dhamana mnashindwa nini kumkamata Mbowe
 
Kaka soma vizuri. Aliyesema hayo ni Focus saanane. Si mleta mada
 
Sasa Kama unamuuliza Mbowe nyie mna polisi,usalama wa taifa na jeshi na nyie bado mnalalamika na kumlaumu Mbowe,Kama mmeweza kwa Lema mkamweka ndani Leo mwezi na ushee mnashindwa nini kumkamata Mbowe.kama mliweza kumtumia Hakim SMS na kubadili mawazo ya kumpa Lema dhamana mnashindwa nini kumkamata Mbowe
Aiseeee naona unaropoka hovyo kabisa. Sijui kama unajua nini umeandika
 
Sasa Kama unamuuliza Mbowe nyie mna polisi,usalama wa taifa na jeshi na nyie bado mnalalamika na kumlaumu Mbowe,Kama mmeweza kwa Lema mkamweka ndani Leo mwezi na ushee mnashindwa nini kumkamata Mbowe.kama mliweza kumtumia Hakim SMS na kubadili mawazo ya kumpa Lema dhamana mnashindwa nini kumkamata Mbowe
Ongata usilie lie...Baba yake Ben ndiye anataka Mbowe awajibike.
 
Hawa watu ni tatizo ndani ya CHADEMA
1. MBOWE
2. LISSU
3. TUMAINI MAKENE
wanailaghai sana familia ya BEN, wanachama wa CHADEMA na Marafiki wa BEN kwa ujumla. Hivi vitaarifa vya kumlinda linda MBOWE vya Lissu na Makene ni hatari sana.
 
Hii mbinu ya chama chako haitafua dafu,hata kama mwajiri wake anahisiwa vyombo vya dola vibainishe.Baada ya kumpandikiza prof cuf,sasa mmekuja na hilo chadema
Lizaboni
 
“Tangu mwanangu Ben amepotea, hatujawahi kumuona (Freeman) Mbowe ambaye ndiye mwajiri wake kama amechukua hatua yoyote ya kukutana na familia yangu, tukashauriana namna ya kumtafuta. Ukimya huu umenistajabisha mno.

“Nilitegemea angekuwa mtu wa kwanza kuja kwangu, tuone njia gani ambayo tunaweza kutumia kumpata Ben. Naumia mno ndugu yangu,” alisema Focus.
Mhalifu afanye yake halafu aje mjadiliane? Ndugu Focus Bora umeamua kumshtaki kwa umma huyu 'mchawi' ajulikane.
 
CHADEMA ni Taasisi. Kilichosemwa na CHADEMA kupitia Taarifa yao ndicho kinachosemwa na wote ndani ya CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe kama Mwenyekiti wao. Hakuna mantiki yoyote ya kujenga propaganda za kumdai au kumhusisha Mbowe na masuala ya Ben Saanane kama mtu binafsi.

Msilete siasa na propaganda katika maisha ya watu. Ben Saanane asitumike kisiasa. Zifanyike juhudi za pamoja kumpata au kujua alipo na kilichomsibu. Familia ya Saanane isipokuwa makini itatumiwa sana kipropaganda katika kipindi hiki cha kumtafuta Ben. Mambo yameshaanza.
 
Kama mzazi najua anaumia sana kuona mwanaye ametoweka kwenye mazingira tatanishi hivyo...Ombi langu tu Mzee Focus asikubali kutumika na wanasiasa uchwara katika sakata hili la Ben...
 
Back
Top Bottom