Focus Saanane: Ninamtaka Mwanangu Ben akiwa hai, amlaumu Mbowe

Hili la Ben linashabihiana na la yeriko kipindi kile cha kampeni ingawa cha kwake hakikutangazwa kwa sababu kulikua na vuguvugu za kampeni tujipe mda bado siamini mawazo ya kuwa Ben kafa.
Ila hili la Ben Saanane hakika limetia fora
 
Hawa watu ni tatizo ndani ya CHADEMA
1. MBOWE
2. LISSU
3. TUMAINI MAKENE
wanailaghai sana familia ya BEN, wanachama wa CHADEMA na Marafiki wa BEN kwa ujumla. Hivi vitaarifa vya kumlinda linda MBOWE vya Lissu na Makene ni hatari sana.
Mtoto wa Chacha Wangwe kila nikimuangalia anavyo jipresent naamini ana akili mara 70 zaidi yako.
Sasa ukitaka kutuaminisha kuwa naye 'anashirikiana na waliomuua' baba yake, uwe tayari kubebe matokeo!
 
Msaidizi wako anapotea unakaa kimya? Inshangza sana!

Mnataka Mbowe aunde jeshil la polisi la chama chake kulinda na kuwatafuta waharifu wanaohujumu chama? Huu ni upumbaavu. Serikali inatakiw akutoa majibu ya kina juu ya hili no matter what. Acheni kujifanya punguani kama zinawatosha!
 
Hili la Ben linashabihiana na la yeriko kipindi kile cha kampeni ingawa cha kwake hakikutangazwa kwa sababu kulikua na vuguvugu za kampeni tujipe mda bado siamini mawazo ya kuwa Ben kafa.
Tena ni dhambi kubwa kukimbilia kusema BEN kafa. Muhimu wadau wa kumtafuta na kusaidia kupatikana kwa taarifa zake waongeze kasi ya kumtafuta. Na zaidi tuzidishe maombi.
 
Mtabaki hivyo hivyo na majungu yenu ya kipuuzi, wenzenu kila leo wanateuliwa mumekalia kuijadili Chadema tu.
 
Haya nilitegemea watu wa upande ule wameanza kumlisha mzee wa watu sumu.Haya kwanini yatokee baada ya Mwigulu na polisi kujitokeza jana?,Mbona siku zote huyu mzee alikuwa kimya?


Mzee kwa ushauri tu hakuna kipindi ambacho unatakiwa uwe na hekima na busara katika kipindi hiki kigumu kwako,Mzee angalia hao wanakuinfluence kwa sasa kuwa mbowe amlete mtoto wako akiwa hai,"kuwa makini mzee kuna kitu wanakijua hao hilo nia
 
Mzee kavunja ukimya lakini nakumbuka Lissu alisema Mbowe ndiye mtu wa mwisho kuwasiliana na Saanane.
Mbowe onesha mtoto wa mwenzio alipo.
 
Mara ya mwisho Ben Saanane aliwasiliana na Mbowe
Mawasiliano hayo una ushahidi nayo?Na je!?Yaliashiria jambo lolote baya juu ya Ben?
Maana mkuu Lizaboni mawasiliano tunayosema ni lazima yawe "evil oriented"
Kwa hiyo criminal sociology tu inakupasa uwe na uwianisho huo
 
Mwigulu ndiye amesema ni Rafiki yake hata kuliko sisi ndugu zake hivyo anatakiwa amtafute rafiki yake ........
Mbowe ndio boss wake anatakiwa ajue Ben yupo wapi kama baba Ben alivyosema....kama Mwigulu ndio rafiki yake basi marafiki Wa Ben wote wamtafute, kwa sababu Ben alikua hana rafiki mmoja tu
 
Mimi ni mgeni naomba ufafanuzi vh kwa mfano mwanangu ni mfanyakazi labda nimwalimu akipotea shule anayofundisha ndo inamta futa au polisi na je mimi kama mzazi wa huyo mwalimu mda ukiwa umeenda sana mwanangu bado hajapatikana nimlalamikie mwalimu wake mkuu au niombe ufafanuzi kutoka polisi kwa akili yangu ndogo polisi ndo wanaotakiwa wamtafute mwangu iwe yuko kwa mwalimu mkiu au kafa. Ila mimi siwezo kudilo na mwalimu mkuu poliso ndo watamuuloza mqalimi mkuu kuwa mwalimu wako yuko wapi. Kwa mfano huo jeshi la polisi lituambia limefikia wapi kujia ben alipo
 
Huu uzi una watu kadhaa Lizaboni Wakudadavuwa TataMadiba

Sasa imekuwa ajenda ya "kisiasa" badala ya uhai wa mtu na maumivu kwa wapendwa wake.
Hizi ni aina ya siasa za kikomunisti...zilitumika sana Ulaya Mashariki na Uchina.Kuingia ndani ya adui yako na kutengeneza mgogoro wa ndani kwa manufaa ya kwako na kubadili upepo.

Haya mambo mafunzo yake makada wengi waliyapatia Jiji la Sophia-Hungary,kumuelezea mtu inahitaji awe na ufahamu wa misingi ya chama cha kikomunisti,iwe ni cha Afrika au Ulaya Mashariki.

Dola inamiliki TCRA,pale kuna kitengo kinachoweza kujua mara ya mwisho Ben Saanane aliongea na nani na alikuwa wapi?

Polisi kitengo cha Cyber Crime wanaweza kuanzia hapo pia,ktk nchi yenye vyombo vyote vya dola vilivyo makini,japo la uhai wa mtu haliangaliwi kwa mitazamo ya chama.
Mkuu, mimi sitaki kuwa mnafiki kama ambavyo mzazi wa Ben Saanane ameamua kuweka unafiki pembeni na kuusema ukweli. wepesi wa kumtafuta Ben ungeonekana kwa MBOWE kuonesha nia na ushirikiano kama mtu ambaye alikuwa karibu sana na Ben kuliko hata mzee Focus mwenyewe. kuweka siasa kwenye hili ni kufuru hata kwa Mungu
 
Huu uzi una watu kadhaa Lizaboni Wakudadavuwa TataMadiba

Sasa imekuwa ajenda ya "kisiasa" badala ya uhai wa mtu na maumivu kwa wapendwa wake.
Hizi ni aina ya siasa za kikomunisti...zilitumika sana Ulaya Mashariki na Uchina.Kuingia ndani ya adui yako na kutengeneza mgogoro wa ndani kwa manufaa ya kwako na kubadili upepo.

Haya mambo mafunzo yake makada wengi waliyapatia Jiji la Sophia-Hungary,kumuelezea mtu inahitaji awe na ufahamu wa misingi ya chama cha kikomunisti,iwe ni cha Afrika au Ulaya Mashariki.

Dola inamiliki TCRA,pale kuna kitengo kinachoweza kujua mara ya mwisho Ben Saanane aliongea na nani na alikuwa wapi?

Polisi kitengo cha Cyber Crime wanaweza kuanzia hapo pia,ktk nchi yenye vyombo vyote vya dola vilivyo makini,japo la uhai wa mtu haliangaliwi kwa mitazamo ya chama.
soma vema, hiki ni kilio cha baba yake Ben.
SAKATA la kupotea ghafla kwa aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bernard Saanane, limechukua sura mpya, baada ya familia yake kumjia juu mwajiri wake, Chadema, kwa kile inachodai chama hicho kimeshindwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kumtafuta.

Akizungumza na MTANZANIA jana, baba mzazi wa Saanane, Focus Saanane, alisema anashangazwa na hatua ya Chadema kushindwa kujitokeza hadharani kumtafuta mwanae ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

“Tangu mwanangu Ben amepotea, hatujawahi kumuona (Freeman) Mbowe ambaye ndiye mwajiri wake kama amechukua hatua yoyote ya kukutana na familia yangu, tukashauriana namna ya kumtafuta. Ukimya huu umenistajabisha mno.

“Nilitegemea angekuwa mtu wa kwanza kuja kwangu, tuone njia gani ambayo tunaweza kutumia kumpata Ben. Naumia mno ndugu yangu,” alisema Focus.

Alimtaka Mbowe ajitokeze na kuipa familia taarifa za mahali alipo Ben, kwani wao wametawaliwa na hofu kubwa kutokana na kijana wao kutoweka akiwa mikononi mwake.

“Ninamtaka Mbowe aniletee mwanangu Ben akiwa mzima, nashindwa kujua yupo wapi na nini kinaendelea mpaka sasa kati yake na Ben, haiwezekani mwajiri ashindwe kujua mfanyakazi wake alipo mpaka sasa… bado haliniingii akilini mwangu… suala hili halileti taswira nzuri kwa jamii kama anaendelea kukaa kimya na hazungumzi chochote, si haki,” alisema.

Akizungumza kwa jazba, Focus aliiomba Serikali na vyombo vyake vya dola isaidie kumtafuta Ben kwa nguvu zote kutokana na juhudi za familia kugonga mwamba.

Pia alikanusha vikali taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, kuwa Ben amefariki dunia. Kwamba familia yake imeitwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwenda kutambua maiti moja iliyochomwa moto maeneo ya Uru Ongoma. Kata ya Uru Kaskazini wilayani Moshi.

CHADEMA

Akijibu malalamiko hayo, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene, alisema si kweli kama Mbowe ameamua kukaa kimya, bali wao wameiachia Serikali kufanya uchunguzi wa kina na kutoa taarifa.

“Wakati jambo hili linatokea, mwenyekiti wetu (Mbowe) alikuwa nje ya nchi, naelewa presha aliyonayo mzazi wa Ben katika suala hili, tunaendelea kuhangaika nalo na kutaka vyombo vya dola vichukue hatua.

“Tunaitaka Serikali ifanyie kazi mambo matatu ambayo yako ndani ya uwezo wake, iseme wapi alipo Ben, mara ya mwisho aliongea kwa simu yake na nani na wapi na itumie kila aina ya uwezo wa kumleta kwa sababu si mtuhumiwa,” alisema Makene.

RPC

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana, kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kuhusu mwili uliookotwa eneo la Uru Ogoma, si wa Ben kama ambavyo iliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

“Uchunguzi uliofanywa umebaini aliyefariki ni Steven Kimario (55), mkazi wa Sanya Juu wilayani Siha, ambaye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira, baada ya kukutwa akifanya jaribio la kubaka mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka tisa.
 
Mawasiliano hayo una ushahidi nayo?Na je!?Yaliashiria jambo lolote baya juu ya Ben?
Maana mkuu Lizaboni mawasiliano tunayosema ni lazima yawe "evil oriented"
Kwa hiyo criminal sociology tu inakupasa uwe na uwianisho huo
tafuta press conference ya Tundu alisema mwenyewe.............
 
bavicha limewafika, hapa ndugu Focus atakuwa kaamua kuwa muwazi kama Zitto ili kumuokoa mwanaye, kwani Chacha Wangwe (RIP) yalimkuta, hapa naona ameamua kumshika mchawi moja kwa moja.Kudos Focus!
Poleni sana. Shetani atazipokea sala zenu kama vile ilivyo kwa wachawi wengine ambao wamepata cha kutafutia bk 7.
 
Back
Top Bottom