Floyd Mayweather kuinunua Newcastle na kumsajili Christiano Ronaldo

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,315
Mwanamasumbwi mwenye sifa, mikogo na majivuno makubwa nchini Marekani, Floyd Mayweather amekuja na jipya wiki hii baada ya kudai anaweza kuinunua klabu ya Newcastle United ambayo ipo sokoni kwa sasa na kumshawishi mchezaji bora wa dunia na mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo kumalizia soka lake lakulipwa ndani ya timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Mayweather ambaye ni bondia machachari awapo ndani na nje ya ulingo na anayetamba zaidi kuwa na fedha za kutosha amesema kuwa anafikiria kufanya uwekezaji katika soka.

Klabu ya Newcastle imekuwa kwenye harakati za kupata mmiliki mpya baada ya Mike Ashley kusemekana kuvunja mazungumzo kati yake na Amanda Staveley ya kuinunua timu hiyo.

Ni vyema ukaamini kuwa ningeweza kuwekeza, ningekuwa na kwenda mara kwa mara bondia huyo amekieleza chombo cha habari cha the Star siku ya Jumapili.


Nimekutana na baadhi ya wachezaji wa Newcastle mwaka jana, niwatu wema. Siku zote naanzisha nafasi za biashara na napenda michezo yote lakini nawekeza kutokana na kichwa changu kinavyonituma na siyo kutoka moyoni.

Kuwekeza kutoka ndani ya moyo ni rahisi kupata hasara lakini mtu akijitokeza na kushirikiana katika mipango ya kibiashara ni rahisi kutengeneza fedha, hivyo ningependa kuwekeza katika soka hatakama siyo mchezo wangu kwakuwa nina watu kila sehemu.

cristiano-ronaldo-mayweather-instagram_806x605_61521523559-600x450.jpg
a88dc7485aafc193fcd8b25e5375054d-600x338.jpg
 
hii ndo bongoland mkuu ...anyway hhuyu jamaa hana financial advisor? ila anyway hela zikizidi kupita kiasi nahis usipokua managed vizuri unakua mental hivi.. kuna siku tutasikia anataka kununua nchi aishi peke yake...
Pesa zinapenda kuamrisha sana, usipokuwa imara utafanya vitu vya hovyo hovyo.
Pesa huamuru ule nini na usile nini kutona na unazo kiasi gani.
Au uende wapi na usiende wapi
 
Rangi nyeusi tuna matatzo sana
aje awekeze stand..
Anafkiri kuendesha timu ya mpira Ni kama kununulia watu bia?
Mbona waswahili mnapenda kuwa negative? Yaani sababu amefanya hivi mtu mweusi tayar mshaanza kuona kuwa hataweza
Aje awekeze njombe mji
Huyu jamaa akifilisika, na ndiko aelekeako, atatumiwa kama sampo ya ujinga na upvmbavu wa watu wenye rangi nyeusi kwenye mashule vizazi vijavyo.
Mjinga tu Mayweather show off za kishamba utafikiri hajazaliwa state
Ha ha haaaaa
Huyu zake anazijua yeye
Chuki na wivu
wabongo bwana tukipata vihela tuna mbwembwe ona sasa huyo mluguru anadhani kumiliki klabu mchezo!!
utajiri alionao unajua kiasi gani unijulishe?ila kitu mipango ndo maana kataja kumchukua Ronaldo,anajua utaweza kutengeneza Pesa ndefu kwa kuuza jezi na matangazo mbali mbali ya biashara hahah
Haaa haaaa haaaa mkuu umenivunja mbavu
Na asipo filisika atatumiwa kama mfano.
na kielelezo cha mtu mweusi mwenye mafanikio.
Sasa inakuaje wewe zako huzijui?
Mmiliki wa sasa mr. mike, tokea 2007 ametumia zaidi ya Trilioni 1 na Bilioni 250 za kitanzania... hio ni kuinunua na gharama nyingine za wachezaji wapya na mambo mengine, sasa jamaa anataka mtu ambaye anaitaka newcastle ainunue si chini ya Trilioni 1 na Bilioni 430 za kitanzania,
dogo floyd kufikia january mwaka huu alikua na utajiri wa Trilioni 2 na bilioni 260 za kitanzania..kwaio pengine jamaa liko siriaz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom