Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,460
- 39,928
Nimejikuta na search google na yahoo kuhusu "ajali za basi" na kuangalia picha mbalimbali za ajali. Mara moja niliona pattern fulani hiyo ambayo imenifanya niulize swali kwa wenzetu wanaojua mambo ya engineering, physics and mechanics au hata metallurgy kuhusiana na mabasi yetu. Ukiondoa vijibasi vidogo vinavyoingizwa nchini mabasi mengi makubwa na malori yanaunganishwa nchini. Mengine yanatumia chasis za malori na kuwekwa body n.k Nakumbuka kulikuwepo hata na kampuni ya "Quality Bodies" or something like that. Lakini nimeangalia kidogo ajali hizi na madhara yake na nimeanza kujiuliza kama ukiiondoa tatizo la barabara yawezekana kuna matatizo ya msingi (structural problems) kwenye mabasi yetu? Na maswali mengine yakaanza:
a. Ni chombo gani kinasimamia quality ya mabasi yanayounganishwa nchini?
b. Viwango (standards) kinachotakiwa katika mabasi ni kwa kiasi gani kimeletwa katika uelewa wa sayansi na teknolojia ya karne hii mpya?
c. Kabla mabasi hayajaingia kwenye huduma yanafanyiwa kwa kiasi gani majaribio ya kuhimili mikikimikiki (stress tests) ili kuhakikisha yatabehave vipi katika ajali maana baadhi ya mabasi ukiyaona unashindwa kuelwa kama ni impact peke yake inayosababisha madhara hivyo au hata structure ya basi haiko katika kuhimili mikikimikiki?
d. Baada ya kulaumu "mwendo kasi" mara nyingi ajali zinapotokea au "kutokufuata sheria za usalama barabarani" yawezekana kuna maelezo ya kifizikia ya ajali hizi - kwa mfano uhusiano wa mwendo, uzito na impact au nguvu (force)? Yawezekana wasomi wetu kama walivyoshindwa kuukosoa ubepari (I couldn't resist that) wameshindwa kufanya utafiti wa kisayansi wa kuelewa chanzo cha ajali hizi (badala ya kukubali tu kuwa dunia ni flat) na kuja na mapendekezo ya nini kifanyike katika uungaji wa magari, maumbo yake n.k?
e. Je muundo wetu wa barabara unachangia vipi kutokea kwa ajali hizi (kwa mfano eneo la Mikumi, Kibaha) ni kinara wa ajali kwanini?
Ninaamini kabisa kuwa na sisi tuna uwezo na wapo watu wenye uwezo wa kuangalia mambo haya kisayansi na kuyaelewa na kuja na mapendekezo ya kisayansi badala ya "kudra" na kusema ni "mapenzi ya Mungu". Anybody?
Angalia hizi picha na jiulize maswali yako na kama unamawazo ya majibu