Jioni ya leo nimebahatika kuongea na dereva wa mabasi ya mikoani ambaye anafanya kazi katika moja ya kampuni kubwa. Nimemwuliza kuhusu ajali nyingi tunasikia tairi za mbele zimepasuka. Anasema kuanzia wamiliki wa mabasi,trafiki,sumatra na wao kama madereva wanajua tatizo ni matairi yasiyokidhi viwango. Anasema ni kampuni chache sana ambazo hazizidi hata 7 magari yao yanafunga tairi mpya za michelin ama bridgestone. Anasema ajali zote tunazisikia za kupasuka tairi za mbele,magari yanakua yamefunga tairi za kichina. Kuhusu ajali ya basi la Deluxe anasema basi ilikua chakavu na tairi za mbele zilikua vipara!