Fizikia ya ajali (The Physics of Accidents): Mabasi yetu yanaundwa au kuunganishwa wapi?

Kupasuka kwa matairi ya mbele ni kitu ambacho kingetokea mara chache sana kama tungekuwa tuna standards za maana zinazofuatwa na barabara nzuri, pia sina uhakika kama unaweza kuweka matairi mawili mawili mbele kwa sababu za steering.
Chukulia gari hilo lina pasuka tairi barabara ya morogoro na kuteremkia kwenye mitaro mikubwa kama handaki! Afu analaumiwa gari, HATUNA VIWANGO VYA BARABARA PIA NI WABISHI NA WENYE KUJALI MASLAHI BINAFSI KWENYE TAALUMA ZETU. Barabara iliosanifiwa vizuri inamwezesha dereva kuokoa gari pindi inapotokea. If there is no clear zone or adequate recovery basi tutumie magari kama vifaru ili yakabiliane na ajali za kujitakia. Tunahitaji kutibu source ya tatizo wala simatokeo ya tatizo.
 
Mkuu nafikiri umesoma thread kuanzia Sept 27 2011, pia ume-download na attachment. Lakini kinachonishangaza zaidi umetoa jibu rahisi kwenye swali gumu, hasa kuhusu mabadiliko ya wataalam wanaoongoza idara husika. Swali langu ni je wataalam hawa wanaupungufu gani uliounona wewe ambao wakiondolewa na kuwekwa wapya matatizo yataisha?, je wataalam hawa wanahusika vipi uendeshaji wa mabasi haya?. Hoja yako ingekuwa na mashiko kama ungeelezea maeneo yafuatazo
  1. Usimamiaji wa sheria za barabarani
  2. Usimamiaji wa ubora wa vyombo vya usafiri na ukaguzi wa kuona kama vinafikia kiwango kinachostahili
  3. Usimamiaji wa utoaji wa leseni za udereva wa magari ya abiria
  4. Usimamiaji na uajenzi wa barabara zinazikidhi kiwango cha usalama wa raia na magari yao
Ukiangalia mambo hayo utakuta ni ta kimfumo zaidi ya kuangalia individuals. Suala la Public safety kwa Tanzania is not a political issue, na hakuna mtu anayejali. Ndiyo maana unakuta barabara inajengwa na mkandarasi, ikikabidhiwa kunakwa hakuna Road maintenance ang managament programmes, mifereji inajaa, vituo vya mabasi vinaangukia watu no body feel responsible. Mtu anaomba leseni ya usafirishaji na kupatiwa bila hata kuangalia kiwango cha gari lake kiko vipi. Unakuta Kampuni inaongoza kwa ajali na bado inaendelea kupata na biashara. Mtu anaamua kubadili Lorry kuwa Bus bila ya kuzingatia the design purpose of a chasis, centre of gravity and stability of a vehicle with live load and then anaruhusiwa kutoa huduma.

Mi nafikiri tunahitaji kuanzia na System kwanza. Hapa nina maana watunga sera, wasimamiaji na wenye mamlaka ya maamuzi. Tanzania tunaishi katika law of the jungle, struggle for existence survival for the fittest. No body cares wewe utapatwa na masahibu gani kwa uzembe wa waliokuwa na dhamana. Kinachoangaliwa ni pesa zaidi usalama.

Mfano katika ujenzi wa barabara, kuna wakati ilifikia milingoti ya taa za barabarani zilikuwa zinagingwa gingwa sana, Solution yake ikawa ni kujengea Column (Concrete column) ili dereva agonge zege na kunusuru mlingoti, maana yake ni kwamba watu wagonge zege na magari wafe ili nguzo ya taa za barabarani ibakie salama. Huu ni upuuzi mkubwa sana, badala ya kuimarisha usimamizi wa sheria barabarani na utoaji wa leseni ambao ndiyo sababu, watu wanalewa na kuendesha magari bila hofu ya kutiwa nguvuni na mkono wa sheria, kwa uvivu tunaweka solution ya 'Nobody cares for your life but we care for our electric post'.
Naelewa nasema nini, mabadiliko ni ya kifra wala sikutoa walewale na kuchomeka walewale. Kuna watendaji waandamizi toka wapate shahada zao pale chuo hawajastuka kujiendeleza ama kuchukua kozi za muda mfupi zi waoneshe dunia inaelekea wapi kwenye fani husika.
Samahani, nafuatilia ajali za barabarani toka mwaka 1998. Suluhu ya mabodi ni sawa na wale wanaoimba kuteketeza ugonjwa wa malaria kwa kugawa chandarua!
Umeongelea utekelezaji wa sheria ya usalama barabarani. Je unatambua kuwa imepitwa na wakati na haitekelezeki kutatua matatizo ya usafiri. Sheria yetu ni BUTU!
Umezungumzia barabara kujengwa kwa viwango, mbona nchi yetu haina viwango vya usanifu wa barabara. Chukulia barabara tano tofauti tanzani utaona zimejengwa tofauti, kwa sababu hatuna viwango.
Uvivu wa kufikiri na kujiendeleza ndo unafanya tunashindwa kubadilika. Kwa bahati mbaya kila sekta Tz imekumbwa na tatizo hili. But one we will change.
 
Kwa kweli tatizo la ajali limekuwa sugu sasa na hakuna hatua za makusudi ambazo zimechukuliwa na major players (wamiliki, watumiaji na regulators) kutatua hili tatizo. Tatizo la ajali Tanzania sasa linajulikana kimataifa. Kwa mfano, serikali ya Uingereza inashauri wananchi wake walio au wanaotembelea Tanzania wasipande mabasi ya masafa marefu kwa sababu yanapata ajali mara kwa mara (Tanzania travel advice) Pamoja na haya yote ajali zikitokea bado tunasema ni mipango ya Mungu. Kama ni mipango ya Mungu basi Uingereza isingewashauri wananchi wake wasipande hayo mabasi kwa vile wakipata ajali na kufa ni mipango ya Mungu.

Ili tuweze ku address hili tatizo ni muhimu kujua vyanzo za hizi ajali. Kuna tafiti nyingi tuu kuhusiana na sababu za ajali za mabasi. Naamini pia ukitembelea libraries zetu utakuta studies nyingi juu ya hili tatizo lakini zinajazana vumbi tuu mle. Sababu mbalimbali zimetolewa. Lakini mimi bado naamini human factor is the major cause of these accidents.

Kuna wataalamu wamefanya study juu ya chanzo cha ajali za mabasi kwenye nchi tano ambazo ni Nepal, Zimbabwe, Thailand, India na Tanzania (http://www.transport-links.org/transport_links/filearea/publications/1_549_PA3574 .pdf). Study inasema kuwa Tanzania ni nchi ya tatu duniani inayoongoza kwa ajali baada ya Afrika ya Kati na Ethiopia. Kwa upande wa Tanzania, study inasema kuwa:

The operational environment for long distance services changed recently. Quantity and fare controls on routes have been liberalised and entry into the industry is now very much dependent on the roadworthiness of the vehicle. The most common buses are 45 – 65 seat capacities. Driver turnover is high and due to an increasing passenger fleet buses compete for passengers by employing touts. It is alleged that, buses race against each other in order to pick up intermediate passengers along the route, on the other hand, the competition for passengers has resulted in some operators introducing semi-luxury and luxury coaches on selected routes to attract more passengers.


Kuhusu sababu zinazosabisha ajali study inasema kuwa:

The travelling public blames deregulation of the public transport system for the increased number of accidents occurring on both urban and long distance services. Inevitably this has led to an increase in the number of buses servicing the network although demand has not similarly increased.

As per police analysis the causes of all road accidents [bus accidents reflect the same trends] can be divided into three main categories:​
• Human factors = 76%​
• Vehicle condition = 17%​
• External factors = 7%

Interviewees' perceptions were that human errors are the principal contributory cause of road accidents. The causes of bus accidents as revealed by respondents are similar to the above but also includes an additional factor "lack of enforcement". The contribution of human error in causing accidents is not only confined to drivers as passengers and pedestrians also contribute to accidents. It is common for passengers to try to disembark from a bus while it is in motion or to distract the attention of the driver. Some fatal bus accidents may occur when drivers take irrational decisions and attempt to cross flooded rivers. Drivers are often encouraged by passengers to cross flooded bridges and as a result make errors in judgement resulting in the bus being washed away.


Nafikiri hata watumiaji wenyewe wa mabasi wanachangia. Unakuta abiria wanaona kabisa basi linakimbia kwa mwendo wa kasi lakini wanakaa kimya. Kuna member mmoja alianzisha thread hapa akiwa kwenye basi akidai kuwa basi linaenda kwa mwendo wa kasi sana. Pamoja na kwamba alikuwa kwenye hakuchukua hatua yoyote zaidi ya kutuma hiyo thread hapa. Kwa hiyo tukubali tusikubali hata sisi abiria wenyewe tunachangia.

Nilishapanda basi moja kwenda huko kaskazini wakataka kutufikisha bila hata kupata chai. Tulipolalamika konda akiungwa mkono na baadhi ya abiria akadai eti kuna abiria ambao wanawahi kwenye mazishi saa nane mchana. Hapa badala ya kuwa mazishi unawezajikuta unajitengenezea mazishi yako mwenyewe. Lakini pia kama study inavyosema kuna link between the degree of privatisation, the amount of regulation or enforcement and the severity of accident.

Kwa hiyo, tukitaka kupunguza hili tatizo kuna mambo mengi sana ya kuangalia ambayo yata involve wamiliki, madereva, makondakta, mafundi, polisi, serikali, regulators, utoaji wa leseni, manufacturers, repairers of vehicles, spare parts and tyres na watumiaji wote wa barabara. Study imetoa recommendations nyingi tuu.
 
bado sijasikia ni wapi mabasi haya yanaunganishwa na ni chombo gani kinasimamia? tuachane na ya Katiba mpya kwanza tuzungumzie right now tusije kudhania katiba mpya itatatua matatizo ya ajali au matatizo mengine yoyote yale. Kuna vitu tunaweza kuvifanya sasa hivi

Mkuu, mabasi mengi yanayotembea Tanzania kwa sasa body hazitengenezwi na Quality Garage or Banbros, Marva za Nairobi-Kenya or kampuni zenye kibari rasmi cha kuunganisha bodies. Hizi kampuni moja ya masharti yake kutengenezewa bus ni kupeleka new chasis ya bus or bus lililipata ajali na kubadilishiwa body. Gharama zao ziko juu na matajiri wengi wa mabasi hawanunui chasis mpya ya basi ilo linajulikana.

Garage zinapatikana wapi? Hood,na Abood wana yard zao Morogoro, Simba coach yao ipo Tanga zilianza kwa ajili ya ukarabati wa basi likipata ajali, sasa nao wanatengeneza body- basi zao nyingi ni Scania model 92H-manufacture date 1987.Matajiri wengi wananunua aina hii ya Scania kwa sababu chasis yake ni ndefu na ngumu. Hata ikitokea hajali haipindi, tajiri anakuja kuokota chasis na kuunda bus jipya. Jiulize kwanini Tanzania bus nyingi ni Scania 92H, Tangu Mswiden atengeneze sasa ni miaka karibia 25 lakini ukiikuta Tanzania ni kama vile imetoka jana kiwandani?:))

Viwanda vingine vidogo vidogo vipo Temeke, na buguruni.Mabasi mengi yanayoenda Mikoa ya kusini na Tanga yanatengenezeo huko.Nilishawai kusafiri na AKIDA coach kutoka Nachingwea-Dar, na kusahau kifurishi, nikaelekezwa kwenda kuchukua kwenye Garage yao Temeke, sikuamini kukuta wanatengeneza body ya new Akida bus.Nilipoukiza material wanapata wapi. Bati na vyuma/bomba wananunua Gerezani Kariakoo: Pia wanapata bati nyingine kwenye basi za zamani (hizi wananunua UDA-kurasini au kwenye minada ya magari chakavu ya serikali kama jeshini).Kapeti na mazuria ya ndani ya basi nako yananunuliwa huko huko Gerezani. Kama haitoshi nilishasafiri tena na Southern coach kutoka Masasi-Dar nilipakia mbao, nikaenda kupakulia kwenye yard yao Temeke nao nikakuta wanategeneza body.

Mafundi wa body wanawapata wapi? kwanza waliokuwa wafanyakazi na vibarua wa TAMCO wengi sasa wapo kwenye hivyo viwanda, pili wanafanyazi wa Quality Garage na kampuni nyingine zilizokua zinaunganisha body zamani, wanawaajili permanent or temporary. Urafiki huu ulianzaje? Unapowapelekea taarifa kwamba bus lako limepata ajali na wakupe appointment ya kulipekeka or waje kulichukua kwenye yard yako, hapohapo wafanyakazi wengine wanafanya deal kwamba kama wakija kukutengenezea huko huko kwako gharama zitapungua maana utalipa labour cost tu, wakati ukipeleka kwao mfano TAMCO or Quality Garage itabidi ulipe gharama nyingi zaidi. Kwa wafanyakazi iyokua TAMCO hili wanalijua.

Shida ya hizo body za mabati na vyuma vya gerezani ni magumu sana na hawana technologia ya kuyeyusha,ndio maana mara kwa mara uzito unazidi wanapokwenda mizani hata kama wana abiria na mizigo michache, pia izo bati kipindi cha ajali zinachinja kama visu na kufunuka kama mianvuli (refer picha ya kwanza ya ajali ya hood). Abiria wengi wanakufa kwa kukatwa na bati.

So suala la stress test na nyinginezo za kupima ubora wa body hapa hakuna na msahau. Serikali inashangia kwa hili, mwaka juzi chama cha wenye mabasi mikoani waliomba wapunguziwe ushuru wa kununua chasis or basi mpya, serikali ikagoma, so tunategemea nini?. Shida yetu ni ile ile hatuishiwi na nahau tamtamu kama ajali aina kinga, ni mipango ya mungu, uzembe wa dereva, ilukua inakuimbia sana na nyinginezo lukuki-huku watu wanaendelea kufa. Thx mwkjj kwa kuleta hii mada may be unaweza kuwazindua usingizini wahusika.
 
Nadhani suala la makosa ya watu kama inavyooneshwa kwenye hiyo ripoti ninashuku kwa sababu ni imani ambayo imekuwa ikijengwa mara kwa mara kuwalaumu madereva. sijui kama ni kweli ni kosa la madereva kwani haiwezekani mabasi mbalimbali yanapata ajlai zinafanana wakati madereva ni tofauti tofauti - kwanini ajali ziwe zinatokea kwenye mabasi zaidi na siyo malori au magari mengine makubwa? Kwanini kwa mfano hatusikii malori ya mafuta yakipinduka pinduka wakati yanapita kwenye barabara hizo hizo?
 
ABIRIA WATEKETEA NDANI YA BASI (Mwananchi)
Juliet Ngarabali, Pwanina Furaha Maugo, Dar
VILIO, majonzi na mayowe jana vilitawala eneo lote la Misugusugu katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam - Morogoro wilayani Kibaha mkoani Pwani, pale basi la Kampuni ya Deluxe lilipopinduka kisha kuwaka moto na kusababisha abiria zaidi ya 25 kuungua.Ajali hiyo ni mbaya zaidi ya zilizotokea hivi karibuni katika barabara hiyo kwani baadhi ya abiria waliteketea kabisa na kubaki majivu huku wenzao wachache waliowahi kutoka ndani ya gari hilo wakishuhudia, lakini hawakuweza kusaidia kuwaokoa.

Ajali hiyo lilitokea saa 9:00 alasiri na basi lililohusika na tukio hilo ni aina ya Volvo mali ya kampuni Diluxe, likitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Polisi wathibitisha
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ernest Mangu alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo alisema ni abiria 17 tu ndio walionusurika na kwamba kumi kati yao walipata majeraha ya kawaida wakati wengine saba walipata majeraha ya moto.

Kamanda Mangu alisema majeruhi wote walikimbizwa kupelekwa katika hospitali teule ya Tumbi, Kibaha .

Mangu alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa gurudumu la mbele kulia la gari hilo ambalo baadaye lilipinduka na kutumbukia korongoroni na kuwaka moto ambao kila baada ya dakika chache ulionekana kuongezeka kuwa mkubwa kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma muda huo wa alasiri.

"Kwa kweli hii ajali naweza kusema ni mbaya na inasikitisha sana maana ni abiria wachache tu ndio walioweza kuokolewa na wenzao zaidi ya 25 tunakadiria waliungua na kuteketea kabisa hadi kuwa majivu kutokana na moto uliokuwepo kuwa mkubwa sana,"alisema Mangu.

Alisema ajali hiyo kama ikilinganishwa na zilizotokea hivi karibuni mkoani humo, wao kama polisi wanakiri hiyo ya jana ni mbaya zaidi na inayosikitisha kwani idadi halisi ya abiria walioteketea haijajulikana na kwamba ofisi yake inafuatilia zaidi kujua idadi halisi ya abiria waliosajiliwa kwenye ofisi za basi hilo Ubungo Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, basi hilo lilikuwa limebeba abiria 42 kutoka Ubungo, lakini kukawa na taarifa kwamba huenda idadi hiyo ikawa imeongezeka kutokana na abiria wengine waliopandia njiani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabani, Mohamed Mpinga, alipoulizwa jana jioni alisema bado haikuweza kuthibitika mara moja idadi halisi ya waliofariki na majeruhi.
Mpinga ambaye alikuwa eneo la tukio alisema uchunguzi na juhudi za kufahamu idadi halisi ya vifo na majeruhi ilikuwa ikifanyika.



Mashuhusa wa ajali
Hata hivyo, taarifa zisizo rasmi zinaeleza awali, basi hilo liliondoka katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo kikiwa na abiria 45, lakini walikuwepo wengine baadhi ambao walipandia njiani katika eneo la Kimara, Mbezi na Maili Moja Kibaha.

Kwa upande wao mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema basi hilo lilikua kwenye mwendo kasi na lilipofika eneo hilo walisikia kishindo kikubwa na walipofuatilia waliona basi hilo likitumbukia kwenye mtaro mkubwa pembezoni mwa barabara huku moshi mkubwa ukifuka kutoka ndani ya gari hilo.

''Sisi kama kawaida yetu tulikua kijiweni na hili basi lilitupita kwa kasi hapa, lakini muda mfupi tulisikia kishindo na tukatoka na kufatilia, tukagundua ni ajali, tulianza kukimbilia kuokoa watu, lakini masikini tulifanikiwa kuwatoa 10, moto ukawa umetuzidi nguvu. Wengi wakawa wanalia kuomba msaada,”alisema Ramadhani Hussein na kuongeza:,

Shuhuda mwingine, Adam Sultan alisema chanzo cha ajli hiyo ni uzembe wa dereva ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake hali eneo hilo halistahili kufanya hivyo kwa kuwa lina mlima.

Kwa upande wa shuhuda Abdallaha Kijukuu alisema kuna uwezekano mkubwa kwamba ajali hiyo imesababishwa na mtarimbo unaoshika matairi ya nyuma (diff), kwamba ilikuwa imepata moto kisha kusababisha gari hilo kupinduka.Mashuhuda hao walisema baada ya ajali hiyo kutokea, waliamua kusogelea gari kwa ajili ya kuokoa watu, lakini walikuta vioo vyote vimefungwa hivyo walianza jitihada za kuvipasua ili kuokoa watu hao.

Alisema walifanikiwa kuokoa majeruhi 8 na wengine walitoka wenyewe na kukimbia eneo la tukio wakati gari likifuka moshi.Majeruhi anena
Mmoja wa majeruhi wa ajali, Danda Juju alisema kwamba huenda kukawa na zaidi ya abiria tisa waliungua ndani ya basi hilo. ,” Nilitokea dirishani na nikaanza kuokoa baadhi ya watu kupitia madrisha mawili tu, moto ulipozidi sikuweza kuendelea, lakini kwa haraka nadhani kama watu tisa watakuwa wameteketea ndani kwa moto,” alisema Juju ambaye ni kada wa NCCR-Mageuzi
Kwa upande wake, Juju alisema ameumia kwenye mguu na mkonono, lakini hali yake haikuwa mbaya sana hivyo aliweza kurejea nyumbani kwake Dar es Salaam.

My Take
Swali la Kifizikia:

Inakuwaje madirisha hayavunjiki au kufunguka kwa nje? Nani anasimamia quality standards za wanaunganisha mabodi ya magari?
 
Mkuu nakumbuka baada ya ajali ya Mohamed Bus kule Singida ambapo gari iliwaka moto na watu kuungulia ndani, kulitolewa tamko kwamba magari yote yawe na milango ya dharura. Kama kawaida yetu ufuatiliaji ulifanyika kwa siku mbili tatu kisha ikawa kimya!!! Sina hakika kama hilo bus lilikuwa na mlango wa dharura na pia sina hakika kama lilikuwa ni bus au Fusso.

Tutasikia tena Mpinga akitoa amri ambazo huwa hazifuatiliwi!
 
ABIRIA WATEKETEA NDANI YA BASI (Mwananchi)

My Take
Swali la Kifizikia:

Inakuwaje madirisha hayavunjiki au kufunguka kwa nje? Nani anasimamia quality standards za wanaunganisha mabodi ya magari?
Iwapo madirisha yote hayafunguki, basi lazima kuwepo na kifaa cha kupasua dirisha juu ya kila dirisha ndani ya basi.
 
Nimejikuta na search google na yahoo kuhusu "ajali za basi" na kuangalia picha mbalimbali za ajali. Mara moja niliona pattern fulani hiyo ambayo imenifanya niulize swali kwa wenzetu wanaojua mambo ya engineering, physics and mechanics au hata metallurgy kuhusiana na mabasi yetu. Ukiondoa vijibasi vidogo vinavyoingizwa nchini mabasi mengi makubwa na malori yanaunganishwa nchini. Mengine yanatumia chasis za malori na kuwekwa body n.k Nakumbuka kulikuwepo hata na kampuni ya "Quality Bodies" or something like that. Lakini nimeangalia kidogo ajali hizi na madhara yake na nimeanza kujiuliza kama ukiiondoa tatizo la barabara yawezekana kuna matatizo ya msingi (structural problems) kwenye mabasi yetu? Na maswali mengine yakaanza:

a. Ni chombo gani kinasimamia quality ya mabasi yanayounganishwa nchini?
b. Viwango (standards) kinachotakiwa katika mabasi ni kwa kiasi gani kimeletwa katika uelewa wa sayansi na teknolojia ya karne hii mpya?
c. Kabla mabasi hayajaingia kwenye huduma yanafanyiwa kwa kiasi gani majaribio ya kuhimili mikikimikiki (stress tests) ili kuhakikisha yatabehave vipi katika ajali maana baadhi ya mabasi ukiyaona unashindwa kuelwa kama ni impact peke yake inayosababisha madhara hivyo au hata structure ya basi haiko katika kuhimili mikikimikiki?
d. Baada ya kulaumu "mwendo kasi" mara nyingi ajali zinapotokea au "kutokufuata sheria za usalama barabarani" yawezekana kuna maelezo ya kifizikia ya ajali hizi - kwa mfano uhusiano wa mwendo, uzito na impact au nguvu (force)? Yawezekana wasomi wetu kama walivyoshindwa kuukosoa ubepari (I couldn't resist that) wameshindwa kufanya utafiti wa kisayansi wa kuelewa chanzo cha ajali hizi (badala ya kukubali tu kuwa dunia ni flat) na kuja na mapendekezo ya nini kifanyike katika uungaji wa magari, maumbo yake n.k?
e. Je muundo wetu wa barabara unachangia vipi kutokea kwa ajali hizi (kwa mfano eneo la Mikumi, Kibaha) ni kinara wa ajali kwanini?

Ninaamini kabisa kuwa na sisi tuna uwezo na wapo watu wenye uwezo wa kuangalia mambo haya kisayansi na kuyaelewa na kuja na mapendekezo ya kisayansi badala ya "kudra" na kusema ni "mapenzi ya Mungu". Anybody?


Angalia hizi picha na jiulize maswali yako na kama unamawazo ya majibu

Mwanakijiji nimefurahishwa na mada yako ya ajali kwani inatutaka tutumie akili zetu ambazo kwa bahati mbaya tumeamua kwa makusudi kabisa kuziweka akiba ili funza wazifaidi zikiwa fresh tutakapokufa na kuzikwa.

Mimi siyo mwanasayansi na sina majibu ya kifizikia kuhusu uwezo wa mabasi yetu kuhimili misukosuko ya barabarani hasa ukizingatia kuwa mengi ya mabodi ya mabasi yanatengenezwa vichochoroni. Nitajaribu kujibu maswali mengine kutokana na uzoefu kidogo nilionao kwenye sekta ya usafiri nchini.

(i) Chombo kinachotoa miongozo ya ubora (standards) na kusimamia ubora wa bidhaa nchini ikiwemo ubora wa viwango vya mabasi ni TBS na ninavyofahamu wana viwango vya mabodi ya mabasi yanayoruhusiwa nchini. Tatizo TBS imebaki jina tu sidhani kama wana uwezo wala nia ya kusimamia ubora wa mabodi yanayotengezwa kila sehemu nchini.
(ii) Viwango vya ubora wa mabodi ya mabasi vipo ila sijui kama vimehuishwa kwa kuzingatia uelewa wa sayansi na teknolojia ya karne hii mpya. Tatizo kubwa ni uwezo mdogo wa TBS wa kusimamia viwango hivyo ukianzia na suala la kusajili karakana za kutengeneza mabodi ya mabasi zinazokidhi viwango vinavyotakiwa.
(iii) Sijawahi kusikia mabasi yakifanyiwa 'stress' test hapa nchini na wala sidhani kama hilo ni moja ya masharti ya TBS kwa hizi karakana zinazotengeneza mabodi ya magari nchini. Ninachojua ni kuwa sheria ya Traffic inataka kabla basi halijaruhusiwa kubeba abiria lifanyiwe ukaguzi wa kina na jeshi la polisi kuona kama linakidhi viwango vya kutembea barabarani (road worthiness test). Kwa bahati mbaya sana uzoefu unaonyesha kuwa jeshi la polisi halina uwezo wala nia ya dhati ya kusimamia zoezi hili la ukaguzi wa vyombo vya kubeba abiria. Ukweli ni kuwa huu umegeuzwa kuwa ni mradi wa kutengeneza pesa za rahisi kwa wahusika.
(iv) Kuna tatizo kubwa zaidi la mfumo wa kisheria wa udhibiti wa madereva nchini. Dereva anafundishwa na chuo cha VETA au mitaani kwenye chuo kilichoidhinishwa na VETA na anapatiwa cheti cha ufaulu wa mtihani wa udereva. Akipata cheti anaenda Polisi ambao wanamfanyia test kuona kama anajua udereva. Akimaliza anapewa kinachoitwa certificate of competency ambayo inapelekwa TRA kwa ajili ya kupata leseni. TRA wao interest yao kubwa ni kodi na hivyo kwao hii leseni ni moja ya nyaraka tu za kufanikisha ukusanyaji wa kodi. Akisha pata leseni anakuwa kiumbe huru ambaye hana taasisi yoyote inayomsimamia wala kufuatilia nyendo zake za kila siku ukiacha hawa matraffic ambao huwa wanamsimamisha anapofanya makosa na kuomba kitu kidogo. Hakuna mawasiliano yoyote ya maana yaliyo endelevu kati ya chuo kilichomfundisha udereva, polisi waliompa mtihani na TRA waliompa leseni na hana chombo chochote kinachomsimamia kuona anaendesha vipi magari.
(iv) Ukweli ni kwamba unaweza kupata nyaraka za kiserikali zote zinazoonyesha kuwa umehitimu udereva bila ya kupitia mafunzo yoyote ya udereva na leseni ya udereva kwa kutoa rushwa kwa watu wachache tu. Hivyo tuna madereva wengi kwenye system ambao sio madereva wahitimu.
(v) Kuhusu muundo wa barabara sina maelezo kwani sio mtaalam wa eneo hilo ila naamini kuwa ukiwa na dereva mahiri na usimamizi mzuri wa sheria za barabarani suala la muundo wa barabara haliwezi kuwa chanzo kikubwa cha ajali. Ajali nyingi zinatokea kwa madereva kuyapita magari mengine kwenye milima au kwenye kona kali ambavyo vinawafanya wasione kuna nini mbele. Dereva makini hawezi kufanya kosa hilo la kizembe hata kama barabara itakuwa haioneshi alama ya kona kali. Lakini dereva mzembe atavunja taratibu tu hata kama barabara itakuwa ni nzuri na yenye alama stahiki za kuwaonya madereva.
(vi) Kuna suala pia la spare za magari zisizokidhi viwango kama matairi na nyinginezo. Hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa kwenye ajali za barabarani. Hata ukiwa ni dereva makini tairi la mbele la basi linapopasuka ukiwa kwenye mwendo wa km 80 kwa saa unahitaji kudra tu za mwenyezi mungu kuepuka ajali.

Nakupongeza kwa kutoa changamoto hii ambayo inataka tubongoe bongo zetu ili kupata suluhisho la kudumu la ajali za barabarani.
 
Mkuu kama kuna mtu atatokea na kujibu hayo maswali basi hili tatizo la ajali litapungua sana hapa nchini. Kuna wakati nilisikia kuwa mabasi mengi yamejengewa tu bodi za mabasi ila yalistahili kuwa malori/mafuso ya kubeba mizigo. Likatolewa tamko la kwamba mwisho wa hayo malori/mafuso kutumika kama mabasi itakuwa siku fulani (nadhani imepita miaka miwili) lakini hadi sasa hayo magari yapo barabarani!! Ilimaminika kuwa hayo malori mabasi yanakuwa yamepewa mzigo mdogo kulinganisha na yanachotakiwa bubeba yakiwa malori kwa hiyo speed huwa kubwa.

Lakini pia kuna hili suala la barabara hasa design. Nasikia barabara zetu zimekuwa designed kwa kuhimili mwendo wa KM 100 kwa saa na si zaidi ya mwendo huo.

Mkuu hapo kwenye nyekundu sio sababu ya msingi, design speed inategemea alignment ilivyo sio kweli kusema kuwa ni 100km/h sehemu nyingine inakuwa more than that.Lakini hata hivyo kama design speed ni 100km/h kuna control speed ( posted speed limit) ambayo yenyewe ni always less than design speed ya alignment husika, hii ndo speed ambayo driver anatakiwa aendeshe gari.
 
Mtazunguka kila angle lakini sababu kubwa ya ajali za Tanzania ni human error kwa maana ya kwamba speed kali.

Mabasi karibu yote yanaenda speed kati ya 120km/h mpaka 150km/h katika barabara ambazo maximum speed ni 80km/h.

Kupasuka mataili kunatokea duniani kote. Ila taili likipasuka wakati uko kwenye 80km/h kuna nafasi kubwa kuweza ku control gari mpaka likasimama. Lakini kama speed ni 120km/h au zaidi sio rahisi kabisa kuweza kulisimamisha hilo gari salama katika barabara ambayo ni nyembamba na haijanyoka.

Ajali za magari zinasidia tu kutuonyesha ujinga wetu kwa maana ya kwamba pamoja na sababu kuwa wazi mno, sisi tunakimbilia kwenye sababu za kipuuzi kama mkono wa mtu au hata kulaumu gari. Fuata speed inayoruhusiwa barabarani na ghafla ajali zitapungua sana.

Nimesafiri na gari binafsi katika barabara zetu mbalimbali. Nimekuwa nikipitwa na mabasi na magari mengine utafikiri mimi natembea kwa miguu. Laiti kila mtu angefuata sheria, hizi ajali zingelipungua sana.

Lakini kwasababu Watanzania tumejijengea tabia ya kutokufuata sheria katika kila jambo, mauti ya ajali itaendelee kutuandama. Tulivyo wajinga, tutaendelea kutafuta sababu za kijinga ili kuhalalisha makosa yetu. Ajali za barabarani ni kama ukimwi tu, tunajua chanzo chake ila hatutaki kukubali ukweli. Ni rahisi kusema kuna mkono wa mtu huku unatimka 160km/h kwenye barabara ya 80km/h. Ujinga kitu kibaya sana, hasa unapoendelezwa na wasomi ambao ungetegemea waelewe risk iliyopo katika kukimbiza gari.

Dereva anaenda speed ya 120km/h huku anaongea na simu na abiria wametulia tu; wakichinjwa kwa ajali wanaanza kutafuta mchawi? Mchawi ni sisi wenyewe ambao hatutaki kufuata sheria na taratibu za nchi. Pia sisi ambao tunawashangilia maderva wazembe wanapokimbia na kulalamika tunapokutwa na majanga ambayo tungeweza kuyaepuka. Hakuna njia ya mkato kwenye hili; ignore sheria za barabarani, unajiandalia kifo cha ajali.
 
Mkuu hapo kwenye nyekundu sio sababu ya msingi, design speed inategemea alignment ilivyo sio kweli kusema kuwa ni 100km/h sehemu nyingine inakuwa more than that.Lakini hata hivyo kama design speed ni 100km/h kuna control speed ( posted speed limit) ambayo yenyewe ni always less than design speed ya alignment husika, hii ndo speed ambayo driver anatakiwa aendeshe gari.

Speed ya juu kwa Tanzania ni 80km/h. Je ni wangapi wanaendesha kwa speed hiyo?
 
Uliza hayo mabus ni ya kina nani?
Ukipata jibu ndipo utakapo jiridhisha ndo maana tunakufa kijinga
 
Kwanza niseme kwamba kama basi lipo ktk standard nzuri hiyo speed ya 80kms katika main road ni ndogo sana. Kwa uzoefu wangu wa kusafiri katika barabara za Tanzania,ajali nyingi zinasababishwa na ubovu wa magari,umakini wa madereva,muundo wa barabara na watumiaji wengine wa barabara kama watembea kwa miguu,baiskeli na daladala. Kuna jambo jingine ambalo sijui kama watu wa Tanroads wamelifanyia utafiti wa kisayansi,nalo ni hizi speed hams kama sikosei, kabla ya kufikia bumps kubwa. Magari yanapata mtetemeko mkubwa,jambo ambalo nadhani baada ya muda fulani tunakua tunasikia kuchomoka matairi ya mbele. Kuhusu muundo wa barabara zetu,ningependekeza watu wasiruhusiwe kujenga karibu na barabara lakini ikiwezekana wajenge upande mmoja wa barabara ili kuondoa uvukaji holela wa watembea kwa miguu hizi barabara zinapopita ktk vijiji na miji midogo huko mikoani.
 
Nadhani suala la makosa ya watu kama inavyooneshwa kwenye hiyo ripoti ninashuku kwa sababu ni imani ambayo imekuwa ikijengwa mara kwa mara kuwalaumu madereva. sijui kama ni kweli ni kosa la madereva kwani haiwezekani mabasi mbalimbali yanapata ajlai zinafanana wakati madereva ni tofauti tofauti - kwanini ajali ziwe zinatokea kwenye mabasi zaidi na siyo malori au magari mengine makubwa? Kwanini kwa mfano hatusikii malori ya mafuta yakipinduka pinduka wakati yanapita kwenye barabara hizo hizo?

Mkuu malori nayo huwa yanapata ajali tena kwa sana sema ajali za malori hazitangazwi kwenye vyombo vya habari. Ukisafiri kwenye barabara kuu za kwenda mikoani lazima ukutane na lori lililopata ajali. On the other hand, kama mabasi yangekuwa yanatembea kwa mwendo wa malori, ajali zingeongezeka au kupungua?

Halafu hiyo human factor haiko limited kwa kwa madereva tuu. Hata wamiliki, polisi na abiria ni human factor inayochangia hizi ajali. Kwa mfano, angalia hiyo picha hapo chini inadaiwa kuchukuliwa tarehe 16 Septemba 2011 ndani ya basi la Aboud lililokuwa likitokea Morogoro kwenda dar ambapo tiketi zilikuwa zinagawiwa kama njugu bila kujali manifest ya abiria. Kama vile haitoshi polisi wa trafiki nae aliomba lift na kuwa miongoni mwa abiria wasiokuwa na viti vya kukaa kama picha inavyoonyesha. Inadaiwa huyu polisi aliomba lift kwenye hili basi ambalo tayari lilikuwa limeshasheheni abiria kinyume na sheria katika maeneo ya Mwidu ambapo basi la Glazia lilipata ajali hivi karibini.

Trafic.jpg


Pia angalia picha za hili ni basi la abiria la Raha Leo lenye namba za usajili T431 ARM linalofanya safari zake kati ya Dar Es Salaalam na Tanga likiwa limesheheni abiria mpaka mlangoni wakati likielekea Dar Es Salaam. Hizi picha zimechukuliwa tarehe 13 September 2011. Hili basi lingepata ajali tungeambiwa lilikuwa na abiria 65 tuu.

IMG-20110913-00232.jpg



IMG-20110913-00231.jpg



Human factor inachangia kwa kiasi kikubwa sana kutokea kwa ajali. Basi linaweza kuwa fit for purpose lakini still human factor ikasababisha ajali.
 
Kwa highway huu ni mwendo mdogo sana. Its about 50 M/h..

Kwa highway zetu hizi huu ni mwendo muafaka kabisa...
-Barabara zetu ni nyembamba
-Watumiaji wengine wa barabara (waenda kwa miguu, waendesha baiskeli, pikipiki bajaji, guta) na mifugo hukatisha hovyo barabarani hivyo kuleta hatari barabarani.
 
Kwa highway huu ni mwendo mdogo sana. Its about 50 M/h..

Ni mwendo mdogo ukilinganisha na wapi au nini? Kwa hizo barabara zetu huo ndio mwendo sahihi kabisa.

Ukienda kwa speed hiyo unapunguza kwa asilimia kubwa uwezekano wa kupata ajali.

Kama nchi za Ulaya zenye highways kubwa na zilizonyoka kwa mfano UK, maximum speed ni 70m/h, kwanini unaona 50m/h kwa Tanzania ni mwendo mdogo sana?

Wengine tukisafiri tunafuata sheria na kwenda speed karibu na hiyo. Sawa tunachelewa kufika tunakokwenda lakini pia hatuhatarishi maisha ya raia wengine bila sababu za msingi.
 
Kwa highway huu ni mwendo mdogo sana. Its about 50 M/h..
Ni mwendo mdogo kwa barabara kuu za Marekani. Lakini Barabara kuu za Tanzania hazihimili mwendo huo! Hapo ndio tunaposhindwa kuelewana manake tunafananisha maembe na mapera! Barabara nyembamba hazina maegesho ya dharura, nyingi hazina mistari ya kati na pembeni, Mitaro mikubwa haijafunikwa, curves zipo tight, etc etc ihali wahandisi watendaji wanaishia kuziita sehemu korofi, polisi wanasema madereva wazembe, magari yanetengenezwa kuendeshwa mpaka 120 MPH. Hauhitaji kujua fizikia hapa bwana!
 
Back
Top Bottom