Fizikia ya ajali (The Physics of Accidents): Mabasi yetu yanaundwa au kuunganishwa wapi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
Nimejikuta na search google na yahoo kuhusu "ajali za basi" na kuangalia picha mbalimbali za ajali. Mara moja niliona pattern fulani hiyo ambayo imenifanya niulize swali kwa wenzetu wanaojua mambo ya engineering, physics and mechanics au hata metallurgy kuhusiana na mabasi yetu. Ukiondoa vijibasi vidogo vinavyoingizwa nchini mabasi mengi makubwa na malori yanaunganishwa nchini. Mengine yanatumia chasis za malori na kuwekwa body n.k Nakumbuka kulikuwepo hata na kampuni ya "Quality Bodies" or something like that. Lakini nimeangalia kidogo ajali hizi na madhara yake na nimeanza kujiuliza kama ukiiondoa tatizo la barabara yawezekana kuna matatizo ya msingi (structural problems) kwenye mabasi yetu? Na maswali mengine yakaanza:

a. Ni chombo gani kinasimamia quality ya mabasi yanayounganishwa nchini?
b. Viwango (standards) kinachotakiwa katika mabasi ni kwa kiasi gani kimeletwa katika uelewa wa sayansi na teknolojia ya karne hii mpya?
c. Kabla mabasi hayajaingia kwenye huduma yanafanyiwa kwa kiasi gani majaribio ya kuhimili mikikimikiki (stress tests) ili kuhakikisha yatabehave vipi katika ajali maana baadhi ya mabasi ukiyaona unashindwa kuelwa kama ni impact peke yake inayosababisha madhara hivyo au hata structure ya basi haiko katika kuhimili mikikimikiki?
d. Baada ya kulaumu "mwendo kasi" mara nyingi ajali zinapotokea au "kutokufuata sheria za usalama barabarani" yawezekana kuna maelezo ya kifizikia ya ajali hizi - kwa mfano uhusiano wa mwendo, uzito na impact au nguvu (force)? Yawezekana wasomi wetu kama walivyoshindwa kuukosoa ubepari (I couldn't resist that) wameshindwa kufanya utafiti wa kisayansi wa kuelewa chanzo cha ajali hizi (badala ya kukubali tu kuwa dunia ni flat) na kuja na mapendekezo ya nini kifanyike katika uungaji wa magari, maumbo yake n.k?
e. Je muundo wetu wa barabara unachangia vipi kutokea kwa ajali hizi (kwa mfano eneo la Mikumi, Kibaha) ni kinara wa ajali kwanini?

Ninaamini kabisa kuwa na sisi tuna uwezo na wapo watu wenye uwezo wa kuangalia mambo haya kisayansi na kuyaelewa na kuja na mapendekezo ya kisayansi badala ya "kudra" na kusema ni "mapenzi ya Mungu". Anybody?

Angalia hizi picha na jiulize maswali yako na kama unamawazo ya majibu
 
Attachments

  • ajalizabasi.pdf
    657.8 KB · Views: 852

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820

Mkuu kama kuna mtu atatokea na kujibu hayo maswali basi hili tatizo la ajali litapungua sana hapa nchini. Kuna wakati nilisikia kuwa mabasi mengi yamejengewa tu bodi za mabasi ila yalistahili kuwa malori/mafuso ya kubeba mizigo. Likatolewa tamko la kwamba mwisho wa hayo malori/mafuso kutumika kama mabasi itakuwa siku fulani (nadhani imepita miaka miwili) lakini hadi sasa hayo magari yapo barabarani!! Ilimaminika kuwa hayo malori mabasi yanakuwa yamepewa mzigo mdogo kulinganisha na yanachotakiwa bubeba yakiwa malori kwa hiyo speed huwa kubwa.

Lakini pia kuna hili suala la barabara hasa design. Nasikia barabara zetu zimekuwa designed kwa kuhimili mwendo wa KM 100 kwa saa na si zaidi ya mwendo huo.
 
Lutifya

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,837
2,652
Mzee Mwanakijiji asante sana kwa post yako.Ni ukweli kuwa ajali zimeongezeka katika kiwango cha exponential rate kwa sasa hasa mabasi. Ni meguswa na topic hii hasa niliposhuhudia maongezi yasiyo rasmi ya madereva wa mabasi kwenye baa moja hivi. Kimsingi walisema pamoja na sababu ambazo umegususia ni kwambwa mabasi mengi pamoja na magari ya mizigo yanafungwa matairi toka chini ambayo kwa kweli sio imara. Matajiri wengi hawataki kufunga matairi kwa mfano aina ya michelin ambayo ni durable kwa sababu ya bei kuwa kubwa.
Chukulia mfano wa basi linalosafiri toka Dar mpaka Mbeya umbali wa karibu 840km kwa mwendo kasi wa zaidi ya 80km/hr na linasimama comfort au Al jazeera restaurant kwa dk kama 10 tu, tairi linapata moto sana kwa sababu ya friction. Tairi za kichina haziwezi kuhimili tractive force ya mwendo na umbali tajwa hapo juu tene yanafungwa mbele. Madreva hao walisema ukienda na lori la mizigo kama malawi na sourth Africa,kama gari yako imefungwa tairi ambazo sio brand inayojulikana kwa ubora kama michelin huendelei na safari.
Muhimu ni kuwa wenye mabasi wapewa na mamlaka husika kufunga tairi imara, ingawa ofcourse kuna factosr nyingi zinazosababisha ajali lakini tunaweza ku-mitigate kwa njia hiyo. Karibu ajali zilizotokea hivi karibuni za mabasi ni kwa sababu tairi za mbele zilipasuka.
Pia mabasi mengi yanayotengenezwa hapa nchini sidhani kama body zinakuwa well balanced. wenzetu kabla ya kuunda body husika wanafanyia simulation ya body assembly kwenye design software kabla ya kupeleka kwenye production ile kucheck dynamic balance.
 
Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,148
12,226
Mkuu kufikia hapa ubongo unafreeze kabisa...imefika mahala sasa nimalizapo umbali fulani safarini namshukuru Mungu "kwa sababu sijafa"...km kuna bodi ya ukaguzi basi niisifu tu kwa kuhakikisha mabasi/malori mengi ni "video coach'' hata km body ni ya plastic..thus all
 
zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,502
7,827
mmmmmh! hii nchi ya kitu kidogo, ndo maana katiba mpya iweke bayana kuwa kusiwe na urafiki kati ya wafanya biashara na serikali, tatizo kama hilo litatatulika tu.
 
Makfuhi

Senior Member
Aug 20, 2008
186
42
Nilichogundua mimi ni kwamba square pipe zimetumika ambazo ni light quality ambazo basi likipigwa kofi bodi inakatika abiria wanabaki nje. mabasi ya zamani bodi zilitengenezwa kutumia angle ndiyo maana likianguka linabaki intact. Kwa kuwa serikali yetu ilienda likizo siku nyingi ikakosa nauli ya kurudi hatuna wa kutusemea.
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,953
3,281
Mkuu MMKJJ,

Utafiti huu ulipaswa uwe umeshafanyika siku nyingi sana na pengine ungesaidia kutotufikisha hapa tulipo. Nadhani, tena nasema nadhani Sumatra na Wizara ya Mambo ya Ndani walipaswa wawe na kitengo cha utafiti wa kwanini ajali zinatokea kwa wingi? nasiyo kungoja hadi wapate maoni/ushauri na au malalamiko toka kwa raia. Serikali hii imelala fofofo!

Taasisi na mamlaka husika anzieni hapa alipoishia Mwanakijiji!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
bado sijasikia ni wapi mabasi haya yanaunganishwa na ni chombo gani kinasimamia? tuachane na ya Katiba mpya kwanza tuzungumzie right now tusije kudhania katiba mpya itatatua matatizo ya ajali au matatizo mengine yoyote yale. Kuna vitu tunaweza kuvifanya sasa hivi
 
Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,968
1,568
Au tuombe wazungu waje kutufikiria?
Naam, kwani miaka ya 60, 70 na mwanzoni mwa miaka ya 80, tulipokuwa na mabasi ya mashirika kama Kamata na Relwe, mabasi yao yalikuwa ya ubora sahihi wa barabara zetu na mengi yalikuwa yanaingia moja moja tuko huko kwao! Hata kampuni binafsi kama Kwacha, Rafiki, Bon City, n.k za miaka hiyo walikuwa na mabasi bora sana.

Hata zilipoanza Garage mbalimbali za uundaji wa mabodi, bado waliendelea kufuata standards zao. Nakumbuka garage kama ya Ujamaa na Quality walivyoweza kuunda bodi zenye kuweza kuhimili ubebaji wa abiria na mizigo ya kutosha pasipo uhatarishaji wa usalama wa abiria na basi lenyewe.

Kuja kwa garage nyingi za kuunda mabodi kunaweza kuwa ni sehemu ya matatizo haya. Siku hizi kuna mabodi toka Kenya ambayo inasemeka yana uzito mkubwa kuliko uwezo wa chasis ya basi. Kuna garage kibao bubu zinaunda mabodi yao na hata baadhi ya kampuni za mabasi zinajiundia mabodi yao. Kama ulivyodokeza hapo juu ndio maana utakuta leo hii chasis ya gari ya mizigo inatumiwa kuwa ya basi.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
bado sijasikia ni wapi mabasi haya yanaunganishwa na ni chombo gani kinasimamia? tuachane na ya Katiba mpya kwanza tuzungumzie right now tusije kudhania katiba mpya itatatua matatizo ya ajali au matatizo mengine yoyote yale. Kuna vitu tunaweza kuvifanya sasa hivi

Mabasi mengi yanaunganishwa Kenya. Msimamiaji ni SUMATRA na TBS
 
Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,968
1,568
Yawezekana ipo haja ya kuongeza mwendo kwani naamini 80k/h ni mwendo wa pole pole sana.
Mabasi mengi yanakwenda kwa speed kati ya 100km/h- 120km/h. Hiyo ya 80km/h ipo kwenye mafaili tu na imechorwa kwenye mabasi hayo. Kama unakumbuka mpango mzima wa governor ulikuwa ni kulazimisha mabasi yote yaende kwa speed ya 80km/h... Lakini umeshindikana!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
Kibunango, umenifanya nijiulize swali jingine.. what about the electronics za mabasi yetu... kuna mtu anajua ni kwa kiasi gani zimekuwa digitized?
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
Mabasi mengi yanaunganishwa Kenya. Msimamiaji ni SUMATRA na TBS

So yanapoingia Tanzania hatuna kiwango tunachotaka kuangalia; je ajali za mabasi ziko hivyo hivyo huko Kenya au ni huku kwetu au mabodi ya Kenya ni tofauti? wao Kenya kuna chombo gani kinachosimamia ubora wa mabasi? Sumatra wamepewa majukumu ya kuregulate viwanda vya mabasi au wana majukumu ya kusimamia vyombo vikiwa tayari vimekamilika na viko barabarani?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,718
28,799
Tatizo ni kubwa sio upande wa engineering tu (kama ni sababu), kuna barabara, utoaji leseni, Bima, vipuri na matairi na viongozi wasiojua nini ni tatizo. Ni combination of factors.

Miaka hiyo kulikuwa na kampuni ya Mohamed Ali ya Nairobi ndiyo ilikuwa inajenga bodi za mabasi EA nkumbuka.(Body built by Mohamed Ali & sons-Nairobi Kenya).

Nilishtuka siku moja niliposikia mabasi yanawekewa chasis za malori kubeba mzigo wa maana!! na hakuna aliyeona hicho ni kioja.

Ajali ni tatizo kubwa sana nchini ni kwa vile tu tunamsingizia mungu tu!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
Mabasi mengi yanakwenda kwa speed kati ya 100km/h- 120km/h. Hiyo ya 80km/h ipo kwenye mafaili tu na imechorwa kwenye mabasi hayo. Kama unakumbuka mpango mzima wa governor ulikuwa ni kulazimisha mabasi yote yaende kwa speed ya 80km/h... Lakini umeshindikana!

lakini hiyo ni spidi ndogo sana kwa barabara kuu.. we need to increase it.
 
Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
611
184
Mkuu Mwanakijiji, somo ulilo leta leo ni la hali ya juu sana katika fani ya uhandisi na usafirishaji.
Kwa kifupi hili ni somo katika Traffic Engineering and Management pamoja na Highway Engineering.
Ni somo ambalo halina jibu la moja kwa moja ingawaje si sababu kubwa ya madudu tunayoyaona barabarani.
Utengenezaji wa magari hasa mabasi ya abiria vile vile ni suala ambalo halijapewa ubunifu unaostahili kulingana na hali ya maendeleo ya sasa.
Kuwa basi ina chassis ya lori hiyosisababu ya basi kupata ajali.
Hebu tujikumbushe yafuatayo:
  • Kumekuwapo na a major improvement in the performance ya motor engines, engine ndogo inakuwa powerful na hivyo kubeba mzigo mzito au kwenda kasi zidi
  • Bara bara zetu hazijaendelea katika viwango kullingana na maendeleo hayo ya motor performance,Ni sehemu chache tu kamaza Chalinze-Ubena Zomozi ndio barabara zinalingana kidogo na uwezo mkubwa wa engine za kisasa.
  • Utngenezaji wa bodi za mabasi hapa Tanzania hauzingatii kabisa ubora na teknologia inayotakiwa. Hii ni licha ya mamlaka mbali mbali zilizopo katika viwango eg TBS . Kwa hapa Tanzania hata hivyo mimi sina habari kuwa kuna karakana yoyote ya serikali inayofanya research yoyote katika stress analysis kulinganana barabara zetu.
  • Kuna uchangiaji mkubwa sana kwa makosa ya binadamu katika kusababisha ajali.Aidha elimu ya usalama barabarani pamoja na ukaguzi wa ubora wa vifaa vyenyewe(magari), rushwa ya askari wa traffic na hata wasimamizi wa Tanroads mizani, vyote hivi vina mchango mkubwa sana katika ajai zinazotokea.
Mkuu Mwanakijiji topic yako ni kubwa sana na najua kiserikali haipo chini ya wizara moja tu. Hapa kuna Wizara ya Ujenzi,Mambo ya Ndani,Tawala za Mikoa nk.
Naomba kuwasilisha
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,559
1,032
bado sijasikia ni wapi mabasi haya yanaunganishwa na ni chombo gani kinasimamia? tuachane na ya Katiba mpya kwanza tuzungumzie right now tusije kudhania katiba mpya itatatua matatizo ya ajali au matatizo mengine yoyote yale. Kuna vitu tunaweza kuvifanya sasa hivi

I think Quality Garage bado wanaendelea na kuunganisha mabasi, sina uhakika kama kuna washindani wengine kwenye biashara hii...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

15 Reactions
Reply
Top Bottom