Fixed account za benki na utajiri wa haraka haraka

SAWEBOY

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
241
173
Wakuu wana JF,

Kuna tetesi kuwa ukifungua fixed account ya 10Million ktk benk za Exim, CRDB, Posta bank, NBC limited au NMB, kwa kila baada ya miezi mitatu - inazaa faidi kati ya sh. 1.8 mill up to 2.1 mil.

Hii ina maana kuwa kwa muda wa mwaka 1, yaani 12 months unakuwa umepata faida ya sh.7.2 million up to 8.4 milion

Je, hizo habari zina ukweli wowote? Kwa anayefahamu plse naomba tufahamishe na sisi ili tuweze invest soon ktk hiyo fixed account.

NB: Nimeuliza hilo coz nipo mbali kidogo, huku madongo kuinama ningekuwa jirani ningefanya follow up nije na data kamili
Asanteni,

Nawasilisha

=================
Katika benki za biashara kuna aina tatu za akaunti, kwa kiingereza zikifahamika kama ‘Savings account’, ‘Current accounts’ na ‘Fixed accounts’

Ukiachana na majina ambayo benki itaamua kuipa akaunti husika lakini huangukia katika aina hizo za akaunti. Namba moja ni akauti ya kuhifadhi pesa ambayo mara nyingi huwa na gharama za uendeshaji na hela yake hupungua kadiri inavyozidi kukaa benki

‘Current accounts’ hii ina sifa kuu ya mtu kuweza kutoa kiwango zaidi ya alichonacho katika benki husika. Mara nyingi huwa wanaziita akaunti za biashara na mwenye akaunti katika aina hii huwa na kitabu cha hawala/hundi

‘Fixed account’ hii ni aina ya akaunti ambayo inalipa mara baada ya muda wake mliokubaliana kuisha. Hii tu huweka pesa benki kwa muda fulani benki nyingi huanzia miezi mitatu, na mtu hatoruhusiwa kutoa hela kwenye akaunti yake hadi muda waliokubaliana kufika

Aina hii ya akaunti hutoa riba kwa aliyeweka hela na haina nyingi hazina makato ya uendeshaji. Aina hii ya akaunti ni moja kati ya uwekezaji mzuri kwa mtu asiyeweza kashkashi za biasahara au akiwa amepata hela ya ghafla na hajui afanyie nini

Ni sawa kuweka hela benki lakini ukiweka kwa ‘savings account’ ni sawa na kuweka mfukoni na muda wowote unaweza kuitoa, lakini ‘fixed account’ mtu hawezi kutoa hela hadi muda utimie

Ukiachilia mbali kuwa na gawio baada ya muda, akaunti hizi pia hutumika kama dhamana ya mikopo kwa taasisi mbalimbali

Signed

Oedipus
Habari ndugu,
Sasa ni hivi, kila bank inatofautiana kutokana na faidaunazoweza kupata kwa kutumia fixed accounts, pia faida inategemea kiwango chafedha na muda unaoziacha pesa zako.

Zaman niliwah kuziona za Exim Bank ilikuwani asilimia chini kidogo ya kumi. Nimejaribu kutazama kwenye web yao kabla sijakujibu itappears wameiondoa ile table iliyokuwa nayo.

USHAURI WANGU
Jaribu kutembele matawi mbali mbali ya benki, utapata maelezo mazuri na kuchagua mwenyewe. Ila kumbuka kuna kitu kinachoitwa compounding yaan tuchukue mfano Benk X wanatoa 8%per annum, then ukiweka 5mil per annum unatarajia kupata lak 4 kwa mwaka.

Hivyo basi mwaka wa pili haitakuwa 8% ya 5mil ila ni 8% ya 5.4mil ukijulisha na ile faida yako ambapo itakuwa 432,00 kwa hiyo itaendelea hivyo hadi mwaka wako watano.
Good luck with your investment, na hongera kwa kuwaza hivyo maana Fixed Deposit ni confirmed profit
 
I know bank huwa interest rate hazitofautiani sana not sure if its BOT regulating it or not.

Ila EXIM interest rate ya fixed & deposit A/C rate ni 6% kwa miezi mitatu so sijui hizo bank nyingine ulizotaja.

SO 10 million +6% = tshs 600,000 kwa miezi mitatu.

Hizo no data za ukweli toka Exim hata mimi ninayo hiyo account
 
I know bank huwa interest rate hazitofautiani sana not sure if its BOT regulating it or not.
Ila EXIM interest rate ya fixed & deposit A/C rate ni 6% kwa miezi mitatu so sijui hizo bank nyingine ulizotaja.

SO 10 million +6% = tshs 600,000 kwa miezi mitatu.

Hizo no data za ukweli toka Exim hata mimi ninayo hiyo account


Asante mkuu kwa hiyo taarifa yenye uhakika kutoka huko EXIM Bank, hopeful wadau wengine watatuhabirisha juu ya benk nyinginezo kuhusu hilo jambo.

Big up sana mkuu.
 
JAMANI WANA JF KWANZA KABISA NAOMBA MCHUKUE TAHADHARI, MARA NYINGI BANKERS HAWAKO WAZI KABISA,, YAWEZEKANA KUTOELEWA KWETU NDIO FAIDA KWAO., WANATOA/TANGAZA TAARIFA NUSUNUSU

Wakisema 6% riba ni kwa mwaka sio hiyo miezi 3 anayotaja that means 6% gawa miezi 12 zidisha miezi 3= 1.5 %
hivyo basi kwa 10,000,000 x 1.5 % = shs 150,000 tu riba utakayolipwa

Mwisho wa kipindi hicho cha miezi 3 utakuta kwenye account 10 mln + 150,000=10,150,000= tu

Utakuwa umeliwa bora hata biashara ya mkaa., sidhani hiyo riba itakusaidia kulinganisha na mtaji huo. badala yake wao watamkopesha mtu hizo pesa zako na ku-charge 18% gawa 12 x 3 =4.5% x 10 miln = shs 450,000= km ni fixed loan.,,

Kwa maelezo zaidi waweza uliza.
 
Hakuna bank inayotoa interest ya zaidi ya asilimia mbili kwenye annual fixed deposits, hizo za miezi mitatu
inategemea na treasury bills rate ziko vipi then wana qoute low.

Kwa kifupi, usitegemee faida doing business with any bank in tanzania

Nakushukuru kwa kutoa neno lenye ukweli na lisilojulikana. Tz banks are the enemies of trade developments tunakwenda kwasababu tu hatuna namna ya kufanya, hata Olosugun Obasanjo aliwahi kusema kwamba in tz at a loan interest rate of 19% hata mfanyabiashara wa madawa ya kulevya hapati faida kubwa kama hii, bank zinatukandamiza sana
 
Ukiwekeza kwangu kila mwezi nitakupatia TShs laki 6 monthly. so kwa miezi mitatu ni million 1 na laki nane, kwa mwaka ni million 7 na laki mbili, but tunaingia mkataba wa miezi mitatu mitatu renewable.

If you ARE interested ni PM for More clarifications
 
nakushukuru kwa kutoa neno lenye ukweli na lisilojulikana .... tz banks are the enemies of trade developments tunakwenda kwasababu tu hatuna namna ya kufanya ..... hata Olosugun Obasanjo aliwahi kusema kwamba in tz at a loan interest rate of 19% hata mfanyabiashara wa madawa ya kulevya hapati faida kubwa kama hii .... bank zinatukandamiza sana

Na mbaya zaidi hata BoT wamenyamaza tu wakiangalia wa-TZ wanavyosurubiwa na hayo mabenki! Sijui wako kwa faida ya nani?
 
I know bank huwa interest rate hazitofautiani sana not sure if its BOT regulating it or not.
Ila EXIM interest rate ya fixed & deposit A/C rate ni 6% kwa miezi mitatu so sijui hizo bank nyingine ulizotaja.

SO 10 million +6% = tshs 600,000 kwa miezi mitatu.

Hizo no data za ukweli toka Exim hata mimi ninayo hiyo account

Mkuu,
Hesabu zangu zinaonyesha kwamba for 10M @6% annual rate, for 3months period utapata 150,000 na siyo 600,000/- kama ulivyoonyesha hapo juu.
I stand to be corrected

Thanks
 
Hakuna hicho kitu. Mbona wengi tungeacha kuhangaika tungewekeza katika fixed deposits tu! Hizo asilimia zinazotajwa ni kwa mwaka.​
 
This thread is very interesting - Tz Banks do charge transaction fees for ATM withdrawals/transactions. What ashame!

Withdrawals were supposed to be free because I draw my own money which bankers lend at interest when they are idle.


I suggest consumer pressure groups to start acting on this- it is not fair charges in the face of global competitions. Where is BOT?!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom