FITNA uwanja wa ndege wa DAR

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
HABARI ZA LEO BWANA MICHUZI,
SISI WAFANYAKAZI WA UWANJA WA NDEGE WA NYERERE TB II TUNA MALAMIKO AMA MA DUKU DUKU YALIYOJAA NA TUMEONA LEO TUWEKE WAZI ILI ANGALAU IJULIKANE NINI KINACHOENDELEA.

MICHUZI WEWE NI FREQUENTLY FLYER UNATUMIA SANA UWANJA HUU. NADHANI UNAKUMBUKA KUWA MWANZONI OFISI ZOTE ZA TICKETING, BUREAU DE CHANGE ZOTE ZILIKUWA NDANI, THEN MWAKA JANA MWISHONI TULIFUKUZWA KAMA MBWA TUKATOLEWA NJE ETI KWA AJILI YA KIUSALAMA NA KULIKUWA NA UJIO WA NAIBU WAZIRI MAMA MAUA DAFTARI. WATU HATUKULALA,MAFUNDI WALIKESHA KUTWA KWA UJENZI NA KUPAKA RANGI KUTA,HII INAONYESHA NI JINSI GANI HAWANA MPANGILIO NA MAMBO YAO.

TULIKUBALI NA TUKAVUMILIA.SASA IKAJA SEHEMU YA KUPEWA VITAMBULISHO VYA AIRPORT,WAFANYAKAZI WOTE WA NJE TUMEPEWA VITAMBULISHO VYA KUISHIA UTAWALA NA SI KWINGINEKO,NA BEI WALIYO CHARGE TZS 20,000/= NI SAWA NA VYA WAFANYAKAZI WENGINE. HII HAIJATULIA KWA KWELI.

SASA MALALAMIKO YETU NI KUWA KUNA BUREAU INAITWA GALAXY INAMILIKIWA NA DADA RAIA WA ASIA, RESHMA DOSSA, IKO NJE. LAKINI GHAFLA JUZI WAMEMPATIA TENA NAFASI NYINGINE NDANI KWA AJILI YA KUFUNGUA BUREUA NA HILI LIKO WAZI KIBANDA KIPO NA KIMEANZA KU OPERATE JANA. SASA MWENZETU ANA MILIKI OFISI MBILI NJE NA NDANI NA ANA KITAMBULISHO CHA KUMRUHUSU KUINIGA NDANI.NA KULIKUWA NA MKUTANO SUALA HILI HALIKUWEPO; SASA KULIKONI??? NDIO HAYA MAMBO AMBAYO RAIS HATAKI KUYAFUMBIA MACHO.

NANUKUUU WARAKA ULIOTUMWA KWETU WOTE WAFANYAKAZI BAADA YA KULIONA HILI.
KULIKONI????
10FEB 2008.
MKURUGENZI WA UWANJA UNALITAMBUA HILI??RAIS NJOO USAFISHE NA AIRPORT.HAKI SAWA KWA WOTE.

KWA NINI GALAXY BUREAU (RESHMA) IWE TENA NDANI?? BASI NA VIBANDA VYOTE VYA NJE VIRUDISHWA NDANI AMA TUPEWE VITAMBULISHO VYA KUINGIA NDANI. HII SIO HAKI NA SI HALALI.( NDIO UFISADI HUU) NINI KINACHOENDELEA HAPO?? BASI HATA IMALASEKO BUREAU WANA HAKI YA KUPEWA.
KULIKONI???????TUNAHITAJI MKUTANO NA VIONGOZI WA UWANJA TENA KWANI HILI SUALA HALIKUWEPO MWANZO.

BY WAFANYAKAZI WA OFISI ZA NJE.

UKIMWI UTUUE NA MAFISADI PIA!!!!!!

KWA KWELI INABIDI RAIS AKIMALIZA YA HUKO ATUME WATU WAKE WAJE WACHUNGUZE NA HUKU ,KUNA BAADHI YA VIONGOZI WAKO MUDA MREFU ILA HAWATAMBUI WAJIBU WAO,NA TUMEWACHOKA .TAA INAHITAJI MABADILIKO SANA,RE SHUFFLE ....TUMECHOKA KUONA SURA HIZO HIZO AMBAZO HAZINA UFANISI WA KAZI,WANAPANDA NA KUSHUKA NGAZI ZA UTAWALA TU,CHAI ZA FLAMINGO CAFETERIA NA SOGA MA OFISINI LAKINI HAKUNA KINACHOFANYIKA.UWANJA UNAVUJA MAJI OVYO,MVUA IKINYESHA UPANDE WA ARRIVAL WATU HAWAWEZI KUPOKEA NDUGU/JAMAA ZAO.,SASA WANAACHA KUSHUGHULIKIA VITU KAMA HIVI WANAHANGAIKA NA MAMBO MENGINE..

-TUNA MENGI YA KUONGEA,TUNAOMBA SUALA HILI ULIFIKISHE MAHALI PAKE.ASANTE SANA LIFANYIE KAZI,UFISADI UKO KILA KONA ILA SI HUUU WA MACHO MACHO NAMNA HII....TUMECHOKA.

source: michuzi blog
 
Ule usemi wa kila mtu na karichmondi kake. Sasa ni wakati wa kila mtu kuaanza kuongea openly bila kujali ili serikali isikie na kuchukua hatua stahiki.
 
Dr Who,

Unaitwa kule kwa Membe na Lowassa ukajibu tuhuma mbona umekimbia? acha kukimbia nenda kajibu hoja kule! kwi kwi kwiii

Ama kweli pale uliparamia mkuki kwa mbele au ulidandia treni kwa mbele kwi kwi kwiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Ulichosema Game Theory ni kweli kabisa. Mimi na familia yangu tumetoka likizo TZ hivi karibuni, na hali tuloikuta kwa kweli pale Uwanja wa Ndege ilikuwa ni ya kusikitisha. Naomba msinielewe vibaya maana kuna wengine wanoweza kudhani nina nyodo, kasumba, etc. lakini jamani kwa nini kuwepo na yafuatayo....?

1. Escalator zisizofanya kazi.
2. Pale arrival/luggage claim lounge ni mtafutano. Yaani ni JOTO, na msongamano wa watu. KWA NINI PASIPANULIWE? KWA NINI WASITENGENEZE AC? (HVAC Systems). Ninasema hivi kwa sababu ninajua kwamba VIP lounge ina AC ambayo ni operational. Kwa nini wasisambaze teh same system kwenye departure and arrival lounges???
3. Kuna wafanyakazi wengi sana sana walikuwa wanazunguka tu, hata sikuona walichokuwa wakifanya kwa kusema ukweli. Ni kama mwana JF alivyosema hapo juu...soga tu! Yaani nadhani idadi ya wafanyakazi ilikuwa ni sambamba na wageni walioko pale arrival lounge.

Haya mambo yetu TZ ya watu na viongozi kushikilia madaraka miaka nenda miaka rudi inatu-cost sana. Oneni what happened to ATC...mambo ya ajabu tu.

Sasa tunasema tunataka kuitangaza Tanzania nje ili watalii watembelee vivutio mbalimbali vya nchini. sasa wakija wapokelewa na hali ya ajabu pale airport, si itatumalizia biashara jamani?

Wana JF tuamke na tuvalie njuga hili swala la Airport ya Dar. Tukumbuke kwamba A FIRST IMPRESSION is always remebered. Mfano mzuri ni kama ukitegemea wageni nyumbani kwako, si unapanga vitu na kufanya usafi zaidi ya siku nyingine zote? Sasa tunategemea watalii na wageni kutoka nchi mbalimbali duniani. Wouldn't we rather make a GOOD FIRST IMPRESSION to our guests right at the front door? And that front door, ladies and gentlemen is THE JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT.

Wake up TAA!
 
Leo mmenikumbusha kisa cha Air hostes mmoja jina ninalo na nitalitoa mkitaka tarehe ,na ndege namba alizua kizaaa zaa na kusababisha polisi kumweka abiria chini ya Ulinzi kisa ni Mkenya kasema ukweli kwamba Ndege iko angani for more than saa moja bado kuna joto kama uko nje .Kila mmoja alikuwa ana sweat ila Watanzania ni wapole wakauchuna .Mkenya aliwaka but bila violence act.Maajabu wakagawa refreshments wakamnyima kisa kasena openly na kufika uwanjani wakamwitia security jamaa akaishia lupango . Ndege zima wakawaka lakini wakaondoka na kumwacha kijana .Nikaona hakuna maana nikajitosa nikahoji uhalali wa tukio lile .Captain na wengine wakasema amemtukana mdada yule mimi nikasema no si kweli . Wakakomaa na mimi nikakomaa nikasema nataka twende Mahakamani na jamaa nampa dhamana then tutaonana . Baada ya kuona hilo waka back off polisi na watumishi wengine wakasema openly kwamba watu wanaonewa na kwamba precision air ina matatizo kila siku abiiri na watumishi wao polisi . Leo mnasema haya basi kuna serius problem pale uwanjani . From now nitakuwa macho nikifika pale .
 
Bila shaka hayo ni matokeo ya maandalizi ya ujio wa Kichaka. Poleni wote mnaoathirika.

Yunic, pamoja na matatizo hayo uliyoyaorodhesha hapo, ambayo yote ni kweli tupu; bahati yako nzuri ni kwamba haikukulazimu kwenda msalani kwenye mojawapo ya vyoo vilivyopo hapo. Si ajabu ungepata ugonjwa wa kutapika bila kutegemea.

Sasa fikiria 'shock' anayoweza kuipata mtu anayeona hali kama hiyo kwa mara yake ya kwanza maishani!

Mambo mengi sehemu mbalimbali maofisini yanatokana na utendaji mbaya wa kazi tu, na sio kwamba ni kwa sababu ya ukosefu wa nyenzo. Na tunaposema sisi ni maskini, umaskini wetu mwingi unasababishwa na tabia zetu mbovu.
 
Nimekubali kabisa maneno yako ndugu Kalamu
 
-----------------------------------------------------------------
Well said ndugu kalamu. kama unavyosema sikuhitaji kwenda msalani, lakini nilihisi kutakuwa na vitu vya ajabu tu huko...maji yenyewe yatoke wapi?

Umasikini wetu ni wa tabia tu. Na uzuri au ubaya wetu waTanzania ni kwamba we are very peaceful people, hatutaki kuwa over agressive na tunachukulia mambo mengi tu kama yalivyo. Kwa maneno mengine ni kwamba kama sisi tungekuwa tunadai UBORA NA/AU KIWANGO CHA JUU KAMA HAKI YETU naona mambo mengi na viongozi wetu popote pale wangejirekebisha. Hivi unajua hata ukiomba risiti dukani mtu anakushangaa? He he he!
 
Leo mmenikumbusha kisa cha Air hostes mmoja jina ninalo na nitalitoa mkitaka tarehe ,na ndege namba alizua kizaaa zaa na kusababisha polisi kumweka abiria chini ya Ulinzi kisa ni Mkenya kasema ukweli kwamba Ndege iko angani for more than saa moja bado kuna joto kama uko nje .Kila mmoja alikuwa ana sweat ila Watanzania ni wapole wakauchuna .Mkenya aliwaka but bila violence act.Maajabu wakagawa refreshments wakamnyima kisa kasena openly na kufika uwanjani wakamwitia security jamaa akaishia lupango . Ndege zima wakawaka lakini wakaondoka na kumwacha kijana .Nikaona hakuna maana nikajitosa nikahoji uhalali wa tukio lile .Captain na wengine wakasema amemtukana mdada yule mimi nikasema no si kweli . Wakakomaa na mimi nikakomaa nikasema nataka twende Mahakamani na jamaa nampa dhamana then tutaonana . Baada ya kuona hilo waka back off polisi na watumishi wengine wakasema openly kwamba watu wanaonewa na kwamba precision air ina matatizo kila siku abiiri na watumishi wao polisi . Leo mnasema haya basi kuna serius problem pale uwanjani . From now nitakuwa macho nikifika pale .

-----------------------------------------------------------------

Jamani mambo hayo ya ajabu. Sasa hawa precision Air si watakosa wateja jamani? Ni yale yale.....We need to demand QUALITY CUSTOMER SERVICE as our right!
 
Sasa huyu Rais sijui atatua mangapi, ina maana watz hawaamini mtu mwingine kumaliza kero zao hadi JK? Watz inabidi tubadilike kidogo, mambo mengine ni simple sasa, kama hili sio issue kabisa kama hawa jamaa hawana woga, ni swala la ku-deal na boss wa hapo uwanjani tu wala halihitaji hata mkurugenzi wa mawasiliano, achalia mbali waziri au Rais. Guys play your part, sio kulialia! Mwishowe mtataka JK aje kuweka sawa hata ndoa zenu!
 
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni; kwenye Kitengo cha ukaguzi wa mizigo ni karaha tupu kama siyo wizi wa mchana. Nilishuhudia watu wengine wakinyanganywa Dawa za Miswaki, Mafuta ya kupaka kwenye final check eti kwa sababu hairuhusiwi kuingia na vitu kama hivyo vyenye kuzidi gramu 100 vikiwa ndani ya Hand-luggage. Maajabu ni kwamba unakuta kwenye ukaguzi wa mwanzo waliviona,badala ya kumshauri Msafiri aviweke kwenye mzigo unaopimwa, wao huuchuna na kusubiri kwenye final check ambapo msafiri hana choice zaidi ya ku-surrender ndipo huambiwa vitu hivyo haviruhusiwi na hivyo huvitaifisha kwa maelezo kuwa wanakwenda kuvichoma. Kwa kweli tabia hii ime-disappoint abiria wengi sana.
 
Mugo"The Great";141528 said:

Haya yote ni sehemu ya uzembe tulionao waTanzania.

Ni jambo ambalo ni rahisi kabisa kuwatangazia, au kuweka matangazo yaliyo wazi kwa wasafiri wote wa ndege ili wajue ni vitu gani visivyoruhusiwa kuwemo kwenye 'hand luggage'.
Huu ni utaratibu sehemu nyingi duniani, hasa hayo mabadiliko yanapoanza kutumika.

Wakishatangaza hivyo, basi wasafiri wanaoendelea kuwa na vitu hivyo, kwa kutokuwa makini au kwa kukaidi wajilaumu wenyewe kwa kutozingatia utaratibu mpya. Kosa la watu wetu ni kuwavamia au kuwategea watu bila ya kuwataarifu mapema.
 
Bila shaka hayo ni matokeo ya maandalizi ya ujio wa Kichaka. Poleni wote mnaoathirika.

Yunic, pamoja na matatizo hayo uliyoyaorodhesha hapo, ambayo yote ni kweli tupu; bahati yako nzuri ni kwamba haikukulazimu kwenda msalani kwenye mojawapo ya vyoo vilivyopo hapo. Si ajabu ungepata ugonjwa wa kutapika bila kutegemea.

Sasa fikiria 'shock' anayoweza kuipata mtu anayeona hali kama hiyo kwa mara yake ya kwanza maishani![/B]

Are you serious?
Mara ya mwisho mlipita lini pale?
Jamani mbona vyoo viko vizuri tu? mbona huko majuu mnakokusifia na sometimes vyoo vyao vinakuwa haviko sawa! Tatizo ni nini? miundombinu au usafi?
 
Haya yote ni sehemu ya uzembe tulionao waTanzania.

Ni jambo ambalo ni rahisi kabisa kuwatangazia, au kuweka matangazo yaliyo wazi kwa wasafiri wote wa ndege ili wajue ni vitu gani visivyoruhusiwa kuwemo kwenye 'hand luggage'.
Huu ni utaratibu sehemu nyingi duniani, hasa hayo mabadiliko yanapoanza kutumika. Wakishatangaza hivyo, basi wasafiri wanaoendelea kuwa na vitu hivyo, kwa kutokuwa makini au kwa kukaidi wajilaumu wenyewe kwa kutozingatia utaratibu mpya. Kosa la watu wetu ni kuwavamia au kuwategea watu bila ya kuwataarifu mapema.
Unajua saa nyingine abiria sisi tu wakaidi, na inapokuwa tunakaexperience ka kusafiri mara kwa mara.
Mara ya mwisho nilipita pale JK, na kulikuwa na katangazo japokuwa kwa waliowageni si rahisi kukaelewa kanamaanisha nini, na mimi nakumbuka kuna dada aliniuliza na kama na liquid n. akanipa mifuko (ya plastiki ya kuseal)
ila kunawengine hawakusikia, au nikutokuelewa tulipofika kwenye connection nyingine (Amterdam) hawakukatisha na chupa zao za konyagi na mafuta ya karafuu waliyokuwa wamebeba.
Saa nyingine tuandike uhalisia sio hisia.
 
Domestoc flights kuna wakati mmoja nimeshuhudia mtoto wa shule anaacha butter yake ya mkate alilia hadi mwisho kisa hawezi kuingia nayo ndani ya ndege .Vipi nalo hili ?
 
Mimi kinachoniudhi ni wale maafisa wa uhamiaji collar za mashati yao nyeusi na ni wachafu kweli hawa ndio watu wa mwanzo mgeni/mtalii akiingia ndani ya nchi anakutana nao.

Halafu wanafanyakazi as if walikuwa night shift mtu anajikongoja kama expectant grand mother vile, Tanzanian passport holder anahudumia kwa muda wa nusu saa! imagine someone ametoka kwenye flight ya usiku kama ya BA over 8 hours then anakuja spend more than 2 hours on the ground kuanzia urasimu wa immigration, mizigo, customs nk in a very unpleasant atmosphere hot, bad smell, staff jeuri etc.
 
Mimi kinachoniudhi ni wale maafisa wa uhamiaji collar za mashati yao nyeusi na ni wachafu kweli hawa ndio watu wa mwanzo mgeni/mtalii akiingia ndani ya nchi anakutana nao.

Halafu wanafanyakazi as if walikuwa night shift mtu anajikongoja kama expectant grand mother vile, Tanzanian passport holder anahudumia kwa muda wa nusu saa! imagine someone ametoka kwenye flight ya usiku kama ya BA over hours then anakuja spend more than 2 hours on the ground kuanzia urasimu wa immigration, mizigo, customs nk in a very unpleasant atmosphere hot, bad smell, staff jeuri etc.

Ndiyo Mzee Masatu .Umsema kweli kabisa .Napita hapo karibia kila wiki naona shida hizo domestic flights zina ujinga mwiiiiiiiiiiiiiiiingi .
 
Sasa huyu Rais sijui atatua mangapi, ina maana watz hawaamini mtu mwingine kumaliza kero zao hadi JK? Watz inabidi tubadilike kidogo, mambo mengine ni simple sasa, kama hili sio issue kabisa kama hawa jamaa hawana woga, ni swala la ku-deal na boss wa hapo uwanjani tu wala halihitaji hata mkurugenzi wa mawasiliano, achalia mbali waziri au Rais. Guys play your part, sio kulialia! Mwishowe mtataka JK aje kuweka sawa hata ndoa zenu!

Watu wanapomlilia JK nafikiri hawana kosa. Kwa system ya Tanzania imewafanya wananchi wamtegee Rais kati kutatua matatizo yao. Imagine kama Rais ana-appoint Directors wote kwenye parastals na serikalini, Mawaziri, Wakuu wa mikoa na Wilaya etc. Sasa kama kazi haziendi vizuri kwenye mashirika then inabidi wamgeukie yule mkuu aliyewachagua. Actually hii system inawapunguzia sana nguvu kidogo Mawaziri na Makatibu wakuu kwa vile wote ni wao pia ni presidential appointees.
 
Mimi kinachoniudhi ni wale maafisa wa uhamiaji collar za mashati yao nyeusi na ni wachafu kweli hawa ndio watu wa mwanzo mgeni/mtalii akiingia ndani ya nchi anakutana nao.

Halafu wanafanyakazi as if walikuwa night shift mtu anajikongoja kama expectant grand mother vile, Tanzanian passport holder anahudumia kwa muda wa nusu saa! imagine someone ametoka kwenye flight ya usiku kama ya BA over 8 hours then anakuja spend more than 2 hours on the ground kuanzia urasimu wa immigration, mizigo, customs nk in a very unpleasant atmosphere hot, bad smell, staff jeuri etc.

Sasa kama serikali inawapa mashati mawili halafu wanategemea usafiri wa daladala, hivi kweli unategemea watafika kazini wasafi ukichukulia joto na humidity ya bongo??? WaTanzania kwa ujumla wanajipenda na ni watanashati. Sema uwezo ni mdogotu!!!!!
 
Jamani Mr. Zero,

Kupewa mashati mawili sio hoja, maana mfano wanafunzi wengi wako kwenye situation kama hiyo, lakini ni watanashati tu. Na kwa wafanyakazi mie naona mambo ni rahisi zaidi. Wafanyakazi wanaweza kubadilishia shati au uniform zake kazini au siyo? Kwa hiyo swala la kuchafuka shati kwenye daladala linaweza kuchangia kwa upande mmoja, lakini solution hapo si ni kufua tu shati kila siku?
 
Back
Top Bottom