Fitna kwangu mwiko - Ukweli ni kwamba siasa safi nchi hii zilikufa na TANU mwaka 1977

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Hili limekuwa wito wangu tena na tena bila kuchoka nikiwaasa watu kuhusu siasa zetu hizi. Nimekuwa nikisema mambo mengi ncho hii hayaendi kwa sababu kama taifa huwa hatufanyi maamuzi ya dhati. Mfumo wa vyama vingi ni mmoja wapo. Tumeukubali kishingo upande tu.

Inasikitisha tunatumia rasilimali nyingi za taifa kwa kitu ambacho hakitusaidii kwa sababu tumekikubali kinafiki tu lakini mioyo yetu haipo huko. Inasikitisha sana!

Binafsi nadhani CCM ilikuja kwa sababu kipindi kile hali ya kisiasa ya Zanzibar ililazimu. Haikuwa long-term plan ya Mwalimu ndiyo maana hakuwahi kuvaa jezi zao hata mara moja. Ila ndiyo hivyo tena, mambo yakawa mambo.

Ushauri wangu kwa watu wa kitengo, Tutengeneezeni basi hata chama cha pili tuwe na vyama angalau viwili vitakavyokuwa vinabadilishana madaraka hata kama ni kiini macho tu, roho zetu zitulie. Mbona kuna nchi wamefanya hivyo na maisha yanaendelea? Mnaweza, jiongezeni kidogo.

Hii michezo inayochezwa kwa maisha ya watanzania huku fedha na muda mwingi wa Watanzania vinapotea bure, havimnufaishi yeyote, hata hao wanaoshangilia.
 
  • Thanks
Reactions: Hey
IMG-20190301-WA0033.jpg
 
Back
Top Bottom