Fitna, gharama za barabara vyamchefua Rais Magufuli

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
USIMAMIZI duni unaofanywa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kwa mkandarasi anayejenga Barabara ya Mpemba-Isongole pamoja na kitendo cha Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene, kumshitaki Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kwake, kimemkera Rais John Magufuli na kutoa maagizo mazito hadharani.

Rais Magufuli yuko mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, aliweka jiwe la msingi wa marabara ya Mpemba-Isongole yenye urefu wa kilomea 50.3 inayojengwa kwa fedha za serikali Sh bilioni 109. Kitendo cha mkandarasi anayejenga barabara hiyo kusuasua tangu mwaka 2017 huku Wizara na Tanroads wakikaa kimya bila kumchukulia hatua yoyote kimemkasirisha Rais Magufuli na kuwaagiza kuanzia sasa wamsimamie ili afanye kazi usiku na mchana na akishindwa wamfukuze.

Alisema barabara hiyo ilitakiwa iwe imeshakamilika tangu mwezi Agosti mwaka huu lakini kutokana na uzembe wa mkandarasi imeshindikana.

Kitu kingine kilichomchukiza Magufuli ni barabara hiyo kujengwa kwa gharama ya Sh bilioni mbili kwa kilometa moja na kumtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe asimwite tena kuweka jiwe la msingi au kufungua barabara iliyojengwa kwa gharama kubwa namna hiyo.

Akerwa na uchongezi Baada ya Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene kupewa nafasi ya kuzungumza, alitumia nafasi hiyo kumshitaki Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa amekuwa kikwazo kwa shughuli za maendeleo wilayani humo. Kauli hiyo ya Mbunge ilimkera Rais na kusema kuwa hana hakika kama kweli madhambi yote yaliyosemwa na mbunge huyo kuhusu mkurugenzi ni ya kweli. “Simtoi huyu Mkurugenzi mpaka nipate taarifa kutoka kwa vyanzo vyangu, taarifa nilizonazo siyo hizi zilizosemwa hapa, taarifa nilizonazo mpaka sasa hakuna ubaya alioufanya, viongozi acheni kuchongeana, uongozi ni pamoja na kuvumiliana,” alisema.
 
Safi kabisa kwa kumuumbua huyo Janet Mbenne na kiherehere chake! Mh Rais kemea majungu manake majungu hayajengi bali yanabomoa. Usijekuta Mbunge alienda kuhemea kwa Mkurugenzi akanyimwa basi akajenga bifu. Mbunge ameshindwa kushirikisha mamlaka ya Mkoa hadi aseme kwa Mh Rais? Wacha aumbuliwe.

Hili la Mh Rais kusema asiitwe tena kwenye barabara zenye gharama kubwa naona ni mara ya pili kulisema hadharani. Nakumbuka kwenye ziara yake kule Mtwara, Ruvuma na Njombe alilisema hili. Sasa inabidi Eng Kamwelwe akae sawa na watu wake wa Tanroads vinginevyo chochote kinaweza kutokea wakati wowote; amina.
 
Back
Top Bottom