Fitina CHADEMA

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
147
Mwandishi wetu, Kigoma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,amezua jambo jingine kwenye chama chake cha Chadema baada ya kueleza kuwa kelele zote ndani ya chama hicho, zinatokana na fitina ambazo zimejengwa baada ya kutangaza kuwa mwaka 2015 atagombea nafasi kubwa kwenye uchaguzi mkuu.Zitto, ambaye alijipatia umaarufu katika Bunge la Tisa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, ndio kwanza ametoka kwenye mgogoro na wabunge wenzake baada ya kutofautiana na uamuzi wao wa kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kuhutubia ili kutuma ujumbe wa msimamo wa chama wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais.

Kabla ya uchaguzi, Zitto alisababisha kizaazaa baada ya kutangaza kugombea uenyekiti wa Chadema katika kipindi ambacho chama hicho kilionekana kutaka mwenyekiti wake wa sasa, Freeman Mbowe aendeleze kazi ya kukijenga chama.
Zitto pia alitofautiana na viongozi wenzake baada ya kutamka hadharani kuwa haungi mkono uamuzi wa katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wa kuwaachisha kazi wafanyakazi wawili kwenye ofisi ya makao makuu ya chama hicho kwa tuhuma za kuvujisha siri.

Tamko lake kwenye mkutano wa hadhara aliouitisha kwenye Uwanja wa Cine Atlas mjini Kigoma juzi unaonekana kukaribisha mgogoro mwingine baina yake na wanachama wenzake baada ya kutuhumu kuwepo na njama dhidi yake kutokana na nia ya kugombea urais mwaka 2015 baada ya Dk Slaa kuzoa kura nyingi katika uchaguzi wa mwaka huu alipogombea nafasi hiyo.
Zitto, ambaye katika siku za karibuni amekuwa akitofautiana na wanachama wenzake kiasi cha kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika uongozi wa kambi ya upinzani bungeni, alisema hayo juzi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika eneo la Cine-Atlas lililo Ujiji mjini Kigoma.

Zitto aliuambia mkutano wa hadhara kuwa kelele zote ndani ya Chadema zimetokana na fitina zinazotengenezwa dhidi yake kwa kuwa kuna uwezekano kwake wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
"Baada ya uchaguzi kumalizika, watu sasa wanajipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine. Kuna watu wanaotaka nihame Chadema kwa kuwa wananiona ni kikwazo kwao, lakini nasema siwezi kuhama kwa kuwa nina mtazamo wa mbele wa kugombea urais," alisema Zitto.

"Kigoma inaweza kumtoa rais ingawa watu wanasema haiwezekani kwa sababu ni mwisho wa reli (ya Kati). Nasema siwezi kufanya makosa ya kuhama kama walivyofanya walionitangulia na wakapoteza dira.
"Kingine najua mtakuwa mmesikia mengi kupitia vyombo vya habari, lakini nataka niwaeleze kwamba sikulishwa sumu na hakuna anayeweza kunipa sumu."
Mbunge huyo ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chadema, aliongeza kusema: "Mimi sing’oki Chadema kamwe na wale wanaotaka nitoke basi waanze wao. Kwa sababu, chama hiki ni chetu. Watu waliteswa, walifungwa jela, hata kupigwa na polisi na kuumizwa kwa ajili ya Chadema. Nasema siwezi kukimbia hata mara moja."

Alisema baadhi ya watu wa Kigoma waliokuwa viongozi wa Chadema na kuamua kukimbilia CCM baada ya kutokea mifarakano ndani ya chama hicho, wamejikuta wakipata aibu kwa kupoteza heshima mkoani Kigoma.
Alisema viongozi hao licha ya kukimbilia CCM, bado mkoa huo haujapiga hatua yoyote kubwa ya kimaendeleo jambo linaloonyesha kwamba maendeleo hayaletwi na chama bali ni juhudi na mikakati ya viongozi kwa kushirikiana na wananchi katika kuibua miradi, kuisimamia na kuitunza kwa faida ya Jamii.

Zitto alibainisha kuwa migogoro yote inayoonekana Chadema ni mchakato wa kidemokrasia lakini kwa ujumla mambo ni shwari ndani ya chama hicho.
"Ndugu zangu nataka niwaambie kwamba, kwa kawaida, baada ya uchaguzi mmoja, watu hujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao. Sasa haya mnayoyasikia ni mchakato wa kidemokrasia tu ndani ya Chadema, lakini kwa ujumla mambo ni shwari," alisema.

Zitto ametoa kauli hiyo takriban majuma mawili tangu alieleza gazeti hili kuwa ameamua kutozungumzia masuala ya chama chake kwa kuwa ameona kufanya hivyo ni kuchochea migogoro.
Zitto alikuwa ametakiwa kutoa msimamo wake baada ya kamati kuu ya Chadema kukataa kuidhinisha uamuzi wa wabunge wa chama hicho kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye na kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kupima mwenyewe uzito wa kitendo hicho cha wabunge wenzake.
 
sasa zitto,kuliko kukigawa chama si bora uondoke tu..!!hiyo nafasi ya juu ipo kila chama.nenda2.wewe ni doa cdm.
 
Zitto ni kiongozi wa chama na mbunge. Anayo kila haki ya kukutana na wananchi na kubadilishana nao mawazo. Lakini pia wananchi wanayo kila haki ya kujua kiongozi na mbunge wao anakuwa anaongea nini na adui namba moja wa nchi yao Rostam usiku wa manane. Tafadhali Zitto tujulishe mlikuwa mnapanga nini, vinginevyo wale walionasa mawasiliano waweke hadharani mawasiliano hayo yalihusu nini, isijekuwa ndiye rais tunayeandaliwa na Rostam.
 
Huyu dogo ana umri gani mpaka aseme ana mpango wa kugombea uraisi 2015 kulingana na katiba ( ya sasa) au ndio kusema hajui anenalo!
 
Huyu dogo ana umri gani mpaka aseme ana mpango wa kugombea uraisi 2015 kulingana na katiba ( ya sasa) au ndio kusema hajui anenalo!


Katiba gani ambayo unaizungumzia wewe? hujui kwamba uchaguzi ujao utakuwa na katiba mpya.
 
Zito hawezi kukigawa chama hata kidogo ila aache kuwasikiliza mafisadi awe anafanya kazi kwa matakwa ya wananchi na chama chake.
 
CHADEMA, just ignore this boy Zitto Kabwe completely. Everybody NOW understands him better than anything else.

Wana-JF, keep suchlike threads about this politician called Zito Kabwe. It more than enough of him in our ears every other day.

Zitto, take a rest now it will so good for you.
 
Zitto ndio kiongozi bora tunamuunga mkono 100% achana na hao wanaokusumbua hiki ni chama cha wananchi sio wachagga au watu wa kaskazini tu hata sisi wa kusini tuna haki na chama.
Uchaguzi ujao chukua form ya uenyekiti utapata tu.
Achana na hao mafisadi katika chama huyo mbowe na slaa wake.
 
Huyu dogo ana umri gani mpaka aseme ana mpango wa kugombea uraisi 2015 kulingana na katiba ( ya sasa) au ndio kusema hajui anenalo!
kwa sasa anamiaka 34 after 5 yrs wil b 39 au watamfyatulia bc ya kuongeza miaka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom