Fisadi ni mtu gani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
FISADI NI MTU GANI?

Barazani naingia, wakijiji nasalimu,
Swali nalipangilia, mkanijuze walimu,
Hili ninaulizia, kwenu ninyi watalaamu,
Fisadi ni mtu gani, mimi ninaulizia.

Neno hili la fisadi, sasa lazidi tangaa,
Limekuja bila hodi, kila kona lasambaa,
Kama tungetoza kodi, "vijisenti" vingejaa,
Fisadi ni mtu gani, nauliza Tanzania.

Fisadi sifaze zipi, naombe mzichambue,
Zimekaa vyepivyepi, wananchi tutambue,
Tukwepe kama makapi, fisadi tuwagundue,
Fisadi ni mtu gani, kujua ni yangu nia!

Kila aliye muizi, huyo naye ni fisadi?
Kila mtu mdokozi, naye aibebe kadi,
Hata yule mchokozi, naye mtu mkaidi,
Fisadi ni mtu gani, nani ataniambia!

Aliye mbadhirifu, kwenye ofisi za umma?
Ajiona mtukufu, ni mvivu kujituma,
Apenda umaarufu, asiyejali dhuluma,
Fisadi ni mtu gani, mchango naulizia!

Asiyependa shauri, mgumu kushaurika,
Kutwa ni mtu wa shari, hapendi kukosoleka,
Anofura kwa jeuri, na ndita imekunjika,
Fisadi ni mtu gani, mashaka yameingia!

Lazima wa serikali, au hata mitaani,
Hili ndilo langu swali, kazini au sokoni,
Karamagi na Balali, sifa zao ndio nini,
Fisadi ni mtu gani, jasho linanishukia!

Mwenye kutumia ngono, kupata akitakacho,
Kutwa atazama porno, tumpe na cheo hicho,
Huyu fisadi wa ngono, au mpaka awe nacho?
Fisadi ni mtu gani, wakijiji ninalia.

Tumewaita Lowassa, na Chenge ni mafisadi,
Bangusilo hasahasa, naye tukampa kadi,
Kila mtu mwenye kosa, jina hili tunanadi,
Fisadi ni mtu gani, nani atanijulia!

Vidole vinaniuma, kuchapa sasa nakoma,
Mkono washika tama, kichwa changu chaniuma,
Swali langu nalituma, kaditamati na tama,
Fisadi ni mtu gani, mimi nawaulizia!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
 
FISADI NI MTU GANI?

Asiyependa shauri, mgumu kushaurika,
Kutwa ni mtu wa shari, hapendi kukosoleka,
Anofura kwa jeuri, na ndita imekunjika,
Fisadi ni mtu gani, mashaka yameingia!

!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)

Fisadi ano fikra, asemalo yeye sawa
Fisadi huyu akera, hataki kuwekwa sawa
Hujiona anang'ara, kumbe ubabe kajawa
Fisadi ni ajionae, yu bora kuliko wenziwe

Fisadi wa madhila, hapendi kuwa mkweli
Fisadi tetea hila, hata kama yu kafeli
Fisadi anazo mila, ajifanya baradhuli
Fisadi hana heshima, ni vyema kumuepuka
 
...Niliwahi kusikia mtu anaeiba wake za watu ndio fisadi kwa hiyo hawa majamaa yanayoiba mali za nchi yetu ni fisadi x1000 kabisa au sio??
 
mama asante kwa maana hiyo.. inaonekana mafisadi wako wengi...

MwanaK wako wengi sana, mimi, wewe na kila mtu ajichunguze mwenyewe na tukigundua ufisadi wetu basi tujirekebishe na tuombe radhi. Ufisadi mkubwa ni wizi wa aina yeyote i.e mke, mume, mali, haki miliki na kubwa ya yote ni wizi wa mali ya umma.
 
Hilo neno umeongea mama....kwani kuna dhambi kubwa na ndogo??? Dhambi ni dhambi tu???
 
Hilo neno umeongea mama....kwani kuna dhambi kubwa na ndogo??? Dhambi ni dhambi tu???

Dhambi ni dhambi kwa kweli, kinachotufautisha uzito wa dhambi ni adhabu inayotolewa na hivyo kuweza kusema hii ni dhambi kubwa (ina adhabu kubwa na hii ni dhambi ndogo ina adhabu ndogo). So ufisadi ni ufisadi lakini nao unatofauti hivyo hivyo. Cha umuhimu ni kuupiga vita ud´fisadi wa aina yeyote. Ufisadi mdogo mdogo tuupige vita ya nguvu kwa ukiachiliwa huzaa ufisadi mkubwa. Mkapa alianza kidogo kidogo 2000 na ilipofika 2005 alikuwa ni fisadi mkubwa.
 
Fisadi ano fikra, asemalo yeye sawa
Fisadi huyu akera, hataki kuwekwa sawa
Hujiona anang'ara, kumbe ubabe kajawa
Fisadi ni ajionae, yu bora kuliko wenziwe

Fisadi wa madhila, hapendi kuwa mkweli
Fisadi tetea hila, hata kama yu kafeli
Fisadi anazo mila, ajifanya baradhuli
Fisadi hana heshima, ni vyema kumuepuka

Mama!

I like how you flow!
 
Ni Mkiuka UTU na UBINAADAMU kwa kutumia mental force kama afanyavyo jambazi kwa kutumia physical force.

Jambazi anakiuka utu na ubinaadamu kwa kutumia maguvu,misuli, silaha za mapaga, bunduki, nk kufikia lengo lake.... .

Mara nyingi Fisadi = Jambazi anayetumia AKILI, Elimu na maarifa kukikuka UTU,UBINAADAMU NA KUKIUKA MAADILI ya jamii!

Mara nyingi FISADI anatumia silaha ya "KALAMU" tu!
 
Karibu watu wengi hapa Jamvini wana misimamo tofauti katika suala zima la kuweka nchi katika mstari. unaweza kujua hilo kwa kusoma sahihi zao ambazo uwa chini ya mabandiko yao.

Kwa mfano sahihi hii nimevutiwa sana nao na inabeba ujumbe mzito sana na hali halisi ya Tz ya leo..Fisadi hakuzaliwa fisadi, ila aweza kufa fisadi!

Ukiangalia kwa kina kauli hii ya MKJJ ina mantiki sana, na ni vema ikajadiliwa na kuona ni jinsi gani system inaweza kumbadilisha mtu... Haya hayapo TZ pekee bali katika ulimwengu mzima wa siasa...
 
Last edited:

Nakubaliana na wewe kuwa Mafisadi hawazaliwi mafisadi!
 
Karibu watu wengi hapa Jamvini wana misimamo tofauti katika suala zima la kuweka nchi katika mstari. unaweza kujua hilo kwa kusoma sahihi zao ambazo uwa chini ya mabandiko yao.

Kwa mfano sahihi hii nimevutiwa sana nao na inabeba ujumbe mzito sana na hali halisi ya Tz ya leo..Fisadi hakuzaliwa fisadi, ila aweza kufa fisadi!

Ukiangalia kwa kina kauli hii ya MKJJ ina mantiki sana, na ni vema ikajadiliwa na kuona ni jinsi gani system inaweza kumbadilisha mtu... Haya hayapo TZ pekee bali katika ulimwengu mzima wa siasa...

wat about ur signature???? kama tuki-save maji na tukawa tunakunywa mvinyo si ndio taifa litakuwa limejaa walevi,matokeo yake tutakuwa tunachagua viongozi KILEVI LEVI ama vp??? ehhhh hatujalewa tupo makini hali unaona inavyoenda MZOBE MZOBE,sikwambii sote tukiwa walevi,hapo si patakuwa hapatoshi.
weekend njema.
 
kabla ya kuangalia sahihi yangu hebu changia mada
 
Kibunango,

Ktk kipindi hiki cha mpito kwa watanzania tutashuhudia mambo mengi yakitokeaa ila sasa haya ya mafisadi mbona yaibuke kwa sasa na wala si 2004 au na 2005? jawabu ni kwamba tayari neno ufisadi litapotea muda si mrefu, hivi karibuni tutasikia kilimo bora, viwanda na mengineyo, ilimradi tu tukijipanga.
 
Neno linaweza kupungua kasi, lakini bado ninajiuliza ni kwa namna gani system inaweza kumbadilisha mtu na kuwa fisadi..
 
Back
Top Bottom