Fisadi ni Mtu anayechukua wake za watu?

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Wajameni naomba kufafanuliwa hili neno FISADI! hapo nyuma tumesikia kua ufisadi ni ubadhirifu wa mali za umma au kujilimbikizia mali kwa njia isiyo halali, lakini hapa karibuni tumemsikia mkubwa mmoja pale Dodoma akidai kua anavyoelewa yeye FISADI ni mtu anayechukua wake za watu jamani naombeni maana ya neno kamili kuhusu FISADI au UFISADI!:help:
 
Kwenye kamusi ya Kiswahili - English ni 'seducer, immoral person'. Kwenye Oxford dictionary 'immoral' maanake "not within society's standards of acceptable, honest and moral behaviour; morally wrong". Halafu 'graft' maanake ni "US the act of getting money or advantage through the dishonest use of political power and influence". Mfano 'The whole government was riddled with graft, bribery, and corruption.'

Sasa angalia maana ya immoral na graft unaona ndani yake kuna dishonest. Na fisadi ni dishonest guy. Nafikiri lina maana zaidi ya moja Spika alitumia ile ya 'seducer' na wengine wanatumia ya pili 'immoral person'. Makinda alitakiwa kufahamu maana zote na kuangalia 'context' sio kukurupuka tu.
 
Nakushukuru sana Mwanamayu:whoo:
 
Bado maana ya seducer haipo kama Makinda alivyotaka tuamini!!! Makinda alisema ni anayechukua wake za watu, ila meaning ya hapo chini as per Cambridge Advanced Learner Dictionery, inazungumzia kitu different.

seduce (PERSUADE) /sI"dju:s/ US /-"du:s/ verb [T]
to persuade someone to have sex with you, often someone younger than you, who has little experience of sex:
Pete lost his virginity at 15 when he was seduced by his best friend's mother.
seducer /sI"dju:.s@r/ US /-"du:.s@`/ noun [C]
someone who seduces people:
The play tells the story of a fabulously wealthy woman who seeks revenge on her heartless seducer.
seductress /sI"dVk.tr@s/ noun [C]
a female seducer
seduction /sI"dVk.S@n/ noun [C or U]
The film depicts Charlotte's seduction by her boss.
seductive /sI"dVk.tIv/ adjective
It was a seductive black evening dress.
She gave him a seductive look.
seductively /sI"dVk.tIv.li/ adverb
seductiveness /sI"dVk.tIv.n@s/ noun

Nakushukuru sana Mwanamayu:whoo:
 
Si sahihi hata kidogo kutafsiri neno Fisadi kwa kuangalia maana yake kwenye Kiingereza (kwa kutumia Swahili-English dictionary) halafu upate maneno hayo tena ubadilishe kutoka English kuja kwenye kiswahili. Ukiangalia neno "Kidogo"utapata maneno mengi kwa kiingereza ikiwa ni pamoja na small, infinitesimal, little, less, minute, n.k. Sasa ukichukua minute kwa kiingereza kwenye kiswahili ina maana mbili: "dakika" na 'kidogo". Kwa utaratibu huu, utaishia kusema neno "kidogo' maana yake "dakika"

Njia ya uhakika ni kuangalia neno Fisadi kwenye kamusi ya Kiswahili-Kiswahili.
 
Ukishatoa hiyo maana unaandika hivi according to Makinda (2010) inakua imetulia when it comes to referencing, kwa hio according to yeye hio ndio maana yake, na yeye anaechukua viserebgeti boyz kama nanihiii, nai yule, yule mbunge ambaye sasa ni mwizi-ri wa dept flani.....
 
ninavyo fahamu mimi neno fisadi limetokana na neno la kiarabu(FASIDI) likiwa na maana kufanya uharibifu ,

Qur-an 2:11"
Na wanapo ambiwa:Msifanye ufisadi ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji"
When it is said to them: "Make not mischief on the earth," they say: "Why, we only want to make peace.
 
Back
Top Bottom