Fisadi Manji anavyomtumia mwekezaji wa Kiingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fisadi Manji anavyomtumia mwekezaji wa Kiingereza

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kiranja, Nov 1, 2011.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mgogoro wa mashamba ya Sileverdale na Mbono ni muendelezo wa mchakato mchafu wa fisadi Yusuf Manji wa kutaka kumchafua Reginald Mengi. Kwanza ni vyema tukafahamu yafuatayo:
  1. Mashamba hayo yanazungumzwa katika hicho kinachoitwa mgogoro yako wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro. Haya mashamba asili yake ni mali ya wanakijiji wanaozunguka eneo hilo kupitia vyama vyao vitatu vya ushirika. Benjamin Mengi aliingia mkataba na wanakijiji kukodisha kwa miaka 60 kwa kodi ambayo analipa kila mwaka, pamoja na masharti mengine ya kutokukata miti na kupanda kahawa kwa masharti maalumu.
  2. Huyo mzungu David Stewart Middleton alikuja Tanzania na kuajiriwa wa Benjamin Mengi katika kampuni ya Alpha Tobacco Tanzania Limited. Alpha ilikua ikifanya majaribio ya kupanda Genetic Modified tobacco katika shamba la Benjamin Mengi la Silverdale. Mzungu huyo alikuwa akilipwa mshahara wa sh 500,000 kwa mwezi na alikuwa akikaa kwenye nyumba ya Benjamin Mengi ndani ya eneo la mashamba hayo akiwa na mkewe Sarah Hamittage. Mradi wa GM Tobacco ulipigwa vita na Bodi ya Tumbaku na kamati za Bunge, na hatimaye ikabidi usitishwe huku Benjamin Mengi akiwa ameingia hasara kubwa.
  3. Baada ya kusitishwa kwa majaribio ya GM tobacco Mzungu huyo alimshauri Benjamin Mengi wafanye mradi wa kuyalima mashamba hayo kwa kupanda mazao mengine kama kahawa na kwamba angepata mtaji mkubwa kwa kazi hiyo kutoka vyanzo vingine. Benjamin Mengi alikubaliana na ushauri huo kwa kuingia ubia katika biashara hiyo na ikizingatiwa wakati huo alikuwa akiuguliwa na marehemu mke wake (saratani), hali ambayo ingemlazimu kusafiri nje ya nchi mara kwa mara kwa matibabu ya mkewe. Aliona ni vyema akapata mshiriki katika kazi.
  4. David Stewart Middleton na mke wake Sarah walitayarisha mikataba na kampuni mpya yenye jina la Silverdale Farm Limited ambako David Stewart Middleton akiwa na hisa saba (7) na Benjamin Mengi akiwa na hisa tatu (3) na wote wakiwa wakurugenzi. Sarah Hamittage ambaye ni mwanasheria alioyesajiliwa Uingereza vile alitayarisha hati ya makabidhiano ambayo ilihamisha maslahi ya kampuni ya Benjamin Mengi iitwayo Fiona (T) Limited, kwenda kampuni mpya ya Silverdale. Maelewano kwa ujumla ilikuwa kwamba Fiona ingehamisha ukodishaji wake wa mashamba hayo kwa kampuni ya ubia ya Silverdale na Fiona ingelipwa fedha za jumla kama fidia ya kuhamisha umiliki wakati huo huo Silverdale ikitakiwa (kimkataba) kuwa kampuni ya ubia kati ya Mzungu huyo na Mtanzania (Benjamin Mengi). Benjamin alitakiwa pia kulipwa Dola za Marekani 2,000 kwa mwezi, ambazo zingekuja kupunguzwa kwenye gawiwo lake la faida ya mwaka.
  5. Benjamin Mengi alikabidhi shamba hilo pamoja na kwamba David Stewart Middleton alikua hajamaliza kulipa malipo ya uhamishaji wa hisa kama ilivyotakiwa katika mkataba.
  6. Matatizo yalianza kujitokeza pale Benjamin Mengi alipokuja kudai fedha zilizosalia katika mkataba wao na stahiki zake za Dola za Marekani 2,000 kwa mwezi. David Stewart Middleton alikuwa mzito kulipa fedha hizo, kiasi cha kutoa hundi ambayo ilirudishwa na benki (bounce cheque). Hali ilizidi kuwa mbaya pale David Stewart Middleton alipodiriki kufanya mkutano wa Bodi ya Wakurengenzi ya kampuni ya Silverdale na kumtoa Benjamin Mengi kama mkurugenzi na kuhamisha maslahi ya kampuni hiyo katika mashamba kwenye kampuni ya Songwe Estates amabayo inamilikiwa na David Stewart Middleton na mke wake Sarah. Benjamin Mengi alipomkabili David Stewart Middleton alikiri kwa maandishi kwamba amefanya kosa na kwamba hatarudia tena kumsaliti mwenyeji wake (Benjamin Mengi). Lakini tofauti na ahadi yake David Stewart Middleton aliendeleza malumbano kwa
  a. Kupeleka nyaraka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) za kumtoa Benjamin Mengi katika ukurugenzi wa kampuni yao ya Silverdale.
  b. Kuwarubuni viongozi wa Vyama vya ushirika wamtambue yeye kama mmliki mpya wa mashamba. David Stewart Middleton alifikia kuwashawishi viongozi hao kutoa matangazo kwenye magazeti
  c. Kukataa katakata kumlipa Benjamin Mengi na kampuni yake kama walivyo kubaliana katika mikataba yao.
  d. Kumzuia Benjamin Mengi asiingie katika mashamba hayo.
  7. Matokeo yake ni kwamba malumbano hayo yanaendelea hadi leo huku kukiwa bado kuna kesi kadhaa Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Moshi. David Stewart Middleton ambaye ndiye aliyeanzisha malumbano hayo alikwishakimbia nchini toka mwaka 2004 na kurudi kwao Uingereza.
  8. David Stewart Middleton na mke wake siyo wawekezaji halali kwasababu:
  a. Hawakufikia kiwango cha chini kilicho wekwa kisheria kwa mtu kujulikana kama mwekezaji amabacho ni Dola za Merakani 200,000 yeye aliwekeza Pauni za Uingereza 60,000 tu ambazo hazifikii kiwango hicho cha kuitwa mwekezaji chini ya Sheria ya Uwekezaji Nchini inayosimamiwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania- Investment Centre (TIC).
  b. Mradi wake na Benjamin Mengi haukusajiliwa na Tanzania Kituo hicho cha Uwekezaji (TIC).
  c. Chini ya sheria ya Ardhi mtu ambaye siyo wa Tanzania raia hawezi kumiliki ardhi isipokuwa pale tu atakapo kuwa amesajiliwa kama mwekezaji. Kwasababu Silverdale (T) Limited ilikuwa ni kampuni ambayo zaidi ya asilimia hamsini ya hisa zake zinamilikiwa na mtu ambaye siyo raia basi ilikuwa haina budi kupata usajili na kinyume chake umiliki wa kampuni ya Siliverdale juu ya mashamba ya Silverdale na Mbono ni batili.
  8. Reginald Mengi aliingia kwenye suala hili mnamo Desemba 2005 baada ya kuombwa na aliyekuwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania. Aliaanza kwa kuwasikiliza David Stewart Middleton na Balozi Pocock nyumbani kwake Reginald Mengi na baada ya hapo aliwaahidi kwamba angejitahiidi kadri ya uwezo wake kulimaliza suala hilo kwa njia ya amani. Akiwa mkweli kwa ahadi yake alizungumza na Benjamin Mengi ambaye baada ya kushawishiwa sana alikubali kwamba mahusiano yarudi kama yalivyo kwenye mikataba yalioingiwa kati yake na David Stewart Middleton. Reginald Mengi alifikisha ujumbe huo kwa David Stewart Middleton, lakini David Stewart Middleton hakupendezwa na pendekezo hayo na badala yake alisisitiza msimamo wake wa kutaka kumiliki mashamba peke yake bila ya mbia mwenzake Benjamin Mengi. Baada ya kuona hivyo Reginald Mengi aliachana na suala hilo.
  9. Reginald Mengi hahusiki kwa vevote vile na jambo hili zaidi ya nia nzuri aliyoonyesha ya kutaka kulimaliza mgogoro kwa amani.
  10. Kuhusishwa kwa Reginald Mengi na suala la mashamba haya kumeaanza mwishoni mwaka 2008 baada ya Sarah Hermitage kuanza kuandika barua pepe na kupost mara nyingi kwenye website yake. Kilichojificha nyuma ya huyu Mama ni:
  a. Ameingia kwenye njama na Yusuf Manji kumchafua Reginald Mengi. Yusuf Manji kwa upande wake anamsaidia Sarah Hermitage fedha na information mbalmbali.
  b. Mama huyu anatumia hali hiyo kama fursa ya kumlazimisha (blackmail) alipwe fedha na Reginald Mengi.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Yule sio mwekezaji, ni mwezaji
   
 3. m

  makongo Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  sasa manji anapata faida gani out of this?
   
 4. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,000
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu Mengi ni mmiliki wa magazeti yaliyoweka ufisadi wa Manji hadharani.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tuwe waangalifu sana tunapowakaribisha "wawekezaji." Hasa katika kilimo.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kati ya vitu vyote kwenye sakata hili ni jinsi gani huyu mzungu anawachukulia Watanzania; yaani jamaa anajitahidi kutumia nguvu za serikali yake kuwatisha wawekezaji kuja nchini na kutupa lawama kwa vyombo vyote vya utawala nchini kwa sababu havikumsaidia yeye mwekezaji Mwingereza. Hili bado sijalielewa vizuri ni kwanini..
   
 7. T

  Tom JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzungu huyu ni dhahiri anawadharau waTZ, yaani sisi watu wa kupelekwa-pelekwa tu.

  Hata hivyo mimi naona strategy ya mzungu hakuna makosa na madai ya Mengi nayo ni sawa - MANJI kama ni kweli kaamua kumchafua Mengi, basi labda kibiashara anafaidika ndio maana kaamua kufanya hivyo - naye yupo sawa. Hamna mbaya hapa, maana haya yote ni USHINDANI wa kibiashara. Kusema ni halali ama si halali, Mahakama ndio iamue AMA WAHUSIKA WENYEWE wakae kitako wayaweke mambo sawa, au kama Mengi hawezi mapigo na amwachie Mzungu mashamba ama na amuuzie Manji biashara zake nk.

  Shrewdness ktk biashara ni muhimu hivyo namchukulia mwingereza amekua ana fight ku-win hayo mashamba kisheria, sasa kusema alikua morally wrong or right hicho ni kitu kingine kabisa. Pia ni investor wengi, awe toka India, China, Uingereza etc (hata ungekua wewe) watapenda kutumia mteremko, ushawishi ama na intimidation ya serikali za nchi zao kwa nchi yetu ili wafanikiwe kuwekeza (wafaidike) hapa kwetu. Cha muhimu ni serikali yetu kusimamia vema sheria na maslahi ya MTANZANIA hasa kua na Mahakama imara na sheria zilizojitosheleza.
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  siwapendi hawa wazungu wanaojiita wawekezaji!
   
 9. s

  sanjo JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  It is a daylight looting suppported by arrogance and institutionalised investment protections.
   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tatizo la wazungu ni kutudharau Watanzania na hasa kwa kuwa kuina wakati wakubwa wetu wanawaabudu sana. Tuwe kama Kenya
   
 11. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  To bring in fisadi Manji into this saga is to divert our attention from the real issue at hand; Benjamin Mengi is a man of questionable integrity as exemplified by his taking a loan from [NICOL] poor peoples investments and in no time declaring bankruptcy of his Moshi pharmaceutical company.!! How can you trust a story told by a man who is so audacious as to steal in broad daylight from people who hardly can afford a meal a day.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nina imani kuwa mzungu huyo ni maskini tu huko kwao. Alishindwa kulipa dola 120,000 kwa kipndi cha miezi sita! Halafu anajiita mwekezaji!!
   
Loading...